< Hesabu 19 >
1 Bwana akamwambia Mose na Aroni:
BWANA akanena na Musa na Haruni, Akasema,
2 “Hivi ndivyo sheria ambayo Bwana ameagiza itakavyo: Waambie Waisraeli wakuletee mtamba mwekundu asiye na dosari wala waa, na ambaye hajapata kufungwa nira.
“Hii ni amri, ni sheria ninayokuamuru: Waambie wana waIsraeli wakuletee ng'ombe mke mwekundu asiyekuwa na kipaku wala waa, ambaye hajawahi kubeba nira.
3 Mpeni kuhani Eleazari huyo mtamba; naye atatolewa nje ya kambi na kuchinjwa mbele yake huyo kuhani.
Mpatie Eliazari kuhani huyo ng'ombe jike. Naye atamtoa nje ya kambi, na mtu mmoja amchinje mbele yake.
4 Kisha kuhani Eleazari atachukua baadhi ya damu yake kwenye kidole chake na kuinyunyiza mara saba kuelekea upande wa mbele ya Hema la Kukutania.
Kisha Eliazari kuhani atachukua sehemu ya damu yake kwa kidole chake na kuinyunyiza mara saba akielekea sehemu ya mbele ya ile hema ya kukutania.
5 Wakati angali akitazama, mtamba huyo atateketezwa: ngozi yake, nyama yake, damu na sehemu zake za ndani.
Na kuhani mwingine atamchoma huyo ng'ombe mbele ya macho yake. Ataichoma ngozi yake, nyama yake, na damu yake pamoja na mavi yake,
6 Kuhani atachukua kuni za mti wa mwerezi, hisopo na sufu nyekundu, na kuvitupa kwenye huyo mtamba anayeungua.
Yule kuhani atachukua mti wa mwerezi, na hisopo na sufu na kivitupa katikati ya huyo ng'ombe anayechomwa.
7 Baada ya hayo, kuhani lazima afue nguo zake, na aoge mwili wake kwa maji. Kisha anaweza kurudi kambini, lakini atakuwa najisi kwa kawaida ya ibada mpaka jioni.
Kisha atazifua nguo zake na kuoga kwenye maji. Ndipo atakuja kambini, ambapo atabaki najisi mpaka jioni ya siku hiyo.
8 Mtu amchomaye huyo mtamba lazima naye pia afue nguo zake na kuoga kwa maji, naye pia atakuwa najisi mpaka jioni.
Yule aliyemchoma huyo ng'ombe mke atafua nguo zake kwa maji na kuoga majini. Naye atabaki najisi mpaka jioni ya siku ile.
9 “Mtu ambaye ni safi atakusanya majivu ya mtamba huyo na kuyaweka mahali ambapo ni safi nje ya kambi kwa taratibu za kiibada. Yatahifadhiwa na jumuiya ya Kiisraeli kwa matumizi katika maji ya utakaso; ni kwa ajili ya kutakasa kutoka dhambini.
Baadaye mtu aliyesafi atayakusanya hayo majivu ya ng'ombe huyo na kuyaweka nje ya kambi kwenye eneo safi. Majivu haya yatatunzwa kwa ajili ya jamii ya watu wa Israeli. Watayachanganya majivu na maji kwa ajili ya utakaso wa dhambi, kwa kuwa majivu yalitokana na sadaka ya dhambi.
10 Mtu akusanyaye majivu ya huyo mtamba ni lazima pia afue nguo zake, kadhalika naye pia atakuwa najisi hadi jioni. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa Waisraeli na kwa wageni wanaoishi miongoni mwao.
Yule aliyeyakusanya majivu ya ng'ombe huyo lazima afue mavazi yake. Atabaki najisi mpaka jioni ya siku ile. Hii itakuwa sheria ya kudumu kwa watu wa Israeli na kwa wageni wanaoishi nao.
11 “Mtu yeyote agusaye maiti ya mtu yeyote atakuwa najisi kwa siku saba.
Yeyote atakayegusa maiti ya mtu atakuwa najisi kwa siku saba.
12 Ni lazima ajitakase mwenyewe kwa maji katika siku ya tatu na siku ya saba, ndipo atakuwa safi. Lakini kama hatajitakasa mwenyewe katika siku ya tatu na ya saba, hatakuwa safi.
Mtu wa jinsi hiyo atajitakasa mwenyewe siku ya tatu na siku ya saba. Ndipo atakapokuwa safi. Lakini kama hatajitakasa mwenyewe katika siku ya tatu, basi hatakuwa safi siku ya saba.
13 Mtu yeyote agusaye maiti ya mtu yeyote na kushindwa kujitakasa mwenyewe hunajisi Maskani ya Bwana. Mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na Israeli. Kwa sababu hajanyunyiziwa maji ya utakaso, yeye ni najisi; unajisi wake unabaki juu yake.
Yeyote atakayegusa mtu aliyekufa, maiti ya mtu aliyekufa na hajajitakasa - mtu huyu anainajisi masikani ya BWANA. Mtu huyo ataondolewa kuwa miongoni mwa Waisraeli kwa sababu maji ya farakano hayakunyunyiziwa kwake. Atabaki najisi; na unajisi wake utabaki kwake.
14 “Hii ndiyo sheria itumikayo wakati mtu amekufa ndani ya hema: Yeyote aingiaye ndani ya hema hilo na yeyote aliye ndani yake watakuwa najisi kwa muda wa siku saba,
Hii ndiyo sheri ya mtu anayefia hemani. Kila mtu aingiaye hemani na kila mtu ambaye tayari yumo hemani atakuwa najisi kwa siku saba.
15 nacho kila chombo kisicho na kifuniko juu yake kitakuwa najisi.
Kila chombo ambacho hakina kifuniko kinanajisika.
16 “Mtu yeyote aliyeko nje mahali pa wazi agusaye mtu aliyeuawa kwa upanga au mtu aliyekufa kwa kifo cha kawaida, au mtu yeyote agusaye mfupa wa mtu aliyekufa au kaburi, atakuwa najisi kwa siku saba.
Vivyo hivyo, kwa mtu aliye nje ya hema ambaye atamgusa mtu aliyeuawa kwa upanga, au mzoga wowote, au mfupa wa mtu, au kaburi—mtu huyo atakuwa najisi kwa siku saba.
17 “Kwa mtu aliye najisi, weka majivu ya sadaka ya utakaso wa dhambi ndani ya chombo, umimine maji safi juu yao.
Fanyeni hivi kwa mtu najisi: twaeni majivu ya sadaka ya dhaambi ya kuteketezwa na myacahanganye kwenye chombo chenye maji ya mto.
18 Kisha mtu aliye safi kwa kawaida za kiibada atachukua hisopo, achovye ndani ya maji, na kunyunyizia hema na vifaa vyote pamoja na watu ambao walikuwamo. Pia ni lazima amnyunyizie mtu yeyote ambaye amegusa mfupa wa mtu aliyekufa, au kaburi, au mtu ambaye ameuawa, au mtu ambaye amekufa kifo cha kawaida.
Ndipo mtu aliye safi atachukua hisopo, na kutia katika hayo maji, na kunyunyizia juu ya hema, na katika vyombo vyote vilivyo hemani, na kwa watu waliokuwepo, na kwa yule aliyegusa ule mfupa, mtu aliyeuawa, maiti, au kaburi.
19 Mtu ambaye ni safi ndiye atakayemnyunyizia yeyote ambaye ni najisi siku ya tatu na siku ya saba, na katika siku ya saba atamtakasa mtu huyo. Mtu ambaye ametakaswa lazima afue nguo zake na kuoga kwa maji, na jioni ile atakuwa safi.
Katika siku ya tatu na siku ya saba, yule mtu aliye msafi atamnyunyizia yule mtu asiyekuwa safi. Katika siku ya saba mtu najisi atajitakasa mwenyewe. Atazifua nguo zake na kuoga kwenye maji. Jioni yake atakuwa safi.
20 Lakini ikiwa mtu ambaye ni najisi hakujitakasa mwenyewe, ni lazima akatiliwe mbali na jumuiya, kwa sababu ameinajisi Maskani ya Bwana. Maji ya utakaso hayajanyunyizwa juu yake, naye ni najisi.
Lakini yule atakayebaki najisi, anayekataa kujitakasa mwenyewe — huyo mtu ataondolewa kutoka kwenye jamii, kwa sababu amepanajisi patakatifu pa BWANA. Hajanyunyiziwa maji ya utakaso; atabaki najisi.
21 Hii ni sheria ya kudumu kwao. “Mtu yeyote ambaye ananyunyiza yale maji ya utakaso lazima pia afue nguo zake, na yeyote ambaye hugusa maji ya utakaso atakuwa najisi mpaka jioni.
Hii itakuwa sheria ya kudumu kuhusiana na hali ya hivi. Yule mtu anayenyunyizia maji ya farakano atafua mavazi yake. Yule atakayeyagusa maji ya farakano atakuwa najisi mpaka jioni.
22 Kitu chochote anachogusa mtu aliye najisi kitakuwa najisi, na yeyote akigusaye huwa najisi mpaka jioni.”
Chochote kile ambacho kitaguswa na mtu najisi kitakuwa najisi. na mtu atakayekigusa naye atakuwa najisi mpaka jioni.