< Hesabu 21 >

1 Mfalme wa Kikanaani wa Aradi aliyeishi huko Negebu aliposikia kwamba Waisraeli walikuwa wanakuja kwa njia ya Atharimu, aliwashambulia Waisraeli na kuwateka baadhi yao.
וישמע הכנעני מלך ערד ישב הנגב כי בא ישראל דרך האתרים וילחם בישראל וישב ממנו שבי
2 Ndipo Israeli akaweka nadhiri hii kwa Bwana: “Ikiwa utawatia watu hawa mikononi mwetu, tutaiangamiza kabisa miji yao.”
וידר ישראל נדר ליהוה ויאמר אם נתן תתן את העם הזה בידי--והחרמתי את עריהם
3 Bwana akasikiliza ombi la Waisraeli, naye akawapa ushindi juu ya Wakanaani. Wakawaangamiza kabisa na miji yao; hivyo mahali pale pakaitwa Horma.
וישמע יהוה בקול ישראל ויתן את הכנעני ויחרם אתהם ואת עריהם ויקרא שם המקום חרמה
4 Waisraeli wakasafiri kutoka mlima Hori kupitia njia inayoelekea Bahari ya Shamu, kuizunguka Edomu. Lakini watu wakakosa uvumilivu njiani,
ויסעו מהר ההר דרך ים סוף לסבב את ארץ אדום ותקצר נפש העם בדרך
5 wakamnungʼunikia Mungu na Mose, wakisema, “Kwa nini umetupandisha kutoka Misri ili tufe jangwani? Hakuna mkate! Hakuna maji! Nasi tunachukia sana chakula hiki duni!”
וידבר העם באלהים ובמשה למה העליתנו ממצרים למות במדבר כי אין לחם ואין מים ונפשנו קצה בלחם הקלקל
6 Ndipo Bwana akapeleka nyoka wenye sumu katikati yao; wakawauma watu, nao Waisraeli wengi wakafa.
וישלח יהוה בעם את הנחשים השרפים וינשכו את העם וימת עם רב מישראל
7 Watu wakamjia Mose na kusema, “Tumetenda dhambi wakati tuliponena dhidi ya Bwana na dhidi yako. Mwombe Bwana ili atuondolee hawa nyoka.” Hivyo Mose akawaombea hao watu.
ויבא העם אל משה ויאמרו חטאנו כי דברנו ביהוה ובך--התפלל אל יהוה ויסר מעלינו את הנחש ויתפלל משה בעד העם
8 Bwana akamwambia Mose, “Tengeneza nyoka wa shaba na umweke juu ya mti; yeyote aliyeumwa na nyoka anaweza kumtazama na akaishi tena.”
ויאמר יהוה אל משה עשה לך שרף ושים אתו על נס והיה כל הנשוך וראה אתו וחי
9 Kwa hiyo Mose akatengeneza nyoka wa shaba na kumweka juu ya mti. Kisha wakati mtu yeyote aliumwa na nyoka, naye akamtazama yule nyoka wa shaba, aliishi.
ויעש משה נחש נחשת וישמהו על הנס והיה אם נשך הנחש את איש--והביט אל נחש הנחשת וחי
10 Waisraeli waliendelea na safari yao na wakapiga kambi huko Obothi.
ויסעו בני ישראל ויחנו באבת
11 Kisha wakaondoka Obothi na kupiga kambi huko Iye-Abarimu, katika jangwa linalotazamana na Moabu kuelekea mawio ya jua.
ויסעו מאבת ויחנו בעיי העברים במדבר אשר על פני מואב ממזרח השמש
12 Kutoka hapo waliendelea mbele wakapiga kambi kwenye Bonde la Zeredi.
משם נסעו ויחנו בנחל זרד
13 Wakasafiri kutoka hapo na kupiga kambi kando ya Mto Arnoni, ambao uko katika jangwa lililoenea hadi nchi ya Waamori. Arnoni ni mpaka wa Moabu, kati ya Moabu na Waamori.
משם נסעו ויחנו מעבר ארנון אשר במדבר היצא מגבל האמרי כי ארנון גבול מואב בין מואב ובין האמרי
14 Ndiyo sababu Kitabu cha Vita vya Bwana kinasema: “…Mji wa Wahebu nchini Seifa na mabonde ya Arnoni,
על כן יאמר בספר מלחמת יהוה את והב בסופה ואת הנחלים ארנון
15 na miteremko ya mabonde inayofika hadi mji wa Ari na huelekea mpakani mwa Moabu.”
ואשד הנחלים אשר נטה לשבת ער ונשען לגבול מואב
16 Kutoka hapo waliendelea mbele hadi kisima cha Beeri; kwenye kisima ambacho Bwana alimwambia Mose, “Wakusanye watu pamoja, nami nitawapa maji.”
ומשם בארה הוא הבאר אשר אמר יהוה למשה אסף את העם ואתנה להם מים
17 Kisha Israeli akaimba wimbo huu: “Bubujika, ee kisima! Imba kuhusu maji,
אז ישיר ישראל את השירה הזאת עלי באר ענו לה
18 kuhusu kisima ambacho kilichimbwa na wakuu, ambacho watu mashuhuri walikifukua, watu mashuhuri wakiwa na fimbo za utawala na bakora.” Kisha wakatoka jangwani kwenda Matana,
באר חפרוה שרים כרוה נדיבי העם במחקק במשענתם וממדבר מתנה
19 kutoka Matana wakafika Nahalieli, kutoka Nahalieli wakafika Bamothi,
וממתנה נחליאל ומנחליאל במות
20 na kutoka Bamothi wakafika kwenye bonde lililoko Moabu, mahali ambapo kilele cha Pisga kinatazamana na nyika.
ומבמות הגיא אשר בשדה מואב--ראש הפסגה ונשקפה על פני הישימן
21 Israeli akawatuma wajumbe kumwambia Sihoni mfalme wa Waamori:
וישלח ישראל מלאכים אל סיחן מלך האמרי לאמר
22 “Uturuhusu tupite katika nchi yako. Hatutageuka kando kwenda katika mashamba au mashamba ya mizabibu, ama kunywa maji kutoka kisima chochote. Tutasafiri kwenye njia kuu ya mfalme hata tutakapokuwa tumekwisha kupita katika nchi yako.”
אעברה בארצך לא נטה בשדה ובכרם--לא נשתה מי באר בדרך המלך נלך עד אשר נעבר גבלך
23 Lakini Sihoni hakumruhusu Israeli apite katika nchi yake. Alilikutanisha jeshi lake lote, wakaondoka kwenda jangwani ili kupigana na Israeli. Alipofika huko Yahazi, akapigana na Israeli.
ולא נתן סיחן את ישראל עבר בגבלו ויאסף סיחן את כל עמו ויצא לקראת ישראל המדברה ויבא יהצה וילחם בישראל
24 Hata hivyo, Israeli alimshinda kwa upanga na kuiteka ardhi yake kutoka Arnoni mpaka Yaboki, lakini ni hadi kufikia nchi ya Waamoni tu, kwa sababu mipaka yake ilikuwa imezungushwa ukuta.
ויכהו ישראל לפי חרב ויירש את ארצו מארנן עד יבק עד בני עמון--כי עז גבול בני עמון
25 Israeli akaiteka miji yote ya Waamori na kuikalia, pamoja na Heshboni na makazi yote yanayoizunguka.
ויקח ישראל את כל הערים האלה וישב ישראל בכל ערי האמרי בחשבון ובכל בנתיה
26 Heshboni ulikuwa mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alikuwa amepigana dhidi ya mfalme wa Moabu aliyetangulia na akawa amechukua ardhi yake yote mpaka Arnoni.
כי חשבון--עיר סיחן מלך האמרי הוא והוא נלחם במלך מואב הראשון ויקח את כל ארצו מידו עד ארנן
27 Ndiyo sababu watunga mashairi husema: “Njoo Heshboni na ujengwe tena; mji wa Sihoni na ufanywe upya.
על כן יאמרו המשלים באו חשבון תבנה ותכונן עיר סיחון
28 “Moto uliwaka kutoka Heshboni, mwali wa moto kutoka mji wa Sihoni. Uliteketeza Ari ya Moabu, raiya wa mahali pa Arnoni palipoinuka.
כי אש יצאה מחשבון להבה מקרית סיחן אכלה ער מואב בעלי במות ארנן
29 Ole wako, ee Moabu! Umeharibiwa, enyi watu wa Kemoshi! Amewatoa wanawe kuwa wakimbizi, na binti zake kama mateka kwa Mfalme Sihoni wa Waamori.
אוי לך מואב אבדת עם כמוש נתן בניו פליטם ובנתיו בשבית למלך אמרי סיחון
30 “Lakini tumewashinda; Heshboni umeharibiwa hadi Diboni. Tumebomoa hadi kufikia Nofa, ulioenea hadi Medeba.”
ונירם אבד חשבון עד דיבן ונשים עד נפח אשר עד מידבא
31 Kwa hiyo Israeli akaishi katika nchi ya Waamori.
וישב ישראל בארץ האמרי
32 Baada ya Mose kutuma wapelelezi kwenda mji wa Yazeri, Waisraeli waliteka viunga vya mji huo na kuwafukuza Waamori waliokuwa wanaishi huko.
וישלח משה לרגל את יעזר וילכדו בנתיה ויירש (ויורש) את האמרי אשר שם
33 Kisha wakageuka na kwenda katika njia inayoelekea Bashani, naye Ogu mfalme wa Bashani pamoja na jeshi lake lote wakatoka kupigana nao huko Edrei.
ויפנו ויעלו דרך הבשן ויצא עוג מלך הבשן לקראתם הוא וכל עמו למלחמה--אדרעי
34 Bwana akamwambia Mose, “Usimwogope Ogu, kwa sababu nimeshamkabidhi mikononi mwako, pamoja na jeshi lake lote na nchi yake. Mtendee kama ulivyomtendea Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.”
ויאמר יהוה אל משה אל תירא אתו--כי בידך נתתי אתו ואת כל עמו ואת ארצו ועשית לו--כאשר עשית לסיחן מלך האמרי אשר יושב בחשבון
35 Kwa hiyo wakamuua, pamoja na wanawe na jeshi lake lote, bila ya kumwacha hata mtu mmoja hai. Nao wakaimiliki nchi yake.
ויכו אתו ואת בניו ואת כל עמו עד בלתי השאיר לו שריד ויירשו את ארצו

< Hesabu 21 >