< Mithali 29 >

1 Mtu anayeendelea kuwa na shingo ngumu baada ya maonyo mengi, ataangamia ghafula, wala hapati dawa.
איש תוכחות מקשה-ערף-- פתע ישבר ואין מרפא
2 Wenye haki wanapostawi, watu hufurahi; waovu watawalapo, watu hulia kwa huzuni.
ברבות צדיקים ישמח העם ובמשל רשע יאנח עם
3 Mtu apendaye hekima huleta furaha kwa baba yake, bali aambatanaye na makahaba hutapanya mali yake.
איש-אהב חכמה ישמח אביו ורעה זונות יאבד-הון
4 Kwa haki mfalme huipa nchi uthabiti, bali mfalme aliye na tamaa ya rushwa huiangamiza.
מלך--במשפט יעמיד ארץ ואיש תרומות יהרסנה
5 Yeyote amsifuye jirani yake isivyostahili, anautandaza wavu kuitega miguu yake.
גבר מחליק על-רעהו רשת פורש על-פעמיו
6 Mtu mbaya hutegwa na dhambi yake mwenyewe bali mwenye haki huweza kuimba na kufurahi.
בפשע איש רע מוקש וצדיק ירון ושמח
7 Mwenye haki hujali haki kwa ajili ya maskini, bali mwovu hajishughulishi na hilo.
ידע צדיק דין דלים רשע לא-יבין דעת
8 Wenye mzaha huuchochea mji, bali watu wenye hekima hugeuzia mbali hasira.
אנשי לצון יפיחו קריה וחכמים ישיבו אף
9 Kama mwenye hekima akienda mahakamani na mpumbavu, mpumbavu hukasirika na kudhihaki, wala hakuna amani.
איש-חכם--נשפט את-איש אויל ורגז ושחק ואין נחת
10 Watu wamwagao damu humchukia mtu mwadilifu na hutafuta kumuua mtu mnyofu.
אנשי דמים ישנאו-תם וישרים יבקשו נפשו
11 Mpumbavu huonyesha hasira yake yote, bali mwenye hekima hujizuia.
כל-רוחו יוציא כסיל וחכם באחור ישבחנה
12 Kama mtawala akisikiliza uongo, maafisa wake wote huwa waovu.
משל מקשיב על-דבר-שקר-- כל-משרתיו רשעים
13 Mtu maskini na mtu anayeonea wanafanana kwa jambo hili: Bwana hutia nuru macho yao wote wawili.
רש ואיש תככים נפגשו-- מאיר עיני שניהם יהוה
14 Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki, kiti chake cha enzi kitakuwa thabiti siku zote.
מלך שופט באמת דלים-- כסאו לעד יכון
15 Fimbo ya maonyo hutia hekima, bali mtoto aliyeachiwa bila maonyo humwaibisha mama yake.
שבט ותוכחת יתן חכמה ונער משלח מביש אמו
16 Wakati waovu wanapostawi, pia dhambi vivyo hivyo, lakini wenye haki wataliona anguko lao.
ברבות רשעים ירבה-פשע וצדיקים במפלתם יראו
17 Mrudi mwanao, naye atakupa amani, atakufurahisha nafsi yako.
יסר בנך ויניחך ויתן מעדנים לנפשך
18 Mahali pasipo na ufunuo, watu kujizuia, bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.
באין חזון יפרע עם ושמר תורה אשרהו
19 Mtumishi hawezi kuonywa kwa maneno matupu, ajapoelewa, hataitikia.
בדברים לא-יוסר עבד כי-יבין ואין מענה
20 Je, unamwona mtu azungumzaye kwa haraka? Kuna matumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko yeye.
חזית--איש אץ בדבריו תקוה לכסיל ממנו
21 Kama mtu akimdekeza mtumishi wake tangu ujanani, atamletea sikitiko mwishoni.
מפנק מנער עבדו ואחריתו יהיה מנון
22 Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi, naye mtu mwenye hasira ya haraka hutenda dhambi nyingi.
איש-אף יגרה מדון ובעל חמה רב-פשע
23 Kiburi cha mtu humshusha, bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu hupata heshima.
גאות אדם תשפילנו ושפל-רוח יתמך כבוד
24 Anayekubaliana na mwizi ni adui wa nafsi yake mwenyewe; huapishwa lakini hathubutu kushuhudia.
חולק עם-גנב שונא נפשו אלה ישמע ולא יגיד
25 Kuwaogopa watu huwa ni mtego, bali yeyote amtumainiaye Bwana atakuwa salama.
חרדת אדם יתן מוקש ובוטח ביהוה ישגב
26 Wengi hutafuta kusikilizwa na mtawala, bali mtu hupata haki kutoka kwa Bwana.
רבים מבקשים פני-מושל ומיהוה משפט-איש
27 Mwenye haki huwachukia sana wasio waaminifu; waovu huwachukia sana wenye haki.
תועבת צדיקים איש עול ותועבת רשע ישר-דרך

< Mithali 29 >