< Mithali 5 >
1 Mwanangu, sikiliza kwa makini hekima yangu, sikiliza vizuri maneno yangu ya busara,
Mwanangu, zingatia hekima yangu; sikiliza kwa makini ufahamu wangu,
2 ili uweze kutunza busara na midomo yako ihifadhi maarifa.
ili ujifunze busara na midomo yako iweze kuhifadhi maarifa.
3 Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba hudondoza asali, na maneno ya kinywa chake ni laini kuliko mafuta;
Maana midomo ya malaya hutiririsha asali na kinywa chake ni laini kuliko mafuta,
4 lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo, mkali kama upanga ukatao kuwili.
lakini mwishoni anakuwa mchungu kama mnyoo, hukata kama upunga mkali.
5 Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo; hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini. (Sheol )
Miguu yake huelekea mauti; hatua zake huelekea njia yote ya kuzimu. (Sheol )
6 Yeye hafikiri juu ya njia ya uzima; njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui.
Hafikirii njia ya uzima. Hatua za miguu yake hupotea, maana hajui anakwenda wapi.
7 Sasa basi wanangu, nisikilizeni; msiache ninalowaambia.
Sasa, wanangu, nisikilizeni; wala msiache kusikiliza maneno ya kinywa changu.
8 Njia zenu ziwe mbali naye, msiende karibu na mlango wa nyumba yake,
Lindeni njia yenu mbali naye wala msiende karibu na mlango wa nyumba yake.
9 usije ukatoa nguvu zako nzuri kwa wengine na miaka yako kwa aliye mkatili,
Kwa njia hiyo hamtawapa wengine heshima yenu au miaka ya uzima wenu kwa mtu mkatiri;
10 wageni wasije wakasherehekea utajiri wako na jitihada yako ikatajirisha nyumba ya mwanaume mwingine.
wageni usije kufanya karamu kwa utajiri wenu; kazi mliyoifanya haitaenda katika nyumba ya wageni.
11 Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu, wakati nyama na mwili wako vimechakaa.
Mwishoni mwa maisha yenu mtajuta ambapo nyama na mwili wenu vitaangamia.
12 Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu! Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo!
Nanyi mtasema, “Namna gani nilichukia fundisho na moyo wangu ulidharau sahihisho!
13 Sikuwatii walimu wangu wala kuwasikiliza wakufunzi wangu.
Sikuweza kuwatii walimu wangu au kuwasikiliza walionielekeza.
14 Nimefika ukingoni mwa maangamizi kabisa katikati ya kusanyiko lote.”
Nilikuwa nimeharibika kabisa katikati ya kusanyiko, miongoni mwa makutano ya watu.”
15 Kunywa maji kutoka kwenye kisima chako mwenyewe, maji yanayotiririka kutoka kwenye kisima chako mwenyewe.
Munywe maji kutoka kwenye birika lenu mwenyewe na munywe maji yanatiririka kutoka kwenye kisima chenu.
16 Je, chemchemi zako zifurike katika barabara za mji na vijito vyako vya maji viwanjani?
Je inapaswa chemichemi yenu ifurike popote na mifereji yenu ya maji itiririke katika njia kuu?
17 Na viwe vyako mwenyewe, kamwe visishirikishwe wageni.
Yawe yenu wenyewe peke yenu wala si kwa wageni.
18 Chemchemi yako na ibarikiwe na umfurahie mke wa ujana wako.
Chemichemi yako ibarikiwe na umfurahie mke wa ujana wako.
19 Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri: matiti yake na yakutosheleze siku zote, nawe utekwe daima na upendo wake.
Maana ni ayala apendezaye na kulungu mwenye uzuri. Matiti yake na yakujaze furaha muda wote; daima na utekwe na upendo wake.
20 Kwa nini mwanangu, utekwe na mwanamke kahaba? Kwa nini ukumbatie kifua cha mke wa mwanaume mwingine?
Mwanangu, kwa nini uwe mateka wa malaya, kwa nini uyakumbatie matiti ya mwanamke mgeni?
21 Kwa maana njia za mtu ni wazi kabisa mbele za Bwana, naye huyapima mapito yake yote.
Yehova huona kila kitu afanyacho mtu na huangalia mapito yake yote.
22 Matendo mabaya ya mtu mwovu humnasa yeye mwenyewe; kamba za dhambi yake humkamata kwa nguvu.
Mtu mwovu atatekwa na makosa yake mwenyewe; kamba za dhambi yake zitamnasa kwa nguvu.
23 Atakufa kwa kukosa nidhamu, akipotoshwa kwa upumbavu wake mwenyewe.
Atakufa kwa kukosa maonyo; atapotelea mbali kwa upumbavu wake wingi.