< Hesabu 5 >

1 Bwana akamwambia Mose,
BWANA alinena na Musa. Akasema,
2 “Waamuru Waisraeli kumtoa nje ya kambi mtu yeyote ambaye ana ugonjwa wa ngozi uambukizao, au anayetokwa na majimaji ya aina yoyote, au ambaye ni najisi kwa utaratibu wa ibada kwa sababu ya maiti.
“Waamuru wana wa Israel wawatoe watu wote wenye magonjwa ya ngozi yanayoambukiza, na kila mwenye mwenye vidonda vinavyotoa harufu, na ambaye amenajisika kwa kugusa maiti.
3 Hii itakuwa ni kwa wote, yaani, wanaume na wanawake; watoeni nje ya kambi ili wasije wakanajisi kambi yao, ambamo ninaishi miongoni mwao.”
Awe mme au mke, umtoa kambini. Ili wasije wakaitia unajisi kambi, kwa sababu Mimi huishi ndani yake,”
4 Waisraeli wakafanya hivyo; wakawatoa nje ya kambi. Wakafanya kama vile Bwana alivyokuwa amemwelekeza Mose.
Watu wa Israeli walifanya hivyo. Waliwatoa kambini, Kama BWANA alivyomwagiza Musa. Watu wa Israeli walimtii BWANA.
5 Bwana akamwambia Mose,
Tena BWANA akanena na Musa. Akasema,
6 “Waambie Waisraeli, ‘Wakati mwanaume au mwanamke akimkosea mwenzake kwa njia yoyote, na kwa hivyo akawa si mwaminifu kwa Bwana, mtu huyo ana hatia,
“Nena na wana wa Israeli. mtu mume na mtu mke akifanya dhambi yeyote ambayo watu hufanyiana wao kwa wao, na mtu huyo akamwasi BWANA, mtu huyo atakuwa na hatia.
7 na ni lazima atubu dhambi aliyoifanya. Ni lazima atoe malipo kamili kwa ajili ya kosa lake, aongeze sehemu ya tano juu ya malipo hayo na kutoa yote kwa mtu aliyemkosea.
Ndipo huyo mtu ataungama hiyo dhambi aliyoifanya. Mtu huyo atarudisha malipo ya hatia yake na kuongeza kwenye malipo hayo sehemu ya tano zaidi. Atamlipa huyo aliyemtendea makosa
8 Lakini ikiwa mtu huyo hana jamaa ya karibu ambaye malipo yanaweza kufanywa kwa ajili ya kosa, malipo yatakuwa mali ya Bwana, nayo ni lazima apewe kuhani, pamoja na kondoo dume ambaye anatumika kufanyia upatanisho kwa ajili yake.
Lakini kama huyo mtu huyu aliyetendewa kosa hana ndugu wa kupokea hayo malipo, basi atalipa hayo malipo ya hatia kwangu kupitia kuhani pamoja na kondoo dume kwa ajili ya sadaka yake mwenyewe.
9 Matoleo yote matakatifu ya Waisraeli wanayoleta kwa kuhani yatakuwa yake.
Kila sadaka ya wana wa Israeli, vitu ambavyo vimetengwa na vikaletwa kwa kuhani na watu wa Israeli, vitakuwa vyake.
10 Kila kitu cha mtu kilichowekwa wakfu ni chake mwenyewe, lakini kile atoacho kwa kuhani kitakuwa cha kuhani.’”
Sadaka ya kila mtu itakuwa ya kuhani; kama mtu yeyote atatoa kitu chochote kwa kuhani, kitakuwa chake.”
11 Kisha Bwana akamwambia Mose,
Tena BWANA akanena na Musa. Akasema,
12 “Nena na Waisraeli uwaambie: ‘Ikiwa mke wa mtu amepotoka na si mwaminifu kwa mumewe,
“Nena na wana wa Israel. Uwaambie, 'kama mke wa mtu ataasi na kufanya dhambi dhidi ya mume wake.
13 kwa kukutana kimwili na mwanaume mwingine, tendo hili likafichika kwa mumewe na unajisi wake usigundulike (kwa kuwa hakuna ushahidi dhidi yake, naye hakukamatwa katika tendo hilo),
Halafu mtu mwingine akalala naye. Kwa sababu, hiyo atakuwa amenajisika. Na hata kama mume wake hakuona na hajui, hata kama hakuna mtu aliyemkamta akiwa katika tendo na hakuna mtu wa kushuhudia dhidi yake; hata hivyo ile roho ya wivu itaendele kumjulisha yule mume kuwa mke wake amenajisika.
14 nazo hisia za wivu zikamjia mumewe na kumshuku mkewe, naye mke yule ni najisi, au mumewe ana wivu na akamshuku ingawa si najisi,
Ingawa, roho ya wivu inaweza kumdanganya yule mwanamume wakati mke wake hajanajisika.
15 basi atampeleka mkewe kwa kuhani. Huyo mume itampasa apeleke pia sadaka ya unga wa shayiri kiasi cha sehemu ya kumi ya efa kwa niaba ya mkewe. Huyo mwanaume kamwe asimimine mafuta juu ya huo unga wala asiweke uvumba juu yake, kwa sababu ni sadaka ya nafaka kwa ajili ya wivu, sadaka ya ukumbusho ili kukumbushia uovu.
Kwa mazingira hayo, yule mwanamume anapaswa kumpeleka mke wake kwa kuhani. Yule mwanamume anapaswa kutoa sadaka ya divai kwa ajili yake. Atapaswa kuleta sehemu ya kumi ya efa ya unga wa shayiri. Asitie mafuta juu yake wala asitie ubani juu yake maana ni sadaka ya unga ya wivu, ni sadaka ya unga ya ukumbusho wa uovu.
16 “‘Kuhani atamleta huyo mwanamke na kumsimamisha mbele za Bwana.
Ndipo kuhani atasogeza karibu na kumweka mbele ya BWANA.
17 Kisha kuhani atachukua sehemu ya maji matakatifu ndani ya gudulia la udongo na kuchanganya na baadhi ya vumbi kutoka sakafu ya Maskani.
Kuhani atachukua kikombe cha maji matakatifu na atachukua mavumbi ya kwenye masikani. Ataweka yale mavumbi kwenye maji.
18 Baada ya kuhani kumsimamisha huyo mwanamke mbele za Bwana, atazifungua nywele za huyo mwanamke na kuweka sadaka ya ukumbusho mikononi mwake, ile sadaka ya nafaka kwa ajili ya wivu, huku kuhani mwenyewe akishikilia yale maji machungu yaletayo laana.
Kisha kuhani atamweka huyo mwanamke mbele za BWANA na atazifungua nywele kichwani kwa huyo mwanamke. Atamwekea mikononi mwake hiyo sadaka ya unga kwa ajili ya ukumbusho, ambayo ni sadaka ya unga kwa ajili ya wivu.
19 Kisha kuhani atamwapiza huyo mwanamke, akimwambia, “Ikiwa hakuna mwanaume mwingine aliyekutana kimwili nawe, wala hujapotoka na kuwa najisi wakati ukiwa umeolewa na mumeo, maji haya machungu yaletayo laana na yasikudhuru.
Kuhani atashikilia mikononi mwake maji machungu yanayoweza kuleta laana. Kuhani atamweka huyo mwanamke chini ya kiapo na kumwambia. 'Kama haujafanya uzinzi na mwanaume mwingine, na kama hajakengeuka na kufanya uovu, basi utakuwa huru na maji haya yanayoweza kuleta laana.
20 Lakini ikiwa umepotoka wakati ukiwa umeolewa na mume wako na umejinajisi mwenyewe kwa kukutana kimwili na mwanaume mwingine asiyekuwa mumeo”;
Lakini kama wewe, mwanamke uliye chini ya mume wako, umekengeuka, na kama umenajisika, na kama mwanamume mwingina amelala nawe,
21 hapa kuhani atamweka huyo mwanamke chini ya laana ya kiapo akisema: “Bwana na awafanye watu wako wakulaani na kukukataa, wakati Bwana atakapolifanya paja lako kupooza na tumbo lako kuvimba.
ndipo, (kuhani atamtaka huyo mwanamke aape kiapo kinachoweza kuleta laana kwake, na kwamba ataendelea kumwambia yule mwanamke) 'BWANA atakufanya wewe kuwa laana itakayooneshwa kuwa hivyo kwa watu wako. Hii itatokea pale BWANA atakapoyafanya mapaja yako kuoza na tumbo lako kuvimba.
22 Maji haya yaletayo laana na yaingie ndani ya mwili wako ili tumbo lako livimbe na paja lako lipooze.” “‘Kisha mwanamke atasema, “Amen. Iwe hivyo.”
Haya maji ambayo huleta laana yataingia tumboni mwako na kulifanya tumbo lako kuvimba na mapaja yako kuoza,' mwanamke alitakiwa kujibu, 'Ndiyo, hayo yanipate kama mimi ni mwenye hatia.'
23 “‘Kuhani ataandika laana hizi kwenye kitabu, kisha atazioshea laana hizo kwenye yale maji machungu.
Naye kuhani ataziandika laana hizi kwenye kitabu, na kisha kuzifuta laana zilizoandikwa kwa maji ya uchungu.
24 Kuhani atamnywesha yule mwanamke yale maji machungu yaletayo laana, nayo maji haya yatamwingia na kumsababishia maumivu makali.
Naye kuhani atamwelekeza yule mwanamke kunywa yale maji machungu yaletayo laana. Yale maji yaletayo laana yataingia na kuwa machungu.
25 Kuhani atachukua sadaka ya nafaka kwa ajili ya wivu kutoka mikononi mwa huyo mwanamke, naye ataipunga mbele za Bwana na kuileta madhabahuni.
Kuhani ataitwaa ile sadaka ya unga ya wivu mikononi mwa yule mwanamke. Atailekeza ile sadaka ya unga mbele ya BWANA na kuileta madhabahuni.
26 Kisha kuhani atachota sadaka ya nafaka mkono uliojaa kama sehemu ya kumbukumbu na kuiteketeza juu ya madhabahu, baada ya hayo, atamtaka huyo mwanamke anywe yale maji.
Kuhani atachukua konzi ya sadaka ya unga mkononi mwake kama sadaka ya kuwakilisha, na kuiteketeza madhabahuni. Ndipo atakapompatia mwanamke yale maji machungu ili ayanywe.
27 Kama amejitia unajisi na kukosa uaminifu kwa mumewe, wakati anapotakiwa anywe maji yale yaletayo laana, yatamwingia na kusababisha maumivu makali; tumbo lake litavimba na paja lake litapooza, naye atakuwa amelaaniwa miongoni mwa watu wake.
Wakati wa kumpa yale maji ili anywe, kama amenajisika kwa sababu alifanya uovu dhidi ya mume wake, ndipo yale maji yaletayo laana yatamwingia na kuwa machungu. Tumbo lake litavimba na paja lake litaoza. Yule mwanamke atalaaniwa kati ya watu wake.
28 Hata hivyo, ikiwa huyo mwanamke hakujitia unajisi, naye ni safi, atasafishwa hatia na ataweza kuzaa watoto.
Lakini kama yule mwanake hajanajisika na kama ni msafi, basi atakuwa huru. Tena ataweza kubeba uja uzito.
29 “‘Basi, hii ndiyo sheria ya wivu mwanamke anapopotoka na kujitia unajisi akiwa ameolewa na mumewe,
Hii ndiyo sheria ya wivu. Ni sheria ya mwanamke anayekengeuka kwa mumewe na kunajisika.
30 au hisia za wivu zinapomjia mwanaume kwa sababu ya kumshuku mkewe. Kuhani atamfanya huyo mwanamke kusimama mbele za Bwana na atatumia sheria hii yote kwa huyo mwanamke.
Ni sheria ya mwanamume mwenye roho ya wivu kwa mkewe. Atamleta mwanamke mbele ya BWANA, na kuhani atamfanyia huyo mwanamke kila kitu ambacho sheria ya wivu inamtaka kufanya.
31 Mume atakuwa hana hatia ya kosa lolote, bali mwanamke atayachukua matokeo ya dhambi yake.’”
Yule mwanamume atakuwa hana hatia kwa kumleta mke wake kwa kuhani. Na yule mwanmke atauchukua uovu wake.”

< Hesabu 5 >