< Hesabu 32 >

1 Kabila la Wareubeni na Wagadi, waliokuwa na makundi makubwa ya ngʼombe, kondoo na mbuzi, waliona kuwa nchi ya Yazeri na nchi ya Gileadi ni nzuri kwa mifugo.
ומקנה רב היה לבני ראובן ולבני גד--עצום מאד ויראו את ארץ יעזר ואת ארץ גלעד והנה המקום מקום מקנה
2 Hivyo walimjia Mose, na kuhani Eleazari na viongozi wa jumuiya, na kuwaambia,
ויבאו בני גד ובני ראובן ויאמרו אל משה ואל אלעזר הכהן ואל נשיאי העדה לאמר
3 “Atarothi, Diboni, Yazeri, Nimra, Heshboni, Eleale, Sebamu, Nebo na Beoni,
עטרות ודיבן ויעזר ונמרה וחשבון ואלעלה ושבם ונבו ובען
4 nchi ambayo Bwana ameishinda mbele ya wana wa Israeli, inafaa kwa mifugo, nao watumishi wako wana mifugo.
הארץ אשר הכה יהוה לפני עדת ישראל--ארץ מקנה הוא ולעבדיך מקנה
5 Kama tumepata kibali mbele ya macho yako, nchi hii na ipewe watumishi wako kama milki yetu. Usitufanye tuvuke Yordani.”
ויאמרו אם מצאנו חן בעיניך--יתן את הארץ הזאת לעבדיך לאחזה אל תעברנו את הירדן
6 Mose akawaambia Wagadi na Wareubeni, “Je, watu wa nchi yenu watakwenda vitani wakati ninyi mmeketi hapa?
ויאמר משה לבני גד ולבני ראובן האחיכם יבאו למלחמה ואתם תשבו פה
7 Kwa nini mmewakatisha Waisraeli tamaa wasivuke katika nchi ambayo Bwana amewapa?
ולמה תנואון (תניאון) את לב בני ישראל--מעבר אל הארץ אשר נתן להם יהוה
8 Hivi ndivyo baba zenu walivyofanya wakati nilipowatuma kutoka Kadesh-Barnea kuipeleleza nchi.
כה עשו אבתיכם בשלחי אתם מקדש ברנע לראות את הארץ
9 Baada ya kufika kwenye Bonde la Eshkoli na kuitazama nchi, waliwakatisha tamaa Waisraeli wasiingie katika nchi ambayo Bwana alikuwa amewapa.
ויעלו עד נחל אשכול ויראו את הארץ ויניאו את לב בני ישראל--לבלתי בא אל הארץ אשר נתן להם יהוה
10 Siku ile hasira ya Bwana iliwaka naye akaapa kiapo hiki:
ויחר אף יהוה ביום ההוא וישבע לאמר
11 ‘Kwa kuwa hawakunifuata kwa moyo wote, hakuna mtu yeyote mwenye miaka ishirini au zaidi ambaye alikuja kutoka Misri atakayeona nchi niliyoahidi kwa kiapo kwa Abrahamu, Isaki na Yakobo;
אם יראו האנשים העלים ממצרים מבן עשרים שנה ומעלה את האדמה אשר נשבעתי לאברהם ליצחק וליעקב כי לא מלאו אחרי
12 hakuna hata mmoja isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, Mkenizi, na Yoshua mwana wa Nuni, kwa sababu walimfuata Bwana kwa moyo wote.’
בלתי כלב בן יפנה הקנזי ויהושע בן נון כי מלאו אחרי יהוה
13 Hasira ya Bwana iliwaka dhidi ya Waisraeli na akawafanya watangetange katika jangwa kwa miaka arobaini, mpaka kizazi chote cha wale waliofanya maovu mbele yake kimeangamia.
ויחר אף יהוה בישראל וינעם במדבר ארבעים שנה--עד תם כל הדור העשה הרע בעיני יהוה
14 “Nanyi mko hapa, uzao wa wenye dhambi, mkisimamia mahali pa baba zenu na mkimfanya Bwana kuwakasirikia Waisraeli hata zaidi.
והנה קמתם תחת אבתיכם--תרבות אנשים חטאים לספות עוד על חרון אף יהוה--אל ישראל
15 Kama mkigeuka na mkiacha kumfuata, atawaacha tena watu hawa wote jangwani, na mtakuwa sababu ya maangamizi yao.”
כי תשובן מאחריו ויסף עוד להניחו במדבר ושחתם לכל העם הזה
16 Ndipo wakamjia Mose na kumwambia, “Tungalitaka kujenga mazizi hapa kwa ajili ya mifugo yetu na miji kwa ajili ya wanawake wetu na watoto.
ויגשו אליו ויאמרו גדרת צאן נבנה למקננו פה וערים לטפנו
17 Lakini sisi tuko tayari kuchukua silaha zetu na kutangulia mbele ya Waisraeli mpaka tutakapowaleta mahali pao. Wakati huo wanawake wetu na watoto wataishi katika miji yenye ngome, kwa ajili ya ulinzi dhidi ya wenyeji wa nchi.
ואנחנו נחלץ חשים לפני בני ישראל עד אשר אם הביאנם אל מקומם וישב טפנו בערי המבצר מפני ישבי הארץ
18 Hatutarudi nyumbani mwetu mpaka kila Mwisraeli apokee urithi wake.
לא נשוב אל בתינו--עד התנחל בני ישראל איש נחלתו
19 Hatutapokea urithi wowote pamoja nao ngʼambo ya Yordani, kwa sababu urithi wetu umekuja kwetu upande wa mashariki ya Yordani.”
כי לא ננחל אתם מעבר לירדן והלאה כי באה נחלתנו אלינו מעבר הירדן מזרחה
20 Kisha Mose akawaambia, “Kama mtafanya jambo hili, kama mtajivika silaha mbele za Bwana kwa ajili ya vita,
ויאמר אליהם משה אם תעשון את הדבר הזה אם תחלצו לפני יהוה למלחמה
21 na kama ninyi nyote mtakwenda mmejivika silaha ngʼambo ya Yordani mbele za Bwana mpaka awe amewafukuza adui zake mbele zake,
ועבר לכם כל חלוץ את הירדן לפני יהוה עד הורישו את איביו מפניו
22 hadi wakati nchi itakapokuwa imeshindwa mbele za Bwana, ndipo mtaweza kurudi na kuwa huru kutoka masharti yenu kwa Bwana na Israeli. Nayo nchi hii itakuwa milki yenu mbele za Bwana.
ונכבשה הארץ לפני יהוה ואחר תשבו--והייתם נקים מיהוה ומישראל והיתה הארץ הזאת לכם לאחזה--לפני יהוה
23 “Lakini mkishindwa kufanya hili, mtakuwa mnatenda dhambi dhidi ya Bwana; nanyi kuweni na hakika kuwa dhambi yenu itawapata.
ואם לא תעשון כן הנה חטאתם ליהוה ודעו חטאתכם אשר תמצא אתכם
24 Jengeni miji kwa ajili ya wanawake na watoto wenu, na mazizi kwa ajili ya mbuzi na kondoo zenu, lakini fanyeni yale mliyoahidi.”
בנו לכם ערים לטפכם וגדרת לצנאכם והיצא מפיכם תעשו
25 Wagadi na Wareubeni wakamwambia Mose, “Sisi watumishi wako tutafanya kama bwana wetu anavyotuagiza.
ויאמר בני גד ובני ראובן אל משה לאמר עבדיך יעשו כאשר אדני מצוה
26 Watoto na wake zetu, makundi ya mbuzi na kondoo, na makundi ya ngʼombe zetu, watabaki hapa katika miji ya Gileadi.
טפנו נשינו מקננו וכל בהמתנו--יהיו שם בערי הגלעד
27 Lakini watumishi wenu, kila mwanaume aliyevaa silaha za vita, watavuka ngʼambo kupigana mbele za Bwana, sawa kama bwana wetu anavyosema.”
ועבדיך יעברו כל חלוץ צבא לפני יהוה--למלחמה כאשר אדני דבר
28 Kisha Mose akatoa amri kuhusu wao kwa kuhani Eleazari, na Yoshua mwana wa Nuni na viongozi wa jamaa za makabila ya Waisraeli.
ויצו להם משה את אלעזר הכהן ואת יהושע בן נון ואת ראשי אבות המטות לבני ישראל
29 Mose akawaambia, “Ikiwa Wagadi na Wareubeni, kila mwanaume aliyevaa silaha za vita, atavuka Yordani pamoja nanyi mbele za Bwana, basi wakati mtakapoishinda nchi iliyoko mbele yenu, wapeni nchi ya Gileadi kama milki yao.
ויאמר משה אלהם אם יעברו בני גד ובני ראובן אתכם את הירדן כל חלוץ למלחמה לפני יהוה ונכבשה הארץ לפניכם--ונתתם להם את ארץ הגלעד לאחזה
30 Lakini kama hawatavuka pamoja nanyi wakiwa wamevaa silaha za vita, lazima wakubali kupokea milki yao pamoja nanyi katika nchi ya Kanaani.”
ואם לא יעברו חלוצים אתכם--ונאחזו בתככם בארץ כנען
31 Wagadi na Wareubeni wakajibu, “Watumishi wako watafanya lile Bwana alilosema.
ויענו בני גד ובני ראובן לאמר את אשר דבר יהוה אל עבדיך כן נעשה
32 Tutavuka mbele za Bwana kuingia Kanaani tukiwa tumevaa silaha za vita, lakini mali tutakayoirithi itakuwa ngʼambo hii ya Yordani.”
נחנו נעבר חלוצים לפני יהוה ארץ כנען ואתנו אחזת נחלתנו מעבר לירדן
33 Kisha Mose akawapa Wagadi, Wareubeni, na nusu ya kabila la Manase mwana wa Yosefu ufalme wa Sihoni mfalme wa Waamori, na ufalme wa Ogu mfalme wa Bashani, nchi yote pamoja na miji yake, na nchi inayowazunguka.
ויתן להם משה לבני גד ולבני ראובן ולחצי שבט מנשה בן יוסף את ממלכת סיחן מלך האמרי ואת ממלכת עוג מלך הבשן הארץ לעריה בגבלת--ערי הארץ סביב
34 Wagadi wakajenga Diboni, Atarothi, Aroeri,
ויבנו בני גד את דיבן ואת עטרת ואת ערער
35 Atroth-Shofani, Yazeri, Yogbeha,
ואת עטרת שופן ואת יעזר ויגבהה
36 Beth-Nimra na Beth-Harani kama miji iliyozungushiwa ngome, tena wakajenga mazizi kwa ajili ya makundi yao ya mbuzi na kondoo.
ואת בית נמרה ואת בית הרן ערי מבצר וגדרת צאן
37 Nao Wareubeni wakajenga upya miji ya Heshboni, Eleale na Kiriathaimu,
ובני ראובן בנו את חשבון ואת אלעלא ואת קריתים
38 pia Nebo na Baal-Meoni (majina ya hiyo miji yalibadilishwa) na Sibma. Miji waliyoijenga upya waliipa majina.
ואת נבו ואת בעל מעון מוסבת שם--ואת שבמה ויקראו בשמת את שמות הערים אשר בנו
39 Wazao wa Makiri mwana wa Manase walikwenda Gileadi, wakaiteka nchi na kuwafukuza Waamori waliokuwa huko.
וילכו בני מכיר בן מנשה גלעדה--וילכדה ויורש את האמרי אשר בה
40 Kwa hiyo Mose akawapa Wamakiri, wazao wa Manase, nchi ya Gileadi, nao wakakaa huko.
ויתן משה את הגלעד למכיר בן מנשה וישב בה
41 Yairi, mzao wa Manase, akateka makao yao, akayaita Hawoth-Yairi.
ויאיר בן מנשה הלך וילכד את חותיהם ויקרא אתהן חות יאיר
42 Naye Noba akateka Kenathi na makao yaliyoizunguka, akayaita Noba kwa jina lake.
ונבח הלך וילכד את קנת ואת בנתיה ויקרא לה נבח בשמו

< Hesabu 32 >