< Zaburi 1 >

1 Heri mtu yule ambaye haendi katika shauri la watu waovu, wala hasimami katika njia ya wenye dhambi, au kuketi katika baraza la wenye mizaha.
Amebarikiwa mtu yule asiye enenda katika ushauri wa waovu, au kusimama katika njia ya wenye dhambi, au kukaa katika kusanyiko la wenye mizaha.
2 Bali huifurahia sheria ya Bwana, naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana.
Bali yeye huifurahia sheria ya Yahwe, na huitafakari sheria yake mchana na usiku.
3 Mtu huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao huzaa matunda kwa majira yake na majani yake hayanyauki. Lolote afanyalo hufanikiwa.
Atakuwa kama mti uliopandwa karibu na mkondo wa maji ambao huzaa matunda yake kwa majira yake, ambao majani yake hayakauki; lolote afanyalo litafanikiwa.
4 Sivyo walivyo waovu! Wao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
Waovu hawako hivyo, wao badala yake ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
5 Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu, wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.
Kwa hivyo waovu hawatasimama katika hukumu, wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.
6 Kwa maana Bwana huziangalia njia za mwenye haki, bali njia ya waovu itaangamia.
Kwa kuwa Yahweh huikubali njia ya wenye haki, njia ya waovu itaangamizwa.

< Zaburi 1 >