< Zaburi 101 >

1 Zaburi ya Daudi. Nitaimba juu ya upendo wako na haki yako; kwako wewe, Ee Bwana, nitaimba sifa.
לדוד מזמור חסד ומשפט אשירה לך יהוה אזמרה׃
2 Nitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama: utakuja kwangu lini? Nitatembea nyumbani mwangu kwa moyo usio na lawama.
אשכילה בדרך תמים מתי תבוא אלי אתהלך בתם לבבי בקרב ביתי׃
3 Sitaweka mbele ya macho yangu kitu kiovu. Ninayachukia matendo ya watu wasio na imani; hawatashikamana nami.
לא אשית לנגד עיני דבר בליעל עשה סטים שנאתי לא ידבק בי׃
4 Moyo wa ukaidi utakuwa mbali nami; nitajitenga na kila ubaya.
לבב עקש יסור ממני רע לא אדע׃
5 Kila amsingiziaye jirani yake kwa siri, huyo nitamnyamazisha; mwenye macho ya dharau na moyo wa kiburi huyo sitamvumilia.
מלושני בסתר רעהו אותו אצמית גבה עינים ורחב לבב אתו לא אוכל׃
6 Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi, ili waweze kuishi pamoja nami; yeye ambaye moyo wake hauna lawama atanitumikia.
עיני בנאמני ארץ לשבת עמדי הלך בדרך תמים הוא ישרתני׃
7 Mdanganyifu hatakaa nyumbani mwangu, yeye asemaye kwa uongo hatasimama mbele yangu.
לא ישב בקרב ביתי עשה רמיה דבר שקרים לא יכון לנגד עיני׃
8 Kila asubuhi nitawanyamazisha waovu wote katika nchi; nitamkatilia mbali kila mtenda mabaya kutoka mji wa Bwana.
לבקרים אצמית כל רשעי ארץ להכרית מעיר יהוה כל פעלי און׃

< Zaburi 101 >