< Hesabu 33 >

1 Hivi ndivyo vituo katika safari ya Waisraeli walipotoka Misri kwa vikosi chini ya uongozi wa Mose na Aroni.
Hizi ndizo safari za wana wa Israeli hapo walipotoka katika nchi ya Misri pamoja na makundi yao ya kijeshi chini ya uongozi wa Musa na Haruni.
2 Kwa agizo la Bwana, Mose aliweka kumbukumbu ya vituo katika safari yao. Hivi ndivyo vituo katika safari yao:
Musa aliandika maeneo yote tangu walipoondoka mpaka walipofika, kama alivyoamuriwa na BWANA. Hizi ndizo safari zao kama kutoka kwao kulivyokuwa kwa kila walipotoka.
3 Waisraeli walisafiri kutoka Ramesesi katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, siku iliyofuata Pasaka. Walitembea kwa ujasiri wazi mbele ya Wamisri wote,
Mwezi wa kwanza walisafiri kutoka Ramesi, waliondoka siku ya kumi na tano. Asubuhi siku iliyofuata baada ya Pasaka, Wana wa Israeli waliondoka wazi wazi, mbele ya machoya Wamisri wote.
4 waliokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza wote, ambao Bwana alikuwa amewaua katikati yao, kwa kuwa Bwana alikuwa ameleta hukumu juu ya miungu yao.
Hii ilitokea wakati Wamisiri walipokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza, ambao BWANA alikuwa amewaua miongoni mwao, kwa kuwa pia alikuwa ameiadhibu miungu yao.
5 Waisraeli waliondoka Ramesesi na kupiga kambi huko Sukothi.
Wana wa Israeli walisafiri kutoka Ramesi na kuweka kambi
6 Wakaondoka Sukothi na kupiga kambi huko Ethamu, pembeni mwa jangwa.
Sukothi. Walisafiri toka Sukothi na kuweka kambi Ethamu, mwisho wa nyika.
7 Wakaondoka Ethamu, wakageuka wakarudi Pi-Hahirothi, hadi mashariki ya Baal-Sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli.
Wakasafiri kutoka Ethamu wakarudi mpaka Pi-Hahirothi, ambayo inaikabili Baali Zephoni, ambapo waliweka kambi kuikabili Migidoli
8 Wakaondoka Pi-Hahirothi wakapita katikati ya bahari mpaka jangwani, na baada ya kusafiri kwa siku tatu katika Jangwa la Ethamu, walipiga kambi huko Mara.
Kisha wakasafiri toka mkabala wa Pi-Hairothi na kupita katikati ya bahari kuelekea nyikani. Wakasafiri safari ya siku tatu katika nyika ya Ethamu na kuweka kambi Mara.
9 Wakaondoka Mara wakaenda Elimu, mahali ambapo palikuwa na chemchemi kumi na mbili na mitende sabini, huko wakapiga kambi.
Wakasafiri kutoka Mara kufika Elimu. Pale Elimu kulikuwa na chemichemi kumi na mbili za maji na miti sabini ya mitende. hapo ndipo walipoweka kambi.
10 Wakaondoka Elimu na kupiga kambi kando ya Bahari ya Shamu.
Walisafiri kutoka Elimu na kuweka kambi karibu na Bahari ya Shamu.
11 Wakaondoka kando ya Bahari ya Shamu na kupiga kambi katika Jangwa la Sini.
Walisafiri kutoka Bahari ya Shamu na kuweka kambi katika nyika ya Sini.
12 Wakaondoka katika Jangwa la Sini, wakapiga kambi huko Dofka.
Walisafiri kutoka nyika ya Sini na kuweka kambi Dofka.
13 Wakaondoka Dofka, wakapiga kambi huko Alushi.
Wakasafiri kutoka Dofka na kuweka kambi Alushi.
14 Wakaondoka Alushi, wakapiga kambi Refidimu, mahali ambapo hapakuwa na maji kwa ajili ya watu kunywa.
Wakasafiri kutoka Alushi na kuweka kambi Refidimu, ambapo watu walikosa maji ya kunywa.
15 Wakaondoka Refidimu na kupiga kambi katika Jangwa la Sinai.
Walisafiri kutoka Refidimu na kuweka kambi kwenye nyika ya Sinai.
16 Wakaondoka katika Jangwa la Sinai na kupiga kambi huko Kibroth-Hataava.
Walisafiri kutoka nyika ya Sinai na kuweka kambi Kibrothi Hataava.
17 Wakaondoka Kibroth-Hataava na kupiga kambi huko Haserothi.
Walisafiri kutoka Kibrothi Hataava na kuweka kambi Hazerothi.
18 Wakaondoka Haserothi na kupiga kambi huko Rithma.
Walisafiri kutoka Hazerothi na kuweka kambi Rithima.
19 Wakaondoka Rithma na kupiga kambi huko Rimon-Peresi.
Walisafiri kutoka Rithima na kuweka kambi Rimoni Perezi.
20 Wakaondoka Rimon-Peresi na kupiga kambi huko Libna.
Walisafiri kutoka Rimoni Perezi na kuweka kambi Libna.
21 Wakaondoka Libna na kupiga kambi huko Risa.
Walisafiri kutoka Libna na kuweka kambi Risa.
22 Wakaondoka Risa na kupiga kambi huko Kehelatha.
Walisafiri kutoka Risa na kuweka kambi Kehelatha.
23 Wakaondoka Kehelatha na kupiga kambi kwenye mlima Sheferi.
Walisafiri kutoka Kehelatha na kuweka kambi kwenye Mlima Sheferi.
24 Wakaondoka kwenye mlima Sheferi na kupiga kambi huko Harada.
Walisafiri kutoka Mlima Sheferi na kuweka kambi Harada.
25 Wakaondoka Harada na kupiga kambi huko Makelothi.
Walisafiri kutoka Harada na kuweka kambi Makelothi.
26 Wakaondoka Makelothi na kupiga kambi huko Tahathi.
Walisafiri kutoka Makelothi na kuweka kambi Tahathi.
27 Wakaondoka Tahathi na kupiga kambi huko Tera.
Walisafiri kutoka Ttahalathi na kuweka kambi Tera.
28 Wakaondoka Tera na kupiga kambi huko Mithka.
Walisafiri kutokaTera na kuweka kambi Mithika.
29 Wakaondoka Mithka na kupiga kambi huko Hashmona.
Walisafiri kutoka Mithika na kuweka kambi Hashimona.
30 Wakaondoka Hashmona na kupiga kambi Moserothi.
Walisafiri kutoka Hashimona na kuweka kambi Moserothi.
31 Wakaondoka Moserothi na kupiga kambi huko Bene-Yakani.
Walisafiri kutoka Moserothi na kuweka kambi Bene Jaakani.
32 Wakaondoka Bene-Yakani na kupiga kambi huko Hor-Hagidgadi.
Walisafiri kutoka Bene Jaakani na kuweka kambi Hori Hagidigadi.
33 Wakaondoka Hor-Hagidgadi na kupiga kambi huko Yotbatha.
Walisafiri kutoka Hori Hagidigadi na kuweka kambi Jotibatha.
34 Wakaondoka Yotbatha na kupiga kambi huko Abrona.
Walisafiri kutoka Jotibatha na kuweka kambi Abrona.
35 Wakaondoka Abrona na kupiga kambi huko Esion-Geberi.
Walisafiri kutoka Abrona na kuweka kambi Ezioni Geberi.
36 Wakaondoka Esion-Geberi na kupiga kambi huko Kadeshi katika Jangwa la Sini.
Walisafiri toka Ezioini Geberi na kuweka kambi katika nyika ya Sini kule Kadeshi.
37 Wakaondoka Kadeshi na kupiga kambi kwenye Mlima Hori, mpakani mwa Edomu.
Walisafiri kutoka Kadeshi na kuweka kambi Mlima Hori, Pembezoni mwa nchi ya Edomu.
38 Kwa amri ya Bwana, kuhani Aroni alipanda Mlima Hori, mahali alipofia katika siku ya kwanza ya mwezi wa tano, mwaka wa arobaini baada ya Waisraeli kutoka Misri.
Hapo ndipo Haruni kuhani alipoenda kwenye Mlima Hori kwa amri ya BWANA na kufa kule mwaka wa arobaini bada ya Wisraeli kutoka katika nchi ya Misri, katika siku ya kwanza ya mwezi wa tano.
39 Aroni alikufa juu ya Mlima Hori akiwa na umri wa miaka 123.
Haruni alikuwa na umri wa mika 123 alipokufa pale juu ya Mlima Hori.
40 Mfalme Mkanaani wa Aradi, ambaye aliishi huko Negebu ya Kanaani, akasikia kwamba Waisraeli wanakuja.
Wakanaani, mfalme wa Aradi, ambao waliishi kusini mwa nyika katika nchi ya Kanaani, walisikia juu ya ujio wa wana wa Israeli.
41 Wakaondoka kwenye mlima Hori na kupiga kambi huko Salmona.
Walisafiri kutika Mlima Hori n a kuweka kambi Zalimona.
42 Wakaondoka Salmona, wakapiga kambi huko Punoni.
Walisafiri kutoka Zalimona na kuweka kambi Punoni.
43 Wakaondoka Punoni, wakapiga kambi huko Obothi.
Walisafiri kutoka Punoni na kuweka kambi Obothi.
44 Wakaondoka Obothi, wakapiga kambi huko Iye-Abarimu, mipakani mwa Moabu.
Walisafiri kutoka Obothi na kuweka kambi Abarimu, katika mpaka wa Moabu.
45 Wakaondoka Iye-Abarimu, wakapiga kambi huko Dibon-Gadi.
Walisafiri kutoka Abarimu na kuweka kambi Diboni Gadi.
46 Wakaondoka Dibon-Gadi na kupiga kambi huko Almon-Diblathaimu.
Walisafiri kutoka Diboni Gadi na kuweka kambi Alimoni Diblathaimu.
47 Wakaondoka Almon-Diblathaimu na kupiga kambi katika milima ya Abarimu, karibu na Nebo.
Walisafiri kutoka Alimoni Diblathaimu na kuweka kambi kwenye milima ya Abarimu mkabala na Nebo.
48 Wakaondoka kwenye milima ya Abarimu na kupiga kambi kwenye tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ngʼambo ya Yeriko.
Walisafiri kutoka mlima wa Abarimuna kuweka kambi kwenye nyanda za Moabu karibu na Yorodani huko Yeriko.
49 Huko kwenye tambarare za Moabu walipiga kambi kandokando ya Mto Yordani, kuanzia Beth-Yeshimothi mpaka Abel-Shitimu.
Waliweka kambi karibu na Yorodani, kutoka Bethi Jeshimothi mpaka Abeli Shitimu katika nyanda za Moabu.
50 Katika tambarare za Moabu kando ya Yordani kuvukia Yeriko, Bwana akamwambia Mose,
Hapo BWANA alinenana Musa katika nyanda za Moabu karibu na Yorodani kule Yeriko akasema,
51 “Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapovuka Mto Yordani kuingia Kanaani,
“Nena na wana wa Israeli uwaambie. 'Mtakapovuka mto Yorodani kuingia Kanaani,
52 wafukuzeni wakazi wote wa nchi iliyo mbele yenu. Haribuni sanamu zao zote za kuchongwa, na sanamu zilizotengenezwa kwa kuyeyusha chuma, na kupabomoa mahali pao pa ibada.
ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote mbele yenu. Mtaziharibu sanamu zote za kuchongwa. Mtaziharibu sanamu zao za kusubu na kuharibu mahali pao pote palipoinuka.
53 Mtaimiliki nchi hiyo na kukaa huko, kwa kuwa nimewapeni ninyi kuimiliki.
Mtachukua hiyo ardhi iwe mali yenu na muishi ndani yake, kwa sababu nimewapeni hiyo nchi iwe mali yenu.
54 Mtaigawanya nchi hiyo kwa kupiga kura, kufuatana na koo zenu. Kwa kundi kubwa zaidi toa urithi mkubwa zaidi, na kwa kundi dogo zaidi urithi mdogo zaidi. Chochote kinachowaangukia kwa kura kitakuwa chao. Mtaigawanya nchi kufuatana na makabila ya babu zenu.
Mtairithi hiyo nchi kwa kupiga kura, kwa kufuata kila ukoo. Kwa zile koo kubwa kubwa mtawapa sehemu kubwa ya ardhi, na kwa zile koo ndogo ndogo mtawapa sehemu ndogo ya ardhi. Kura itakapoanguka kwenye kila ukoo, hiyo ardhi itakuwa mali yake. Mtairithi ardhi kufuata ukoo wa kabilla la jamaa zenu.
55 “‘Lakini kama hamkuwafukuza wenyeji wakaao katika nchi hiyo, wale mtakaowaruhusu wabaki watakuwa kama sindano kwenye macho yenu na miiba kwenu kila upande. Watawasumbua katika nchi mtakayoishi.
Lakini kama hamtawafukuza wenyeji wa nchi hiyo watoke mbele yenu, ndipo wale watu mtakaowaruhusu wakae nanyi watakapokuwa kama sindano machoni mwenu na miiba katika mbavu zenu. Watayafanya maisha yenu yawe magumu katika nchi mnayoishi.
56 Kisha nitawatenda ninyi kile ambacho nimepanga kuwatenda wao.’”
Ndipo itakapotokea kuwa kile ambacho Mimi ninakusudia kufanya kwa wale watu, Nitawafanyia pia ninyi'”

< Hesabu 33 >