< Hesabu 14 >

1 Usiku ule watu wote wa jumuiya walipaza sauti zao na kulia kwa sauti kuu.
Usiku huo watu wote walilia kwa sauti.
2 Waisraeli wote wakanungʼunika dhidi ya Mose na Aroni, nalo kusanyiko lote wakawaambia, “Laiti tungekuwa tumefia humo nchi ya Misri! Au humu kwenye hili jangwa!
Watu wote wa Israeli wakamlalamikia Musa na Haruni. Watu wote wakawaambia, “Ni bora kama tungelifia katika nchi ya Misri, au katika hili!
3 Kwa nini Bwana anatuleta katika nchi hii ili tufe kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watachukuliwa kama nyara. Je, isingekuwa bora kwetu kurudi Misri?”
Kwa nini BWANA alituleta katika nchi hii ili tufe kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa watumwa wao. Je, si bora kwetu kurudi Misri?”
4 Wakasemezana wao kwa wao, “Inatupasa kumchagua kiongozi na kurudi Misri.”
Wakasemezana wao kwa wao, “Na tuchague kiongozi mwingine, turudi Misri.”
5 Ndipo Mose na Aroni wakaanguka kifudifudi mbele ya kusanyiko lote la Kiisraeli lililokusanyika hapo.
Ndipo Musa na Haruni wakalala kifudifudi mbele ya kundi lote la wana wa Israeli.
6 Yoshua mwana wa Nuni na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwa watu wale waliokwenda kuipeleleza nchi, wakararua nguo zao,
Joshua mwana wa Nuni na Kalebu mwana wa Yefune, ambao walikuwa miongoni mwa wale waliokuwa waemtumwa kwenda kuipeleleza nchi wakachana mavazi yao.
7 wakasema na kusanyiko lote la Kiisraeli, wakawaambia, “Nchi tuliyopita katikati yake na kuipeleleza ni nzuri sana sana.
Wakawaambia watu wote wa Israeli. Walisema, “Ile nchi tuliyopita katikati yake ni nchi nzuri sana.
8 Ikiwa Bwana anapendezwa nasi, atatuongoza kuingia katika nchi ile, nchi itiririkayo maziwa na asali, naye atatupa nchi hiyo.
Kama BWANA amependezwa nasi, basi atatuingiza katika nchi hii na kutupatia. Ile nchi inatiririka maziwa na asali.
9 Ila tu msimwasi Bwana. Wala msiwaogope watu wa nchi hiyo, kwa sababu tutawameza. Ulinzi wao umeondoka, lakini Bwana yupo pamoja nasi. Msiwaogope.”
Lakini msimwasi BWANA, na msiwahofie hao wakazi wa nchi hiyo. Tutawateketeza kwa urahisi kama kula chakula. Ulinzi wao utaondolewa kutoka kwao, kwa sababu BWANA yuko pamoja nasi. Msiwahofie.”
10 Lakini kusanyiko lote likazungumza juu ya kuwapiga kwa mawe. Ndipo utukufu wa Bwana ukaonekana katika Hema la Kukutania kwa Waisraeli wote.
Lakini watu wote walitishia kuwapiga kwa mawe mpaka wafe. Kisha utukufuwa BWANA ukaonekana kwenye hema ya kukutania kwa watu wote wa Israeli.
11 Bwana akamwambia Mose, “Watu hawa watanidharau mpaka lini? Wataendelea kukataa kuniamini mimi mpaka lini, ingawa nimetenda ishara za miujiza miongoni mwao?
BWANA akamwambi Musa, “watu hawa watanidharau hadi lini? Wataendelea kutoniamini mpaka lini? Nijapokuwa nimefanya ishara kwa nguvu zangu kati yao?
12 Nitawapiga kwa tauni na kuwaangamiza, lakini nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa lenye nguvu kuliko wao.”
Nitawapiga kwa mapigo, na kuwaondolea urithi, na kufanya taifa kubwa kutoka kwenye ukoo wako ambalo litakuwa kubwa na lenye nguvu kuliko wao.
13 Mose akamwambia Bwana, “Ndipo Wamisri watasikia juu ya jambo hili! Kwa uweza wako uliwapandisha watu hawa kutoka miongoni mwao.
Musa akamwambia BWANA, “Kama utafanya hivi, Na Wamisiri wakisikia habari hizi, na kwa sababu uliwaokoa kutoka kwao kwa nguvu zako.
14 Nao watawaambia wenyeji wa nchi hii jambo hili. Wao tayari wameshasikia kwamba wewe, Ee Bwana, upo pamoja na watu hawa, na kuwa wewe, Ee Bwana, umeonekana uso kwa uso, nalo wingu lako hukaa juu yao. Tena wewe unawatangulia kwa nguzo ya wingu mchana na kwa nguzo ya moto usiku.
Basi watawaambia wakazi wa nchi hii. Wamesikia ya kuwa wewe BWANA u kati ya watu hawa, kwa sababu uso wako waonekana. Wingu lako husimama juu ya watu wetu. Wewe huwatangulia katika nguzo ya wingu wakati wa mchana na katika nguzo ya moto wakati wa usiku.
15 Ikiwa utawaua watu hawa wote mara moja, mataifa ambayo yamesikia taarifa hii kukuhusu wewe watasema,
Sasa kama utawaua hawa watu kama mtu mmoja, basi mataifa ambao wamesikia sifa zako watasema,
16 ‘Bwana alishindwa kuwaingiza watu hawa katika nchi aliyowaahidi kwa kiapo; hivyo akawaua jangwani.’
“Kwa Sababu BWANA hana uwezo wa kuwapeleka watu hawa katika nchi ambayo aliwaapia kuwapa, ndiyo maana amewaua katika jangwa hili.'
17 “Basi sasa nguvu za Bwana na zionekane, sawasawa na vile ulivyosema:
Sasa, nakusihi, utumie uweza wako. Kwa kuwa umesema kuwa,
18 ‘Bwana si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo na mwenye kusamehe dhambi na uasi. Lakini haachi kumwadhibu mwenye hatia, huadhibu watoto kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne.’
'BWANA si mwepesi wa hasira na ni mwingi wa uaminifu katika agano. Yeye husamehe uovu na uasi. Kwa vyovyote vile atafutilia hatia atakapoleta hukumu ya dhambi za mababu juu ya wazao wao, kwa kizazi cha tatu na cha nne.'
19 Kwa kadiri ya upendo wako mkuu, usamehe dhambi ya watu hawa, kama vile ulivyowasamehe tangu wakati walitoka Misri mpaka sasa.”
Ninakusihi uwasameha watu hawa dhambi zao kwa sababu ya ukuu wa uaminifu wa agano lako, kama vile ambavyo umekuwa ukiwasamehe watu hawa tokea wakati wakiwa Misri mpaka sasa.”
20 Bwana akajibu, “Nimewasamehe kama ulivyoomba.
BWANA akasema, Nimewasamehe kwa kama ulivyoomba,
21 Hata hivyo, kwa hakika kama niishivyo, na kwa hakika kama utukufu wa Bwana uijazavyo dunia yote,
bali kama Niishivyo, na kama vile dunia yote itakavyojazwa na utukufu wangu,
22 hakuna hata mmoja wa watu hawa ambao waliuona utukufu wangu na ishara za miujiza niliyotenda huko Misri na huko jangwani, lakini ambaye hakunitii na akanijaribu mara hizi kumi,
watu wote walioona utukufu wangu na ishara za nguvu zangu nilizotenda kule Misri na kule jangwani - Lakini bado wamenijaribu mara kumi sasa na hawakuisikiliza sauti yangu.
23 hakuna hata mmoja wao atakayeona nchi niliyowaahidi baba zao kwa kiapo. Hakuna hata mmoja ambaye amenidharau atakayeiona.
Kwa hiyo nasema kwamba hakika hawataiona nchi ile ambayo niliwaahdi kuwapa mababu zao. Hakuna hata mmoja wao ambao wamenidharau watakaoiona,
24 Lakini kwa sababu mtumishi wangu Kalebu ana roho ya tofauti na ananifuata kwa moyo wote, nitamwingiza katika nchi aliyoiendea, nao wazao wake watairithi.
isipokuwa mtumishi wangu Kalebu, kwa sababu alikuwa na roho nyingine. Yeye amenifuata kwa ukamilifu; Yeye nitampeleka katika nchi hiyo ambayo alienda kuipeleleza. Wazao wake wataimilki.
25 Kwa kuwa Waamaleki na Wakanaani wanaishi katika mabonde, kesho geukeni mwelekee jangwani kwa kufuata njia iendayo Bahari ya Shamu.”
(Sasa Waamaleki na Wakanani waliishi katika bonde.) Kesho mtageuka na kwenda katika jangwa kwa njia ya bahari ya Shamu.”
26 Bwana akamwambia Mose na Aroni:
BWANA akanena na Musa na Haruni, akasema,
27 “Jumuiya hii ovu itanungʼunika dhidi yangu hadi lini? Nimesikia malalamiko ya hawa Waisraeli wanaonungʼunika.
“Nitaivumilia jamii ya watu hawa waovu ambao wananinung'unikia mpaka lini? Nimeyasikia malalamiko ya wana wa Israeli dhidi yangu.
28 Hivyo waambie, ‘Hakika kama niishivyo, asema Bwana, nitawafanyia vitu vilevile nilivyosikia mkisema:
Waambie, 'Kama niishivyo,' asema BWANA, 'kama vile mlivyosema katika masikio yake, nitawafanyia jambo hili:
29 Kila mmoja wenu mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi ambaye alihesabiwa na amenungʼunika dhidi yangu, miili yenu itaanguka katika jangwa hili.
Maiti zenu zitaanguka katika jangwa hili, Ninyi nyote mliolalamika dhidi yangu, ninyi mliohesabiwa kwenye ile sensa, idadi yote ya watu kuanzia umri wa mika ishirini na kuendelea.
30 Hakuna hata mmoja wenu atakayeingia katika nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kuwa makao yenu, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.
Kwa hakika hamtaingia kwenye ile nchi ambayo niliahidi kuwapa kuwa makazi yenu, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Joshua mwana wa Nuni.
31 Lakini watoto wenu ambao mlisema watachukuliwa kama mateka, nitawaingiza humo ili waifurahie nchi ambayo ninyi mmeikataa.
Bali watoto wenu ambao mlisema kuwa watakuwa watumwa, wao ndio nitakaowapeleka katika nchi hiyo. Wao wataifurahia nchi ambayo nInyi mmeikataa!
32 Lakini ninyi, miili yenu itaanguka katika jangwa hili.
Lakini ninyi, maiti zenu zitaanguka katika jangwa hili.
33 Watoto wenu watakuwa wachungaji wa mifugo hapa kwa miaka arobaini, wakiteseka kwa ajili ya kukosa uaminifu kwenu, hadi mwili wa mtu wenu wa mwisho ulale katika jangwa hili.
Watoto wenu watakuwa wachungaji katika jangwa hili kwa muda wa miaka arobaini. Lazima watabeba madhara ya matendo yenu ya kutokuamini mpaka mwisho wa maiti ya mwisho jangwani.
34 Kwa miaka arobaini, mwaka mmoja kwa kila siku katika zile siku arobaini mlizoipeleleza nchi, mtateseka kwa ajili ya dhambi zenu, na kujua jinsi ilivyo vibaya kunifanya mimi kuwa adui yenu.’
Kama vile ilivyo hesabu ya siku ambayo mliipeleleza nchi—siku arobaini, vivyo hivyo mtabeba madhara ya dhambi zenu kwa muda wa miaka arobaini—mwaka mmoja kwa kila siku moja, na mtajua kuwa ni sawa na kuwa adui yangu.
35 Mimi Bwana nimesema, na hakika nitafanya mambo haya kwa jumuiya hii yote ovu, ambayo imefungamana pamoja dhidi yangu. Watakutana na mwisho wao katika jangwa hili; hapa ndipo watafia.”
Mimi BWANA nimesema. Hakika nitafanya hivi kwa kizazi hiki chote kiovu ambacho kimekusanyika kinyume na Mimi. Wao watakatwa kabisa, na watafia hapa.'”
36 Hivyo watu wale ambao Mose alikuwa amewatuma kuipeleleza nchi, waliorudi na kuifanya jumuiya nzima kunungʼunika dhidi ya Mose kwa kueneza taarifa mbaya kuhusu hiyo nchi:
Kwa hiyo wale wanaume ambao Musa aliwatuma kwenda kuingalia ile nchi wote walikufa kwa tauni mbele ya BWANA.
37 watu hawa waliohusika kueneza taarifa mbaya kuhusu hiyo nchi walipigwa na kuanguka kwa tauni mbele za Bwana.
Hawa ni wale ambao waliorudi na kutoa taarifa mbaya juu ya nchi. Hii iliwafanya watu wote wamlalamikie Musa.
38 Miongoni mwa watu waliokwenda kuipeleleza hiyo nchi, ni Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune peke yao waliosalia.
Kati ya watu wale waliokuwa wameenda kuiangalia nchi ile, ni Joshua mwana wa Nuni na Kalebu mwana wa Yefune tu ndio waliobaki hai.
39 Mose alipotoa taarifa hii kwa Waisraeli wote, waliomboleza kwa uchungu.
Musa alipowataarifu mambo haya watu wote wa Israeli waliomboleza sana.
40 Mapema asubuhi siku iliyofuata walipanda juu kuelekea kwenye nchi ya vilima virefu, wakasema, “Tumetenda dhambi. Tutakwea mpaka mahali Bwana alipotuahidi.”
Waliamka asubuhi na mapema wakaenda juu ya mlima na kisha wakasema, “Tazama, tuko hapa, na tutaenda mahali pale ambapo BWANA ametuahidi, kwa kuwa tumetenda dhambi.”
41 Lakini Mose akasema, “Kwa nini hamtii amri ya Bwana? Jambo hili halitafanikiwa!
Lakini Musa akasema, “Kwa nini sasa mnapinga amri ya BWANA? hamtafanikiwa.
42 Msipande juu, kwa kuwa Bwana hayupo pamoja nanyi. Mtashindwa na adui zenu,
Msiende, kwa sababu BWANA hayuko pamoja nanyi kuwalinda dhidi ya maadui zenu.
43 kwa kuwa Waamaleki na Wakanaani watapambana nanyi huko. Kwa sababu mmemwacha Bwana, hatakuwa pamoja nanyi, ninyi mtaanguka kwa upanga.”
Waamaleki na Wakanaani wako kule, na mtakufa kwa upanga kwa sababu mliumtegea mgongo BWANA na hamkumfuata. Kwa hiyo hatakuwa pamoja nanyi.
44 Hata hivyo, kwa kiburi chao walipanda juu kuelekea nchi ya vilima virefu, ijapokuwa Mose hakutoka kambini wala Sanduku la Agano la Bwana.
Lakini walithubutu kukwea mlimani; lakini si Musa wala Sanduku la agano la BWANA walioondoka kambini.
45 Ndipo Waamaleki na Wakanaani walioishi katika hiyo nchi ya vilima wakateremka na kuwashambulia, wakawapiga njia yote hadi Horma.
Kisha Waamaleki walikuja chini, pia wale Wakanaani walioshi kwenye hiyo milima. Wakawavamia Waisreli wakawapiga na kuwaangusha mpaka Horima.

< Hesabu 14 >