< Mithali 24 >

1 Usiwaonee wivu watu waovu, usitamani ushirika nao;
אַל־תְּקַנֵּא בְּאַנְשֵׁי רָעָה וְאַל־תתאו תִּתְאָיו לִהְיוֹת אִתָּֽם׃
2 kwa maana mioyo yao hupanga mambo ya jeuri, nayo midomo yao husema juu ya kuleta madhara.
כִּי־שֹׁד יֶהְגֶּה לִבָּם וְעָמָל שִׂפְתֵיהֶם תְּדַבֵּֽרְנָה׃
3 Kwa hekima nyumba hujengwa, nayo kwa njia ya ufahamu huimarishwa
בְּחָכְמָה יִבָּנֶה בָּיִת וּבִתְבוּנָה יִתְכּוֹנָֽן׃
4 kwa njia ya maarifa vyumba vyake hujazwa vitu vya thamani na vya kupendeza.
וּבְדַעַת חֲדָרִים יִמָּלְאוּ כָּל־הוֹן יָקָר וְנָעִֽים׃
5 Mtu mwenye hekima ana uwezo mkubwa, naye mtu mwenye maarifa huongeza nguvu,
גֶּֽבֶר־חָכָם בַּעוֹז וְאִֽישׁ־דַּעַת מְאַמֶּץ־כֹּֽחַ׃
6 kwa kufanya vita unahitaji uongozi na kwa ushindi washauri wengi.
כִּי בְתַחְבֻּלוֹת תַּעֲשֶׂה־לְּךָ מִלְחָמָה וּתְשׁוּעָה בְּרֹב יוֹעֵֽץ׃
7 Hekima i juu mno kwa mpumbavu, katika kusanyiko langoni hana lolote la kusema.
רָאמוֹת לֶֽאֱוִיל חָכְמוֹת בַּשַּׁעַר לֹא יִפְתַּח־פִּֽיהוּ׃
8 Yeye apangaye mabaya atajulikana kama mtu wa hila.
מְחַשֵּׁב לְהָרֵעַ לוֹ בַּֽעַל־מְזִמּוֹת יִקְרָֽאוּ׃
9 Mipango ya upumbavu ni dhambi, watu huchukizwa na mwenye dhihaka.
זִמַּת אִוֶּלֶת חַטָּאת וְתוֹעֲבַת לְאָדָם לֵֽץ׃
10 Ukikata tamaa wakati wa taabu, jinsi gani nguvu zako ni kidogo!
הִתְרַפִּיתָ בְּיוֹם צָרָה צַר כֹּחֶֽכָה׃
11 Okoa wale wanaoongozwa kwenye kifo; wazuie wote wanaojikokota kuelekea machinjoni.
הַצֵּל לְקֻחִים לַמָּוֶת וּמָטִים לַהֶרֶג אִם־תַּחְשֽׂוֹךְ׃
12 Kama mkisema, “Lakini hatukujua lolote kuhusu hili,” je, yule apimaye mioyo halitambui hili? Je, yule awalindaye maisha yenu halijui hili? Je, hatamlipa kila mtu kulingana na aliyotenda?
כִּֽי־תֹאמַר הֵן לֹא־יָדַעְנוּ זֶה הֲ‍ֽלֹא־תֹכֵן לִבּוֹת ׀ הֽוּא־יָבִין וְנֹצֵר נַפְשְׁךָ הוּא יֵדָע וְהֵשִׁיב לְאָדָם כְּפָעֳלֽוֹ׃
13 Ule asali mwanangu, kwa kuwa ni nzuri; asali kutoka kwenye sega ni tamu kwa kuonja.
אֱכָל־בְּנִי דְבַשׁ כִּי־טוֹב וְנֹפֶת מָתוֹק עַל־חִכֶּֽךָ׃
14 Ujue pia kwamba hekima ni tamu kwa nafsi yako, kama ukiipata, kuna matumaini kwako ya siku zijazo, nalo tumaini lako halitakatiliwa mbali.
כֵּן ׀ דְּעֶה חָכְמָה לְנַפְשֶׁךָ אִם־מָצָאתָ וְיֵשׁ אַחֲרִית וְתִקְוָתְךָ לֹא תִכָּרֵֽת׃
15 Usivizie kama haramia afanyavyo ili kuyashambulia makao ya mwenye haki, wala usiyavamie makazi yake,
אַל־תֶּאֱרֹב רָשָׁע לִנְוֵה צַדִּיק אַֽל־תְּשַׁדֵּד רִבְצוֹ׃
16 Kwa maana ingawa mtu mwenye haki huanguka mara saba, huinuka tena, lakini waovu huangushwa chini na maafa.
כִּי שֶׁבַע ׀ יִפּוֹל צַדִּיק וָקָם וּרְשָׁעִים יִכָּשְׁלוּ בְרָעָֽה׃
17 Usitazame kwa kufurahia adui yako aangukapo; wakati ajikwaapo, usiruhusu moyo wako ushangilie.
בִּנְפֹל אויביך אֽוֹיִבְךָ אַל־תִּשְׂמָח וּבִכָּשְׁלוֹ אַל־יָגֵל לִבֶּֽךָ׃
18 Bwana asije akaona na kuchukia akaiondoa ghadhabu yake mbali naye.
פֶּן־יִרְאֶה יְהוָה וְרַע בְּעֵינָיו וְהֵשִׁיב מֵעָלָיו אַפּֽוֹ׃
19 Usikasirike kwa sababu ya watu wabaya wala usiwaonee wivu waovu,
אַל־תִּתְחַר בַּמְּרֵעִים אַל־תְּקַנֵּא בָּרְשָׁעִֽים׃
20 kwa maana mtu mbaya hana tumaini la siku zijazo, nayo taa ya waovu itazimwa.
כִּי ׀ לֹֽא־תִהְיֶה אַחֲרִית לָרָע נֵר רְשָׁעִים יִדְעָֽךְ׃
21 Mwanangu, mche Bwana na mfalme, wala usijiunge na waasi,
יְרָֽא־אֶת־יְהוָה בְּנִי וָמֶלֶךְ עִם־שׁוֹנִים אַל־תִּתְעָרָֽב׃
22 kwa maana hao wawili watatuma maangamizi ya ghafula juu yao, naye ni nani ajuaye maafa wawezayo kuleta?
כִּֽי־פִתְאֹם יָקוּם אֵידָם וּפִיד שְׁנֵיהֶם מִי יוֹדֵֽעַ׃
23 Hii pia ni misemo ya wenye hekima: Kuonyesha upendeleo katika hukumu si vyema:
גַּם־אֵלֶּה לַֽחֲכָמִים הַֽכֵּר־פָּנִים בְּמִשְׁפָּט בַּל־טֽוֹב׃
24 Yeyote amwambiaye mwenye hatia, “Wewe huna hatia,” Kabila zitamlaani na mataifa yatamkana.
אֹמֵר ׀ לְרָשָׁע צַדִּיק אָתָּה יִקְּבֻהוּ עַמִּים יִזְעָמוּהוּ לְאֻמִּֽים׃
25 Bali itakuwa vyema kwa wale watakaowatia hatiani wenye hatia, nazo baraka tele zitawajilia juu yao.
וְלַמּוֹכִיחִים יִנְעָם וַֽעֲלֵיהֶם תָּבוֹא בִרְכַּת־טֽוֹב׃
26 Jawabu la uaminifu ni kama busu la midomoni.
שְׂפָתַיִם יִשָּׁק מֵשִׁיב דְּבָרִים נְכֹחִֽים׃
27 Maliza kazi zako za nje, nawe uweke mashamba yako tayari, baada ya hayo, jenga nyumba yako.
הָכֵן בַּחוּץ ׀ מְלַאכְתֶּךָ וְעַתְּדָהּ בַּשָּׂדֶה לָךְ אַחַר וּבָנִיתָ בֵיתֶֽךָ׃
28 Usishuhudie dhidi ya jirani yako bila sababu, au kutumia midomo yako kudanganya.
אַל־תְּהִי עֵד־חִנָּם בְּרֵעֶךָ וַהֲפִתִּיתָ בִּשְׂפָתֶֽיךָ׃
29 Usiseme, “Nitamtenda kama alivyonitenda mimi; nitamlipiza mtu yule kwa kile alichonitendea.”
אַל־תֹּאמַר כַּאֲשֶׁר עָֽשָׂה־לִי כֵּן אֶֽעֱשֶׂה־לּוֹ אָשִׁיב לָאִישׁ כְּפָעֳלֽוֹ׃
30 Nilipita karibu na shamba la mvivu, karibu na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili,
עַל־שְׂדֵה אִישׁ־עָצֵל עָבַרְתִּי וְעַל־כֶּרֶם אָדָם חֲסַר־לֵֽב׃
31 miiba ilikuwa imeota kila mahali, ardhi ilikuwa imefunikwa na magugu, na ukuta wa mawe ulikuwa umebomoka.
וְהִנֵּה עָלָה כֻלּוֹ ׀ קִמְּשֹׂנִים כָּסּוּ פָנָיו חֲרֻלִּים וְגֶדֶר אֲבָנָיו נֶהֱרָֽסָה׃
32 Nikatafakari moyoni mwangu lile nililoliona, nami nikajifunza somo kutokana na niliyoyaona:
וָֽאֶחֱזֶה אָנֹכִֽי אָשִׁית לִבִּי רָאִיתִי לָקַחְתִּי מוּסָֽר׃
33 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika:
מְעַט שֵׁנוֹת מְעַט תְּנוּמוֹת מְעַט ׀ חִבֻּק יָדַיִם לִשְׁכָּֽב׃
34 hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi, na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.
וּבָֽא־מִתְהַלֵּךְ רֵישֶׁךָ וּמַחְסֹרֶיךָ כְּאִישׁ מָגֵֽן׃

< Mithali 24 >