< Zaburi 10 >

1 Kwa nini, Ee Bwana, unasimama mbali? Kwa nini unajificha wakati wa shida?
耶和华啊,你为什么站在远处? 在患难的时候为什么隐藏?
2 Katika kiburi chake, mwovu humtesa maskini, waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga.
恶人在骄横中把困苦人追得火急; 愿他们陷在自己所设的计谋里。
3 Hujivunia tamaa za moyo wake; humbariki mlafi na kumtukana Bwana.
因为恶人以心愿自夸; 贪财的背弃耶和华,并且轻慢他。
4 Katika kiburi chake, mwovu hamtafuti Mungu, katika mawazo yake yote hakuna nafasi ya Mungu.
恶人面带骄傲,说:耶和华必不追究; 他一切所想的都以为没有 神。
5 Njia zake daima hufanikiwa; hujivuna na amri zako ziko mbali naye, huwacheka kwa dharau adui zake wote.
凡他所做的,时常稳固; 你的审判超过他的眼界。 至于他一切的敌人, 他都向他们喷气。
6 Anajisemea mwenyewe, “Hakuna kitakachonitikisa, daima nitakuwa na furaha, kamwe sitakuwa na shida.”
他心里说:我必不动摇, 世世代代不遭灾难。
7 Kinywa chake kimejaa laana, uongo na vitisho; shida na ubaya viko chini ya ulimi wake.
他满口是咒骂、诡诈、欺压, 舌底是毒害、奸恶。
8 Huvizia karibu na vijiji; kutoka mafichoni huwanasa wasio na hatia, akivizia wapitaji.
他在村庄埋伏等候; 他在隐密处杀害无辜的人。 他的眼睛窥探无倚无靠的人;
9 Huvizia kama simba aliye mawindoni; huvizia kumkamata mnyonge, huwakamata wanyonge na kuwaburuza katika wavu wake.
他埋伏在暗地,如狮子蹲在洞中。 他埋伏,要掳去困苦人; 他拉网,就把困苦人掳去。
10 Mateka wake hupondwa, huzimia; wanaanguka katika nguvu zake.
他屈身蹲伏, 无倚无靠的人就倒在他爪牙之下。
11 Anajisemea mwenyewe, “Mungu amesahau, huficha uso wake na haoni kabisa.”
他心里说: 神竟忘记了; 他掩面永不观看。
12 Inuka Bwana! Inua mkono wako, Ee Mungu. Usiwasahau wanyonge.
耶和华啊,求你起来! 神啊,求你举手,不要忘记困苦人!
13 Kwa nini mtu mwovu anamtukana Mungu? Kwa nini anajiambia mwenyewe, “Hataniita nitoe hesabu?”
恶人为何轻慢 神, 心里说:你必不追究?
14 Lakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni, umekubali kuyapokea mkononi mwako. Mhanga anajisalimisha kwako, wewe ni msaada wa yatima.
其实你已经观看; 因为奸恶毒害,你都看见了, 为要以手施行报应。 无倚无靠的人把自己交托你; 你向来是帮助孤儿的。
15 Vunja mkono wa mtu mwovu na mbaya, mwite atoe hesabu ya maovu yake ambayo yasingejulikana.
愿你打断恶人的膀臂; 至于坏人,愿你追究他的恶,直到净尽。
16 Bwana ni Mfalme milele na milele, mataifa wataangamia watoke nchini mwake.
耶和华永永远远为王; 外邦人从他的地已经灭绝了。
17 Unasikia, Ee Bwana, shauku ya wanaoonewa, wewe huwatia moyo, na kusikiliza kilio chao,
耶和华啊,谦卑人的心愿, 你早已知道。 你必预备他们的心, 也必侧耳听他们的祈求,
18 ukiwatetea yatima na walioonewa, ili mwanadamu, ambaye ni udongo, asiogopeshe tena.
为要给孤儿和受欺压的人伸冤, 使强横的人不再威吓他们。

< Zaburi 10 >