< Hesabu 34 >

1 Bwana akamwambia Mose,
וידבר יהוה אל משה לאמר׃
2 “Waamuru Waisraeli na uwaambie: ‘Mtakapoingia nchi ya Kanaani, nchi ambayo itagawanywa kwenu kama urithi itakuwa na mipaka ifuatayo:
צו את בני ישראל ואמרת אלהם כי אתם באים אל הארץ כנען זאת הארץ אשר תפל לכם בנחלה ארץ כנען לגבלתיה׃
3 “‘Upande wenu wa kusini utajumuisha sehemu ya Jangwa la Sini kufuata mpaka wa Edomu. Upande wa mashariki mpaka wenu wa kusini utaanzia mwisho wa Bahari ya Chumvi,
והיה לכם פאת נגב ממדבר צן על ידי אדום והיה לכם גבול נגב מקצה ים המלח קדמה׃
4 katiza kusini mwa Pito la Akrabimu, endelea mpaka Sini na kwenda kusini ya Kadesh-Barnea. Kisha mpaka huo utaenda hadi Hasar-Adari hadi Azmoni,
ונסב לכם הגבול מנגב למעלה עקרבים ועבר צנה והיה תוצאתיו מנגב לקדש ברנע ויצא חצר אדר ועבר עצמנה׃
5 mahali ambapo utapinda, na kuunganika na Kijito cha Misri na kumalizikia kwenye Bahari ya Kati.
ונסב הגבול מעצמון נחלה מצרים והיו תוצאתיו הימה׃
6 “‘Mpaka wenu wa magharibi utakuwa Bahari ya Kati. Huu utakuwa mpaka wenu upande wa magharibi.
וגבול ים והיה לכם הים הגדול וגבול זה יהיה לכם גבול ים׃
7 “‘Kwa mpaka wenu wa kaskazini, wekeni alama kuanzia Bahari ya Kati hadi mlima Hori,
וזה יהיה לכם גבול צפון מן הים הגדל תתאו לכם הר ההר׃
8 na kutoka mlima Hori hadi Pito la Hamathi. Kisha mpaka utaenda hadi Sedadi,
מהר ההר תתאו לבא חמת והיו תוצאת הגבל צדדה׃
9 kuendelea hadi Zifroni, na kuishia Hasar-Enani. Huu utakuwa mpaka wenu upande wa kaskazini.
ויצא הגבל זפרנה והיו תוצאתיו חצר עינן זה יהיה לכם גבול צפון׃
10 “‘Kwa mpaka wenu wa mashariki, wekeni alama kuanzia Hasar-Enani hadi Shefamu.
והתאויתם לכם לגבול קדמה מחצר עינן שפמה׃
11 Mpaka utaelekea kusini kuanzia Shefamu hadi Ribla upande wa mashariki wa Aini, na kuendelea kwenye miteremko mashariki mwa Bahari ya Kinerethi.
וירד הגבל משפם הרבלה מקדם לעין וירד הגבול ומחה על כתף ים כנרת קדמה׃
12 Kisha mpaka utashuka kuelekea Mto Yordani na kuishia katika Bahari ya Chumvi. “‘Hii itakuwa nchi yenu, ikiwa na mipaka yake kila upande.’”
וירד הגבול הירדנה והיו תוצאתיו ים המלח זאת תהיה לכם הארץ לגבלתיה סביב׃
13 Mose akawaamuru Waisraeli: “Gawanyeni nchi hii kwa kura kama urithi. Bwana ameagiza kwamba itolewe kwa yale makabila tisa na nusu,
ויצו משה את בני ישראל לאמר זאת הארץ אשר תתנחלו אתה בגורל אשר צוה יהוה לתת לתשעת המטות וחצי המטה׃
14 kwa sababu jamaa ya kabila la Reubeni, kabila la Gadi, na nusu ya kabila la Manase wamekwishapokea urithi wao.
כי לקחו מטה בני הראובני לבית אבתם ומטה בני הגדי לבית אבתם וחצי מטה מנשה לקחו נחלתם׃
15 Haya makabila mawili na nusu wamekwishapokea urithi wao upande wa mashariki wa Yordani ngʼambo ya Yeriko, kuelekea mawio ya jua.”
שני המטות וחצי המטה לקחו נחלתם מעבר לירדן ירחו קדמה מזרחה׃
16 Bwana akamwambia Mose,
וידבר יהוה אל משה לאמר׃
17 “Haya ndiyo majina ya watu ambao watakusaidia kugawanya nchi kama urithi: Eleazari kuhani na Yoshua mwana wa Nuni.
אלה שמות האנשים אשר ינחלו לכם את הארץ אלעזר הכהן ויהושע בן נון׃
18 Tena uteue kiongozi mmoja kutoka kila kabila kusaidia kuigawanya nchi.
ונשיא אחד נשיא אחד ממטה תקחו לנחל את הארץ׃
19 Haya ndiyo majina yao: “Kalebu mwana wa Yefune, kutoka kabila la Yuda;
ואלה שמות האנשים למטה יהודה כלב בן יפנה׃
20 Shemueli mwana wa Amihudi, kutoka kabila la Simeoni;
ולמטה בני שמעון שמואל בן עמיהוד׃
21 Elidadi mwana wa Kisloni, kutoka kabila la Benyamini;
למטה בנימן אלידד בן כסלון׃
22 Buki mwana wa Yogli, kiongozi kutoka kabila la Dani;
ולמטה בני דן נשיא בקי בן יגלי׃
23 Hanieli mwana wa Efodi, kiongozi kutoka kabila la Manase mwana wa Yosefu;
לבני יוסף למטה בני מנשה נשיא חניאל בן אפד׃
24 Kemueli mwana wa Shiftani, kiongozi kutoka kabila la Efraimu mwana wa Yosefu;
ולמטה בני אפרים נשיא קמואל בן שפטן׃
25 Elisafani mwana wa Parnaki, kiongozi kutoka kabila la Zabuloni;
ולמטה בני זבולן נשיא אליצפן בן פרנך׃
26 Paltieli mwana wa Azani, kiongozi kutoka kabila la Isakari;
ולמטה בני יששכר נשיא פלטיאל בן עזן׃
27 Ahihudi mwana wa Shelomi, kiongozi kutoka kabila la Asheri;
ולמטה בני אשר נשיא אחיהוד בן שלמי׃
28 Pedaheli mwana wa Amihudi, kiongozi kutoka kabila la Naftali.”
ולמטה בני נפתלי נשיא פדהאל בן עמיהוד׃
29 Hawa ndio watu ambao Bwana aliamuru wagawanye urithi kwa Waisraeli katika nchi ya Kanaani.
אלה אשר צוה יהוה לנחל את בני ישראל בארץ כנען׃

< Hesabu 34 >