< Hesabu 25 >

1 Israeli alipokuwa akikaa Shitimu, wanaume wa Israeli walianza kuzini na wanawake wa Kimoabu,
以色列人住在什亭,百姓與摩押女子行起淫亂。
2 ambao waliwaalika kushiriki katika kutoa kafara kwa miungu yao. Watu wakala na kusujudu mbele ya miungu hii.
因為這女子叫百姓來,一同給她們的神獻祭,百姓就吃她們的祭物,跪拜她們的神。
3 Kwa hiyo Israeli akaungana katika kumwabudu Baali wa Peori. Hasira ya Bwana ikawaka dhidi yao.
以色列人與巴力‧毗珥連合,耶和華的怒氣就向以色列人發作。
4 Bwana akamwambia Mose, “Uwachukue viongozi wote wa watu hawa, uwaue na uwaweke hadharani mchana peupe mbele za Bwana, ili hasira kali ya Bwana iweze kuondoka kwa Israeli.”
耶和華吩咐摩西說:「將百姓中所有的族長在我面前對着日頭懸掛,使我向以色列人所發的怒氣可以消了。」
5 Kwa hiyo Mose akawaambia waamuzi wa Israeli, “Kila mmoja wenu lazima awaue wale wanaume wenu, walioshiriki katika kumwabudu Baali wa Peori.”
於是摩西吩咐以色列的審判官說:「凡屬你們的人,有與巴力‧毗珥連合的,你們各人要把他們殺了。」
6 Ndipo mwanaume wa Kiisraeli akamleta mwanamke wa Kimidiani katika jamaa yake palepale mbele ya Mose na mkutano wote wa Israeli walipokuwa wakilia kwenye lango la Hema la Kukutania.
摩西和以色列全會眾正在會幕門前哭泣的時候,誰知,有以色列中的一個人,當他們眼前,帶着一個米甸女人到他弟兄那裏去。
7 Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani Aroni, alipoona jambo hili, akaondoka kwenye kusanyiko, akachukua mkuki mkononi mwake,
祭司亞倫的孫子,以利亞撒的兒子非尼哈看見了,就從會中起來,手裏拿着槍,
8 akamfuata yule Mwisraeli ndani ya hema. Akawachoma mkuki wote wawili kwa pamoja, ukapenya kwenye mwili wa yule Mwisraeli na mwili wa yule mwanamke. Ndipo tauni iliyokuwepo dhidi ya Waisraeli ikakoma.
跟隨那以色列人進亭子裏去,便將以色列人和那女人由腹中刺透。這樣,在以色列人中瘟疫就止息了。
9 Lakini wale waliokufa kwa hiyo tauni walikuwa watu 24,000.
那時遭瘟疫死的,有二萬四千人。
10 Bwana akamwambia Mose,
耶和華曉諭摩西說:
11 “Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani Aroni, amegeuza hasira yangu mbali na Waisraeli, kwa sababu alikuwa na wivu kama nilio nao kwa heshima yangu miongoni mwao, hata kwamba kwa wivu wangu sikuwaangamiza.
「祭司亞倫的孫子,以利亞撒的兒子非尼哈,使我向以色列人所發的怒消了;因他在他們中間,以我的忌邪為心,使我不在忌邪中把他們除滅。
12 Kwa hiyo mwambie Finehasi ninafanya Agano langu la amani naye.
因此,你要說:『我將我平安的約賜給他。
13 Yeye pamoja na wazao wake watakuwa na Agano la ukuhani milele, kwa sababu alikuwa na wivu kwa ajili ya heshima ya Mungu wake, na akafanya upatanisho kwa Waisraeli.”
這約要給他和他的後裔,作為永遠當祭司職任的約;因他為上帝有忌邪的心,為以色列人贖罪。』」
14 Jina la Mwisraeli ambaye aliuawa pamoja na mwanamke wa Kimidiani ni Zimri mwana wa Salu, kiongozi wa jamaa ya Simeoni.
那與米甸女人一同被殺的以色列人,名叫心利,是撒路的兒子,是西緬一個宗族的首領。
15 Jina la mwanamke wa Kimidiani aliyeuawa ni Kozbi binti wa Suri, aliyekuwa mkuu wa kabila la jamaa ya Wamidiani.
那被殺的米甸女人,名叫哥斯比,是蘇珥的女兒;這蘇珥是米甸一個宗族的首領。
16 Bwana akamwambia Mose,
耶和華曉諭摩西說:
17 “Watendeeni Wamidiani kama adui na mwaue,
「你要擾害米甸人,擊殺他們;
18 kwa sababu wao waliwatendea kama adui wakati waliwadanganya katika tukio la Peori na dada yao Kozbi, binti wa kiongozi wa Kimidiani, mwanamke ambaye aliuawa wakati tauni ilikuja kama matokeo ya tukio la Peori.”
因為他們用詭計擾害你們,在毗珥的事上和他們的姊妹、米甸首領的女兒哥斯比的事上,用這詭計誘惑了你們;這哥斯比,當瘟疫流行的日子,因毗珥的事被殺了。」

< Hesabu 25 >