< Mithali 27 >

1 Usijisifu kwa ajili ya kesho, kwa kuwa hujui ni nini kitakachozaliwa kwa siku moja.
אל תתהלל ביום מחר כי לא תדע מה ילד יום׃
2 Mwache mwingine akusifu, wala si kinywa chako mwenyewe; mtu mwingine afanye hivyo na si midomo yako mwenyewe.
יהללך זר ולא פיך נכרי ואל שפתיך׃
3 Jiwe ni zito na mchanga ni mzigo, lakini kukasirishwa na mpumbavu ni kuzito kuliko vyote viwili.
כבד אבן ונטל החול וכעס אויל כבד משניהם׃
4 Hasira ni ukatili na ghadhabu kali ni gharika, lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu?
אכזריות חמה ושטף אף ומי יעמד לפני קנאה׃
5 Afadhali karipio la wazi kuliko upendo uliofichika.
טובה תוכחת מגלה מאהבה מסתרת׃
6 Majeraha kutoka kwa rafiki yaonyesha uaminifu, bali kubusu kwa adui ni kwingi sana.
נאמנים פצעי אוהב ונעתרות נשיקות שונא׃
7 Yeye aliyeshiba huchukia kabisa asali, bali kwa mwenye njaa hata kile kilicho kichungu kwake ni kitamu.
נפש שבעה תבוס נפת ונפש רעבה כל מר מתוק׃
8 Kama ndege atangatangavyo mbali na kiota chake, ndivyo alivyo mtu atangatangaye mbali na nyumbani mwake.
כצפור נודדת מן קנה כן איש נודד ממקומו׃
9 Manukato na uvumba huleta furaha moyoni, nao uzuri wa rafiki huchipuka kutoka kwenye ushauri wake wa uaminifu.
שמן וקטרת ישמח לב ומתק רעהו מעצת נפש׃
10 Usimwache rafiki yako wala rafiki wa baba yako, tena usiende nyumbani mwa ndugu yako wakati umepatwa na maafa. Bora jirani wa karibu kuliko ndugu aliye mbali.
רעך ורעה אביך אל תעזב ובית אחיך אל תבוא ביום אידך טוב שכן קרוב מאח רחוק׃
11 Mwanangu, uwe na hekima, nawe ulete furaha moyoni mwangu, ndipo nitakapoweza kumjibu yeyote anitendaye kwa dharau.
חכם בני ושמח לבי ואשיבה חרפי דבר׃
12 Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha, bali mjinga huendelea mbele nayo ikamtesa.
ערום ראה רעה נסתר פתאים עברו נענשו׃
13 Chukua vazi la yule awekaye dhamana kwa ajili ya mgeni; lishikilie iwe dhamana kama anafanya hivyo kwa ajili ya mwanamke mpotovu.
קח בגדו כי ערב זר ובעד נכריה חבלהו׃
14 Kama mtu akimbariki jirani yake kwa sauti kuu asubuhi na mapema, itahesabiwa kama ni laana.
מברך רעהו בקול גדול בבקר השכים קללה תחשב לו׃
15 Mke mgomvi ni kama matone yasiyokoma ya siku ya mvua.
דלף טורד ביום סגריר ואשת מדונים נשתוה׃
16 Kumzuia yeye ni kama kuuzuia upepo au kukamata mafuta kwa kiganja cha mkono.
צפניה צפן רוח ושמן ימינו יקרא׃
17 Kama vile chuma kinoavyo chuma, ndivyo mtu amnoavyo mwenzake.
ברזל בברזל יחד ואיש יחד פני רעהו׃
18 Yeye autunzaye mtini atakula tunda lake, naye amtunzaye bwana wake ataheshimiwa.
נצר תאנה יאכל פריה ושמר אדניו יכבד׃
19 Kama uso uonekanavyo kwenye maji, ndivyo hivyo moyo wa mtu humwonyesha alivyo.
כמים הפנים לפנים כן לב האדם לאדם׃
20 Kuzimu na Uharibifu havishibi kadhalika macho ya mwanadamu. (Sheol h7585)
שאול ואבדה לא תשבענה ועיני האדם לא תשבענה׃ (Sheol h7585)
21 Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru kwa ajili ya dhahabu, bali mtu hupimwa kwa sifa azipokeazo.
מצרף לכסף וכור לזהב ואיש לפי מהללו׃
22 Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu, ukimtwanga kama nafaka kwa mchi, hutauondoa upumbavu wake.
אם תכתוש את האויל במכתש בתוך הריפות בעלי לא תסור מעליו אולתו׃
23 Hakikisha kuwa unajua hali ya makundi yako ya kondoo na mbuzi, angalia kwa bidii ngʼombe zako.
ידע תדע פני צאנך שית לבך לעדרים׃
24 Kwa kuwa utajiri haudumu milele, nayo taji haidumu vizazi vyote.
כי לא לעולם חסן ואם נזר לדור דור׃
25 Wakati majani makavu yameondolewa na mapya yamechipua, nayo majani toka milimani yamekusanywa,
גלה חציר ונראה דשא ונאספו עשבות הרים׃
26 wana-kondoo watakupatia mavazi na mbuzi thamani ya shamba.
כבשים ללבושך ומחיר שדה עתודים׃
27 Utakuwa na maziwa mengi ya mbuzi kukulisha wewe na jamaa yako, na kuwalisha watumishi wako wa kike.
ודי חלב עזים ללחמך ללחם ביתך וחיים לנערותיך׃

< Mithali 27 >