< Mithali 11 >

1 Bwana huchukia sana mizani za udanganyifu, bali vipimo sahihi ni furaha yake.
מאזני מרמה תועבת יהוה ואבן שלמה רצונו
2 Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu, bali unyenyekevu huja na hekima.
בא-זדון ויבא קלון ואת-צנועים חכמה
3 Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao.
תמת ישרים תנחם וסלף בגדים ושדם (ישדם)
4 Utajiri haufaidi kitu katika siku ya ghadhabu, bali haki huokoa kutoka mautini.
לא-יועיל הון ביום עברה וצדקה תציל ממות
5 Haki ya wasio na lawama, huwatengenezea njia iliyonyooka, bali waovu huangushwa kwa uovu wao wenyewe.
צדקת תמים תישר דרכו וברשעתו יפל רשע
6 Haki ya wanyofu huwaokoa, bali wasio waaminifu hunaswa na tamaa mbaya.
צדקת ישרים תצילם ובהות בגדים ילכדו
7 Wakati mtu mwovu anapokufa, matumaini yake hutoweka; yote aliyoyatazamia kutokana na nguvu zake huwa si kitu.
במות אדם רשע תאבד תקוה ותוחלת אונים אבדה
8 Mtu mwenye haki huokolewa kutoka taabu, naye mtu mwovu huingia humo badala yake.
צדיק מצרה נחלץ ויבא רשע תחתיו
9 Kwa kinywa chake mtu asiyemwamini Mungu humwangamiza jirani yake, bali kwa maarifa mwenye haki huokolewa.
בפה--חנף ישחת רעהו ובדעת צדיקים יחלצו
10 Wakati mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi; mwovu atowekapo, kuna kelele za furaha.
בטוב צדיקים תעלץ קריה ובאבד רשעים רנה
11 Kutokana na baraka ya mtu mnyofu mji hukwezwa, bali kwa kinywa cha mwovu mji huharibiwa.
בברכת ישרים תרום קרת ובפי רשעים תהרס
12 Mtu asiye na akili humdharau jirani yake, bali mtu mwenye ufahamu huuzuia ulimi wake.
בז-לרעהו חסר-לב ואיש תבונות יחריש
13 Masengenyo husaliti tumaini, bali mtu mwaminifu hutunza siri.
הולך רכיל מגלה-סוד ונאמן-רוח מכסה דבר
14 Pasipo ushauri wa hekima taifa huanguka, bali washauri wengi hufanya ushindi uwe wa hakika.
באין תחבלות יפל-עם ותשועה ברב יועץ
15 Yeye amdhaminiye mgeni hakika atateseka, bali yeyote akataaye kuunga mkono dhamana ni salama.
רע-ירוע כי-ערב זר ושנא תקעים בוטח
16 Mwanamke mwenye moyo wa huruma hupata heshima, bali wanaume wakorofi hupata mali tu.
אשת-חן תתמך כבוד ועריצים יתמכו-עשר
17 Mwenye huruma hujinufaisha mwenyewe, bali mkatili hujiletea taabu mwenyewe.
גמל נפשו איש חסד ועכר שארו אכזרי
18 Mtu mwovu hupata ujira wa udanganyifu, bali yeye apandaye haki huvuna tuzo ya uhakika.
רשע--עשה פעלת-שקר וזרע צדקה שכר אמת
19 Mtu mwenye haki kweli kweli hupata uzima, bali yeye afuatiliaye ubaya huendea kifo chake.
כן-צדקה לחיים ומרדף רעה למותו
20 Bwana huwachukia sana watu wenye moyo wa upotovu, bali hupendezwa na wale ambao njia zao hazina lawama.
תועבת יהוה עקשי-לב ורצונו תמימי דרך
21 Uwe na hakika na hili: Waovu hawataepuka kuadhibiwa, bali wenye haki watakuwa huru.
יד ליד לא-ינקה רע וזרע צדיקים נמלט
22 Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe ndivyo alivyo mwanamke mzuri ambaye hana busara.
נזם זהב באף חזיר-- אשה יפה וסרת טעם
23 Shauku ya mwenye haki huishia tu kwenye mema, bali tumaini la mwovu huishia tu kwenye ghadhabu.
תאות צדיקים אך-טוב תקות רשעים עברה
24 Kuna mtu atoaye kwa ukarimu, hata hivyo hupata zaidi, mwingine huzuia, lakini huwa maskini.
יש מפזר ונוסף עוד וחשך מישר אך-למחסור
25 Mtu mkarimu atastawi; yeye awaburudishaye wengine ataburudishwa mwenyewe.
נפש-ברכה תדשן ומרוה גם-הוא יורא
26 Watu humlaani mtu awanyimae watu nafaka, bali baraka itamkalia kichwani kama taji yeye aliye radhi kuiuza.
מנע בר יקבהו לאום וברכה לראש משביר
27 Yeye atafutaye mema hupata ukarimu, bali ubaya huja kwake yeye autafutaye.
שחר טוב יבקש רצון ודרש רעה תבואנו
28 Yeyote ategemeaye utajiri wake ataanguka, bali mwenye haki atastawi kama jani bichi.
בוטח בעשרו הוא יפול וכעלה צדיקים יפרחו
29 Yeye aletaye taabu kwa jamaa yake atarithi tu upepo, naye mpumbavu atakuwa mtumishi wa wenye hekima.
עכר ביתו ינחל-רוח ועבד אויל לחכם-לב
30 Tunda la mwenye haki ni mti wa uzima, naye mwenye hekima huvuta roho za watu.
פרי-צדיק עץ חיים ולקח נפשות חכם
31 Kama wenye haki watapokea ujira wao duniani, si zaidi sana yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi?
הן צדיק בארץ ישלם אף כי-רשע וחוטא

< Mithali 11 >