< Zaburi 105 >

1 Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake, wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda.
Mshukuruni Yahwe, liitieni jina lake; myafanye matendo yake yajulikane kati ya mataifa.
2 Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa, waambieni matendo yake yote ya ajabu.
Mwimbieni yeye, mwimbieni sifa yeye; semeni matendo yake yote ya ajau.
3 Lishangilieni jina lake takatifu, mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi.
Mjivune katika utakatifu wa jina lake; moyo wao wamtafutao Yahwe ufurahi.
4 Mtafuteni Bwana na nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote.
Mtafuteni Yahwe na nguvu zake; utafuteni uwepo wake siku zote.
5 Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka,
Kumbukeni mambo ya ajabu aliyoyatenda,
6 enyi wazao wa Abrahamu mtumishi wake, enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
miujiza yake na amri zitokazo kinywani mwake, enyi kizazi cha Ibrahimu mtumishi wake, enyi watu wa Yakobo, wachaguliwa wake.
7 Yeye ndiye Bwana Mungu wetu, hukumu zake zimo duniani pote.
Yeye ni Yahwe, Mungu wetu. Amri zake ziko juu ya nchi yote.
8 Hulikumbuka agano lake milele, neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu,
Naye hulikumbuka agano lake milele, neno alilo amuru kwa ajili ya vizazi elfu.
9 agano alilolifanya na Abrahamu, kiapo alichomwapia Isaki.
Hulikumbuka agano alilolifanya na Ibrahimu na kiapo alicho mwapia Isaka.
10 Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri, kwa Israeli liwe agano la milele:
Hiki ndicho alicho mthibitishia Yakobo kama agano na kama agano la milele kwa Israeli.
11 “Nitakupa wewe nchi ya Kanaani kuwa sehemu utakayoirithi.”
Alisema, “Nitakupa wewe ardhi ya Kanaani kama sehemu yako ya urithi.”
12 Walipokuwa wachache kwa idadi, wachache sana na wageni ndani yake,
Alisema hili wakati tu walipokuwa wachache katika hesabu, yaani wachahe sana, nao walikuwa wageni katika nchi.
13 walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine, kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.
Walienda taifa hadi taifa na kutoka ufalme moja kwenda mwingine.
14 Hakuruhusu mtu yeyote awaonee; kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema:
Hakuruhusu yeyote kuwaonea; aliwakemea wafalme kwa ajili yao.
15 “Msiwaguse niliowatia mafuta; msiwadhuru manabii wangu.”
Alisema, “Msiwaguze wapakwa mafuta wangu, na msiwadhuru manabii wangu.”
16 Akaiita njaa juu ya nchi na kuharibu chakula chao chote,
Aliita njaa katika nchi; akaondoa upatikanaji wa mkate wote.
17 naye akatuma mtu mbele yao, Yosefu, aliyeuzwa kama mtumwa.
Akatuma mtu mbele yao; Yusufu aliuzwa kama mtumishi.
18 Walichubua miguu yake kwa minyororo, shingo yake ilifungwa kwa chuma,
Miguu yake ilifungwa kwa pingu; alivishwa mnyororo wa chuma shingoni mwake,
19 hadi yale aliyotangulia kusema yalipotimia, hadi neno la Bwana lilipomthibitisha.
mpaka wakati wa maneno yake ulipotimia, nalo neno la Yahwe lilimjaribu.
20 Mfalme alituma watu wakamfungua, mtawala wa watu alimwachia huru.
Mfalme alituma watumishi kumfungua; mtawala wa watu alimuweka huru.
21 Alimfanya mkuu wa nyumba yake, mtawala juu ya vyote alivyokuwa navyo,
Alimuweka kuwa msimamizi wa nyumba yake kama mtawala wa mali zake zote
22 kuwaelekeza wakuu wa mfalme apendavyo na kuwafundisha wazee wake hekima.
kuwaelekeza wakuu kama alivyopenda na kuwafundisha viongozi wake hekima.
23 Kisha Israeli akaingia Misri, Yakobo akaishi kama mgeni katika nchi ya Hamu.
Kisha Israeli iliingia Misri, na Yakobo aliishi kwa muda katika nchi ya Hamu.
24 Bwana aliwafanya watu wake kuzaana sana, akawafanya kuwa wengi sana kuliko adui zao,
Yahwe aliwajalia watu wake wazae sana, na aliwafanya wenye nguvu kuliko adui zao.
25 ndiye aliigeuza mioyo yao iwachukie watu wake, wakatenda hila dhidi ya watumishi wake.
Alisababisha adui zao wawachukie watu wake, na kuwatendea visivyo watumishi wake.
26 Akamtuma Mose mtumishi wake, pamoja na Aroni, aliyemchagua.
Alimtuma Musa, mtumishi wake, na Haruni, ambaye alikwisha mchagua.
27 Walifanya ishara zake za ajabu miongoni mwao, miujiza yake katika nchi ya Hamu.
Walifanya ishara zake kati ya Wamisri na maajabu yake katika ya nchi ya Hamu.
28 Alituma giza na nchi ikajaa giza, kwani si walikuwa wameyaasi maneno yake?
Alituma giza na likaifanya nchi hiyo kuwa giza, lakini watu wake hawakutii amri zake.
29 Aligeuza maji yao kuwa damu, ikasababisha samaki wao kufa.
Aligeuza maji kuwa damu na aliua samaki wao.
30 Nchi yao ilijaa vyura tele, ambao waliingia hadi kwenye vyumba vya kulala vya watawala wao.
Nchi yao ilijaa vyura, hata katika vyumba vya watawala wao.
31 Alisema, yakaja makundi ya mainzi, na viroboto katika nchi yao yote.
Alisema, na makundi ya inzi na chawa wakaja mjini mwote.
32 Alibadilisha mvua yao ikawa mvua ya mawe, yenye umeme wa radi nchini yao yote,
Aliigeuza mvua yao kuwa mvua ya mawe, pamoja na miali ya moto juu ya ardhi yao.
33 akaharibu mizabibu yao na miti ya tini, na akaangamiza miti ya nchi yao.
Aliiharibu mizabibu yao na mitini yao; akaivunja miti ya mji wao.
34 Alisema, nzige wakaja, tunutu wasio na idadi,
Alisema, na nzige wakaja, nzige wengi sana.
35 wakala kila jani katika nchi yao, wakala mazao ya ardhi yao.
Nzige walikula mboga zao zote za majani katika nchi yao. Walikula mazao yote ardhini.
36 Kisha akawaua wazaliwa wote wa kwanza katika nchi yao, matunda ya kwanza ya ujana wao wote.
Aliua kila mzaliwa wa kwanza katika nchi yao, malimbuko ya nguvu zao.
37 Akawatoa Israeli katika nchi wakiwa na fedha na dhahabu nyingi, wala hakuna hata mmoja kutoka kabila zao aliyejikwaa.
Aliwatoa nje Waisraeli wakiwa na fedha na dhahabu; hakuna mmoja wa kabila lake aliyejikwaa njiani.
38 Misri ilifurahi walipoondoka, kwa sababu hofu ya Israeli ilikuwa imewaangukia.
Misri ilifurahi walipoondoka, maana Wamisri waliwaogopa.
39 Alitandaza wingu kama kifuniko, na moto kuwamulikia usiku.
Alitandaza wingu liwafunike na alifanya moto uwaangazie wakati wa usiku.
40 Waliomba, naye akawaletea kware, akawashibisha kwa mkate wa mbinguni.
Waisraeli waliomba chakula, naye aliwaletea kware na aliwatosheleza kwa mkate kutoka mbiguni.
41 Alipasua mwamba, maji yakabubujika, yakatiririka jangwani kama mto.
Aliugawa mwamba, maji yalimwagika kutoka humo; yalitiririka katika jangwa kama mto.
42 Kwa maana alikumbuka ahadi yake takatifu, aliyompa Abrahamu mtumishi wake.
Kwa maana alikumbuka ahadi yake takatifu aliyoifanya kwa Ibrahimu mtumishi wake.
43 Aliwatoa watu wake kwa furaha, wateule wake kwa kelele za shangwe,
Aliwaongoza watu wake kwa furaha, wateule wake kwa kelele za ushindi.
44 akawapa nchi za mataifa, wakawa warithi wa mali wengine walikuwa wameitaabikia:
Aliwapa nchi za mataifa; walichukua milki ya mali za watu
45 alifanya haya ili wayashike mausia yake na kuzitii sheria zake. Msifuni Bwana.
ili waweze kushika amri zake na kutii sheria zake. Msifuni Yahwe.

< Zaburi 105 >