< Hesabu 17 >
BWANA akanena na Musa, akasema,
2 “Sema na Waisraeli, na ujipatie fimbo kumi na mbili kutoka kwao, moja kutoka kwa kila mmoja wa viongozi wa kabila za baba zao. Andika jina la kila mtu kwenye fimbo yake.
“Waambie wana wa Israeli wakuletee fimbo za kutembelea moja kwa kila jamaa, fimbo kumi na mbili. Uandika jina la kila mmoja kwenye hizo fimbo.
3 Kwenye fimbo ya Lawi andika jina la Aroni, kwa maana ni lazima iwepo fimbo moja kwa kila kiongozi kwa ajili ya kila kabila la baba zao.
Utaandika jina la Haruni kwenye jina la Lawi. Kutakuwa na fimbo moja kwa kila kiongozi kutoka kwenye kabila la mababu zake.
4 Ziweke hizo fimbo ndani ya Hema la Kukutania mbele ya Sanduku la Ushuhuda, mahali nikutanapo nawe.
Utaziweka hizo fimbo kwenye hema ya kukutania mbele ya amri za agano, ambapo Mimi hukutana na wewe. Itakuwa hivi,
5 Fimbo ya mtu nitakayemchagua itachipuka, nami mwenyewe nitayakomesha haya manungʼuniko ya mara kwa mara ya Waisraeli dhidi yako.”
fimbo ya mtu yule ninayemchagua itachipua. Nitazuia watu wa Israeli walalamikao, ambao wanaongea kinyume na wewe.”
6 Hivyo Mose akasema na Waisraeli, nao viongozi wao wakampa fimbo kumi na mbili, fimbo moja kwa ajili ya kila kabila la baba zao, nayo fimbo ya Aroni ikiwa miongoni mwa hizo.
Kwa hiyo Musa akawaambia wana wa Israeli. Viongozi wote wa kabila wakampatia fimbo, fimbo moja kutoka kwa kila kiongozi, aliyechaguliwa kutoka kwenye kila kabila ya babu zao, jumla yake fimbo kumi na mbili. Fimbo ya Haruni ilikuwa miongoni mwa fimbo hizo.
7 Mose akaziweka hizo fimbo mbele za Bwana ndani ya Hema la Ushuhuda.
Ndipo Musa alipoziweka zile fimbo mbele ya BWANA katika hema ya amri ya agano.
8 Siku iliyofuata Mose aliingia kwenye Hema la Ushuhuda akaona ile fimbo ya Aroni ambayo iliwakilisha jamaa ya Lawi haikuwa tu imechipuka, bali pia ilikuwa imetoa machipukizi, kuchanua maua na kuzaa malozi.
Siku iliyofuata Musa aliingia kwenye hema ya amri ya agano, na tazama, fimbo ya Haruni kwa ajili ya Kabila la Lawi ilikuwa imetoa machipukizi. Machipukizi yalikuwa hadi kuchanua maua na kuzaa malozi mabivu!
9 Ndipo Mose akaleta zile fimbo zote kwa Waisraeli wote kutoka mbele za Bwana. Wakaziangalia, na kila mtu akaichukua fimbo yake mwenyewe.
Musa akazitoa fimbo zote kutoka kwa BWANA kwa watu wote wa Israeli, na kila mtu akachukua fimbo yake.
10 Bwana akamwambia Mose, “Rudisha fimbo ya Aroni mbele ya Sanduku la Ushuhuda, ili ihifadhiwe kama alama kwa waasi. Hili litakomesha manungʼuniko yao dhidi yangu, ili kwamba wasife.”
BWANA akamwambua Musa, “Iweke fimbo ya Haruni mbele ya amri za agano. Iweke iwe ishara ya hatia mbele ya watu waliopinga ili ukomeshe malalamiko dhidi yangu, vinginevyo watakufa.”
11 Mose akafanya kama Bwana alivyomwamuru.
Musa akafanya kama BWANA alivyoagiza.
12 Waisraeli wakamwambia Mose, “Tutakufa! Tumepotea, sote tumepotea!
Wana wa Israeli wakanena na Musa wakisema, “tutakufa hapa! Wote tutaangamia!
13 Yeyote akaribiaye Maskani ya Bwana atakufa. Je, sisi sote tutakufa?”
Kila mmoja anayekuja hapa, anayekaribia masikani ya BWANA, atakufa. Je, ni lazima wote tuangamie?”