< Mithali 26 >

1 Kama theluji wakati wa kiangazi au mvua wakati wa mavuno, ndivyo asivyostahili heshima mpumbavu.
כשלג בקיץ וכמטר בקציר כן לא נאוה לכסיל כבוד׃
2 Kama shomoro apigapigavyo mabawa yake au mbayuwayu katika kuruka kwake kasi, ndivyo ilivyo laana isiyo na sababu haimpati mtu.
כצפור לנוד כדרור לעוף כן קללת חנם לא תבא׃
3 Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, nayo fimbo kwa migongo ya wapumbavu!
שוט לסוס מתג לחמור ושבט לגו כסילים׃
4 Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama wewe mwenyewe utakuwa kama yeye.
אל תען כסיל כאולתו פן תשוה לו גם אתה׃
5 Mjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama atakuwa mwenye hekima machoni pake mwenyewe.
ענה כסיל כאולתו פן יהיה חכם בעיניו׃
6 Kama vile ilivyo kujikata miguu au kunywa hasara, ndivyo ilivyo kutuma ujumbe kwa mkono wa mpumbavu.
מקצה רגלים חמס שתה שלח דברים ביד כסיל׃
7 Kama miguu ya kiwete inavyoningʼinia ndivyo ilivyo mithali katika kinywa cha mpumbavu.
דליו שקים מפסח ומשל בפי כסילים׃
8 Kama kufunga jiwe kwenye kombeo, ndivyo ilivyo kumpa mpumbavu heshima.
כצרור אבן במרגמה כן נותן לכסיל כבוד׃
9 Kama mwiba kwenye mkono wa mlevi ndivyo ilivyo mithali kinywani mwa mpumbavu.
חוח עלה ביד שכור ומשל בפי כסילים׃
10 Kama mpiga upinde ambaye hujeruhi ovyo, ndivyo alivyo yeye aajiriye mpumbavu au yeyote apitaye njiani.
רב מחולל כל ושכר כסיל ושכר עברים׃
11 Kama mbwa ayarudiavyo matapiko yake, ndivyo mpumbavu arudiavyo upumbavu wake.
ככלב שב על קאו כסיל שונה באולתו׃
12 Je, unamwona mtu ajionaye mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Liko tumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko kwake.
ראית איש חכם בעיניו תקוה לכסיל ממנו׃
13 Mvivu husema, “Yuko simba barabarani, simba mkali anazunguka mitaa!”
אמר עצל שחל בדרך ארי בין הרחבות׃
14 Kama vile mlango ugeukavyo kwenye bawaba zake, ndivyo mvivu ajigeuzavyo kitandani mwake.
הדלת תסוב על צירה ועצל על מטתו׃
15 Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani, naye huchoka kuupeleka kwenye kinywa chake.
טמן עצל ידו בצלחת נלאה להשיבה אל פיו׃
16 Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake mwenyewe, kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara.
חכם עצל בעיניו משבעה משיבי טעם׃
17 Kama yeye amkamataye mbwa kwa masikio, ndivyo alivyo mtu apitaye njiani na kujiingiza kwenye ugomvi usiomhusu.
מחזיק באזני כלב עבר מתעבר על ריב לא לו׃
18 Kama mtu mwendawazimu atupaye vijinga vya moto au mishale ya kufisha,
כמתלהלה הירה זקים חצים ומות׃
19 ndivyo alivyo mtu amdanganyaye jirani yake na kusema, “Nilikuwa nikifanya mzaha tu!”
כן איש רמה את רעהו ואמר הלא משחק אני׃
20 Bila kuni moto huzimika; pasipo uchongezi ugomvi humalizika.
באפס עצים תכבה אש ובאין נרגן ישתק מדון׃
21 Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, na kama kuni kwenye moto, ndivyo alivyo mtu mgomvi kwa kuchochea ugomvi.
פחם לגחלים ועצים לאש ואיש מדונים לחרחר ריב׃
22 Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu; huingia sehemu za ndani sana za mtu.
דברי נרגן כמתלהמים והם ירדו חדרי בטן׃
23 Kama rangi ingʼaayo iliyopakwa kwenye vyombo vya udongo ndivyo ilivyo midomo laini pamoja na moyo mbaya.
כסף סיגים מצפה על חרש שפתים דלקים ולב רע׃
24 Mtu mwenye nia ya kudhuru wengine hujificha kwa maneno ya midomo yake, lakini moyoni mwake huficha udanganyifu.
בשפתו ינכר שונא ובקרבו ישית מרמה׃
25 Ingawa maneno yake huvutia, usimwamini, kwa maana machukizo saba hujaza moyo wake.
כי יחנן קולו אל תאמן בו כי שבע תועבות בלבו׃
26 Nia yake ya kudhuru wengine inaweza kufichwa na udanganyifu, lakini uovu wake utafichuliwa kwenye kusanyiko.
תכסה שנאה במשאון תגלה רעתו בקהל׃
27 Kama mtu akichimba shimo, atatumbukia ndani yake, kama mtu akivingirisha jiwe, litamrudia.
כרה שחת בה יפל וגלל אבן אליו תשוב׃
28 Ulimi wa uongo, huwachukia wale unaowaumiza, nacho kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.
לשון שקר ישנא דכיו ופה חלק יעשה מדחה׃

< Mithali 26 >