< Hesabu 1 >

1 Bwana alisema na Mose katika Jangwa la Sinai, katika Hema la Kukutania, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, katika mwaka wa pili baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri. Akamwambia,
וידבר יהוה אל משה במדבר סיני באהל מועד באחד לחדש השני בשנה השנית לצאתם מארץ מצרים--לאמר
2 “Hesabu watu wa jumuiya yote ya Waisraeli kwa kufuata koo zao na jamaa zao, ukiorodhesha kila mwanaume kwa jina lake, mmoja mmoja.
שאו את ראש כל עדת בני ישראל למשפחתם לבית אבתם--במספר שמות כל זכר לגלגלתם
3 Wewe na Aroni mtawahesabu kwa migawanyo yao wanaume wote katika Israeli wenye miaka ishirini na kuendelea ambao wanaweza kutumika katika jeshi.
מבן עשרים שנה ומעלה כל יצא צבא בישראל--תפקדו אתם לצבאתם אתה ואהרן
4 Mwanaume mmoja kutoka kila kabila, kila aliye kiongozi wa jamaa yake, atawasaidia.
ואתכם יהיו איש איש למטה--איש ראש לבית אבתיו הוא
5 Haya ndiyo majina ya wanaume watakaowasaidia: “kutoka Reubeni, ni Elisuri mwana wa Shedeuri;
ואלה שמות האנשים אשר יעמדו אתכם לראובן אליצור בן שדיאור
6 kutoka Simeoni, ni Shelumieli mwana wa Surishadai;
לשמעון שלמיאל בן צורישדי
7 kutoka Yuda, ni Nashoni mwana wa Aminadabu;
ליהודה נחשון בן עמינדב
8 kutoka Isakari, ni Nethaneli mwana wa Suari;
ליששכר נתנאל בן צוער
9 kutoka Zabuloni, ni Eliabu mwana wa Heloni;
לזבולן אליאב בן חלן
10 kutoka wana wa Yosefu: kutoka Efraimu, ni Elishama mwana wa Amihudi; kutoka Manase, ni Gamalieli mwana wa Pedasuri;
לבני יוסף--לאפרים אלישמע בן עמיהוד למנשה גמליאל בן פדהצור
11 kutoka Benyamini, ni Abidani mwana wa Gideoni;
לבנימן אבידן בן גדעני
12 kutoka Dani, ni Ahiezeri mwana wa Amishadai;
לדן אחיעזר בן עמישדי
13 kutoka Asheri, ni Pagieli mwana wa Okrani;
לאשר פגעיאל בן עכרן
14 kutoka Gadi, ni Eliasafu mwana wa Deueli;
לגד אליסף בן דעואל
15 kutoka Naftali, ni Ahira mwana wa Enani.”
לנפתלי אחירע בן עינן
16 Hawa walikuwa wanaume walioteuliwa kutoka jumuiya, viongozi wa makabila ya baba zao. Walikuwa wakuu wa koo za Israeli.
אלה קריאי (קרואי) העדה נשיאי מטות אבותם ראשי אלפי ישראל הם
17 Mose na Aroni wakawachukua wanaume hao waliokuwa wamepewa majina yao,
ויקח משה ואהרן את האנשים האלה אשר נקבו בשמת
18 wakaita jumuiya yote pamoja katika siku ya kwanza ya mwezi wa pili. Watu wakaonyesha nasaba zao kwa koo zao na jamaa zao, nao wanaume waliokuwa na miaka ishirini au zaidi waliorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja,
ואת כל העדה הקהילו באחד לחדש השני ויתילדו על משפחתם לבית אבתם במספר שמות מבן עשרים שנה ומעלה--לגלגלתם
19 kama Bwana alivyomwagiza Mose. Hivyo aliwahesabu katika Jangwa la Sinai:
כאשר צוה יהוה את משה ויפקדם במדבר סיני
20 Kutoka wazao wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Israeli: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
ויהיו בני ראובן בכר ישראל תולדתם למשפחתם לבית אבתם במספר שמות לגלגלתם--כל זכר מבן עשרים שנה ומעלה כל יצא צבא
21 Idadi kutoka kabila la Reubeni ilikuwa watu 46,500.
פקדיהם למטה ראובן--ששה וארבעים אלף וחמש מאות
22 Kutoka wazao wa Simeoni: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi walihesabiwa na kuorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
לבני שמעון תולדתם למשפחתם לבית אבתם פקדיו במספר שמות לגלגלתם--כל זכר מבן עשרים שנה ומעלה כל יצא צבא
23 Idadi kutoka kabila la Simeoni walikuwa watu 59,300.
פקדיהם למטה שמעון--תשעה וחמשים אלף ושלש מאות
24 Kutoka wazao wa Gadi: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
לבני גד תולדתם למשפחתם לבית אבתם במספר שמות מבן עשרים שנה ומעלה--כל יצא צבא
25 Idadi kutoka kabila la Gadi walikuwa watu 45,650.
פקדיהם למטה גד--חמשה וארבעים אלף ושש מאות וחמשים
26 Kutoka wazao wa Yuda: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
לבני יהודה תולדתם למשפחתם לבית אבתם במספר שמת מבן עשרים שנה ומעלה--כל יצא צבא
27 Idadi kutoka kabila la Yuda walikuwa watu 74,600.
פקדיהם למטה יהודה--ארבעה ושבעים אלף ושש מאות
28 Kutoka wazao wa Isakari: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
לבני יששכר תולדתם למשפחתם לבית אבתם במספר שמת מבן עשרים שנה ומעלה--כל יצא צבא
29 Idadi kutoka kabila la Isakari walikuwa watu 54,400.
פקדיהם למטה יששכר--ארבעה וחמשים אלף וארבע מאות
30 Kutoka wazao wa Zabuloni: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
לבני זבולן תולדתם למשפחתם לבית אבתם במספר שמת מבן עשרים שנה ומעלה--כל יצא צבא
31 Idadi kutoka kabila la Zabuloni walikuwa watu 57,400.
פקדיהם למטה זבולן--שבעה וחמשים אלף וארבע מאות
32 Kutoka wana wa Yosefu: Kutoka wazao wa Efraimu: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
לבני יוסף לבני אפרים תולדתם למשפחתם לבית אבתם במספר שמת מבן עשרים שנה ומעלה--כל יצא צבא
33 Idadi kutoka kabila la Efraimu walikuwa watu 40,500.
פקדיהם למטה אפרים--ארבעים אלף וחמש מאות
34 Kutoka wazao wa Manase: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
לבני מנשה תולדתם למשפחתם לבית אבתם במספר שמות מבן עשרים שנה ומעלה--כל יצא צבא
35 Idadi kutoka kabila la Manase walikuwa watu 32,200.
פקדיהם למטה מנשה--שנים ושלשים אלף ומאתים
36 Kutoka wazao wa Benyamini: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
לבני בנימן תולדתם למשפחתם לבית אבתם במספר שמת מבן עשרים שנה ומעלה--כל יצא צבא
37 Idadi kutoka kabila la Benyamini walikuwa watu 35,400.
פקדיהם למטה בנימן--חמשה ושלשים אלף וארבע מאות
38 Kutoka wazao wa Dani: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
לבני דן תולדתם למשפחתם לבית אבתם במספר שמת מבן עשרים שנה ומעלה--כל יצא צבא
39 Idadi kutoka kabila la Dani walikuwa watu 62,700.
פקדיהם למטה דן--שנים וששים אלף ושבע מאות
40 Kutoka wazao wa Asheri: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
לבני אשר תולדתם למשפחתם לבית אבתם במספר שמת מבן עשרים שנה ומעלה--כל יצא צבא
41 Idadi kutoka kabila la Asheri walikuwa watu 41,500.
פקדיהם למטה אשר--אחד וארבעים אלף וחמש מאות
42 Kutoka wazao wa Naftali: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
בני נפתלי תולדתם למשפחתם לבית אבתם במספר שמת מבן עשרים שנה ומעלה--כל יצא צבא
43 Idadi kutoka kabila la Naftali walikuwa watu 53,400.
פקדיהם למטה נפתלי--שלשה וחמשים אלף וארבע מאות
44 Hawa walikuwa wanaume waliohesabiwa na Mose, Aroni na viongozi kumi na wawili wa Israeli, kila mmoja akiwakilisha jamaa yake.
אלה הפקדים אשר פקד משה ואהרן ונשיאי ישראל--שנים עשר איש איש אחד לבית אבתיו היו
45 Wanaume wote Waisraeli waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi la Israeli walihesabiwa kufuatana na jamaa zao.
ויהיו כל פקודי בני ישראל לבית אבתם מבן עשרים שנה ומעלה כל יצא צבא בישראל
46 Jumla ya hesabu yao ilikuwa watu 603,550.
ויהיו כל הפקדים--שש מאות אלף ושלשת אלפים וחמש מאות וחמשים
47 Hata hivyo, jamaa ya kabila la Lawi hawakuhesabiwa pamoja na wengine.
והלוים למטה אבתם--לא התפקדו בתוכם
48 Bwana alikuwa amemwambia Mose:
וידבר יהוה אל משה לאמר
49 “Kamwe usihesabu kabila la Lawi wala kuwaweka pamoja katika hesabu ya Waisraeli wengine.
אך את מטה לוי לא תפקד ואת ראשם לא תשא בתוך בני ישראל
50 Badala yake, waweke Walawi kuwa viongozi wa Maskani ya Ushuhuda, juu ya samani zake na kila kitu kilichomo ndani yake. Wao watabeba Maskani na samani zake zote; wataitunza na kupiga kambi kuizunguka.
ואתה הפקד את הלוים על משכן העדת ועל כל כליו ועל כל אשר לו--המה ישאו את המשכן ואת כל כליו והם ישרתהו וסביב למשכן יחנו
51 Wakati wowote Maskani inapohamishwa, Walawi wataifungua, na wakati wowote maskani inapotakiwa kusimamishwa, Walawi watafanya kazi hiyo. Mtu yeyote mwingine ambaye atasogea karibu nayo atauawa.
ובנסע המשכן יורידו אתו הלוים ובחנת המשכן יקימו אתו הלוים והזר הקרב יומת
52 Waisraeli watapiga mahema yao kwa makundi makundi, kila mwanaume katika kambi yake mwenyewe chini ya bendera yake.
וחנו בני ישראל איש על מחנהו ואיש על דגלו לצבאתם
53 Hata hivyo, Walawi watapiga mahema yao kuzunguka Maskani ya Ushuhuda ili ghadhabu isiipate jumuiya ya Waisraeli. Walawi watawajibika kwa utunzaji wa Maskani ya Ushuhuda.”
והלוים יחנו סביב למשכן העדת ולא יהיה קצף על עדת בני ישראל ושמרו הלוים את משמרת משכן העדות
54 Waisraeli walifanya yote haya sawasawa kama Bwana alivyomwamuru Mose.
ויעשו בני ישראל ככל אשר צוה יהוה את משה--כן עשו

< Hesabu 1 >