< Zaburi 100 >

1 Zaburi ya shukrani. Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote.
Mpigieni Yahwe kelele za furaha, enyi nchi yote.
2 Mwabuduni Bwana kwa furaha; njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.
Mtumikieni Yahwe kwa furaha; njoni mbele zake mkiimba kwa furaha.
3 Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu. Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake; sisi tu watu wake, kondoo wa malisho yake.
Mjue kuwa Yahwe ni Mungu; alituumba, na sisi tu wake. Tu watu wake na kondoo wa malisho yake.
4 Ingieni malangoni mwake kwa shukrani na katika nyua zake kwa kusifu, mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.
Ingieni malangoni mwake kwa shukrani na nyuani mwake kwa kusifu. Mshukuruni yeye na litukuzeni jina lake.
5 Kwa maana Bwana ni mwema na upendo wake wadumu milele; uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.
Maana Yahwe ni mwema; uaminifu wa agano lake wadumu milele na uaminifu wake vizazi na vizazi vyote.

< Zaburi 100 >