< Hesabu 27 >
1 Binti za Selofehadi mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, walikuwa wa koo za Manase mwana wa Yosefu. Majina ya hao binti yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa. Walikaribia
那時,若瑟的兒子默納協家族內,責羅斐哈得的女兒們前來,──責羅斐得是赫斐爾的兒子,赫斐爾是基肋阿得的兒子,基肋阿得是瑪基爾的兒子,瑪基爾是默納協的兒子;她們的名字是瑪赫拉、諾阿、曷革拉、米耳加和提爾匝。
2 ingilio la Hema la Kukutania na kusimama mbele ya Mose, kuhani Eleazari, viongozi na kusanyiko lote, wakasema,
她們站在梅瑟、大司祭厄肋阿匝爾、眾領袖和全會眾前,即會幕門口說:
3 “Baba yetu alikufa jangwani. Hakuwa miongoni mwa wafuasi wa Kora, ambao walifungamana pamoja dhidi ya Bwana, lakini alikufa kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe na hakuacha wana.
「我們的父親死在曠野,但他並不是科辣黑黨派中,結黨反抗上主的黨徒,他只是因自已的罪死了,沒有留下兒子。
4 Kwa nini jina la baba yetu lifutike kutoka ukoo wake kwa sababu hakuwa na mwana? Tupatie milki miongoni mwa ndugu za baba yetu.”
為什麼讓我們父親的名字,因為沒有兒子,就由本族中消滅﹖讓我們在我們父親的兄弟中,也分得一份產業」。
5 Kwa hiyo Mose akalileta shauri lao mbele za Bwana,
梅瑟就將她們的案件呈到上主前;
6 naye Bwana akamwambia Mose,
上主訓示梅瑟說:
7 “Wanachosema binti za Selofehadi ni sawa. Ni lazima kwa hakika uwape milki kama urithi miongoni mwa ndugu za baba yao, na kubadili urithi wa baba yao uwe wao.
「責羅哈特的女兒們說得有理;你應在她們父親兄弟中分給她們一份產業,將她們父親的產業轉讓給她們。
8 “Waambie Waisraeli, ‘Ikiwa mtu atakufa naye hakuacha mwana, utampa binti yake urithi wake.
並且你應教訓以色列子民說:一個人死了,若沒有兒子,你們應將他的產業轉讓給他的女兒;
9 Ikiwa hana binti, wape ndugu zake wa kiume urithi wake.
如果連女兒也沒有,應將他的產業分給他的兄弟們。
10 Ikiwa hana ndugu wa kiume toa urithi wake kwa ndugu za baba yake.
如果連一個兄弟也沒有,應將他的產業分給他父親的兄弟們。
11 Ikiwa baba yake hakuwa na ndugu wa kiume, toa urithi wake kwa ndugu wa karibu katika ukoo wake, ili aumiliki. Hili litakuwa dai la sheria kwa Waisraeli, kama Bwana alivyomwamuru Mose.’”
如果他的父親也沒有兄弟,應將他的產業分給他家族中與他最近的親屬,他應繼承產業:這是以色列子民當守的法令,如上主對梅瑟所吩咐的」。
12 Kisha Bwana akamwambia Mose, “Panda juu ya mlima huu katika kilele cha Abarimu uione nchi ambayo nimewapa Waisraeli.
上主對梅瑟說:「你上這座阿巴陵山上去,看一看我賜給以色列子民的地方。
13 Baada ya kuiona, wewe pia utakusanywa pamoja na watu wako kama ndugu yako Aroni alivyokusanywa,
你看了以後,你也畏歸到你親屬那裏去,如你哥哥亞郎歸去一樣。
14 kwa kuwa jumuiya ilipoasi amri yangu kwenye maji katika Jangwa la Sini, wakati jumuiya ilipogombana nami, nyote wawili mliacha kuitii amri yangu ya kuniheshimu kama mtakatifu mbele ya macho yao.” (Haya yalikuwa maji ya Meriba huko Kadeshi, katika Jangwa la Sini.)
因為在親曠野裏,當會眾反叛我時,我命你們在他們眼前以取水顯我為聖時,你們違背 了我的命令」。[這是指在親曠野中,在卡德士的默黎巴取水的事。]
15 Mose akamwambia Bwana,
梅瑟向上主說:
16 “Bwana, Mungu wa roho zote za wanadamu, na amteue mtu juu ya jumuiya hii
「望上主,賜給一切血肉氣息的天主,委派一人管理會眾,
17 ili atoke na kuingia mbele yao, atakayewaongoza katika kutoka kwao na kuingia kwao, ili watu wa Bwana wasiwe kama kondoo wasio na mchungaji.”
叫他處理他們的事件,領導他們出入,免得上主的會眾如無牧之羊」。
18 Kwa hiyo Bwana akamwambia Mose, “Mchukue Yoshua mwana wa Nuni, mtu ambaye Roho yuko ndani yake, uweke mkono juu yake.
上主對梅瑟說:「你應用農的兒子若蘇厄,他是個有精神的人,按手在他身上,
19 Msimamishe mbele ya kuhani Eleazari pamoja na kusanyiko lote, umpe maagizo mbele yao.
叫他站在大司祭厄肋阿匝爾和全會眾前,當著他們的面委派他。
20 Mpe sehemu ya mamlaka yako ili jumuiya yote ya Waisraeli ipate kumtii.
他將你的一些威權授給他,好叫以色列子民全會眾聽從他。
21 Atasimama mbele ya kuhani Eleazari, ambaye atapokea maamuzi kwa ajili yake, kwa kuuliza mbele za Bwana kwa ile Urimu. Kwa amri yake, yeye na jumuiya yote ya Waisraeli watatoka, na kwa amri yake, wataingia.”
他應到大司祭厄肋阿匝爾面前,請司祭為他在上主面前咨詢「烏陵」的決斷,他和一切以色列子民及全會眾,應依照指示去行事」。
22 Mose akafanya kama Bwana alivyomwagiza. Akamtwaa Yoshua na kumsimamisha mbele ya kuhani Eleazari na kusanyiko lote.
梅瑟就照上主吩咐他的做了;選用了若蘇厄,叫他站在大司祭厄肋阿匝爾和全會眾前,
23 Kisha akaweka mikono yake juu ya kichwa cha Yoshua na kumpa maagizo, kama vile Bwana alivyoelekeza kupitia kwa Mose.
按 手在他身上,委派了他,全照上主藉著梅瑟所吩咐的。