< Zaburi 100 >

1 Zaburi ya shukrani. Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote. 2 Mwabuduni Bwana kwa furaha; njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe. 3 Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu. Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake; sisi tu watu wake, kondoo wa malisho yake. 4 Ingieni malangoni mwake kwa shukrani na katika nyua zake kwa kusifu, mshukuruni yeye na kulisifu jina lake. 5 Kwa maana Bwana ni mwema na upendo wake wadumu milele; uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.

< Zaburi 100 >