< Hesabu 13 >

1 Bwana akamwambia Mose,
Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia, “tuma watu waende kuipeleleza nchi ya Kanani, ambayo nimewapa wana wa Israeli.
2 “Watume baadhi ya watu wakaipeleleze nchi ya Kanaani, ambayo ninawapa Waisraeli. Kutoka kwa kila kabila la baba zao, tuma mmoja wa viongozi wao.”
Tuma mwanamume mmoja kutoka kila jamaa ya kabila. Kila mwanamume awe kiongozi katika kabila lake.”
3 Hivyo kwa agizo la Bwana Mose akawatuma kutoka Jangwa la Parani. Wote walikuwa viongozi wa Waisraeli.
Musa akawatuma kutoka jangwa la Parani, ili watii amri ya BWANA. Watu wote hao walikuwa viongozi wa watu wa Israeli.
4 Haya ndiyo majina yao: kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri;
Majina yao yalikuwa haya yafuatayo: kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri;
5 kutoka kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori;
Kutoka kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori;
6 kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune;
Kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune;
7 kutoka kabila la Isakari, Igali mwana wa Yosefu;
Kutoka kabila la Isakari, Igali mwana wa Yusufu,
8 kutoka kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni;
Kutoka kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni;
9 kutoka kabila la Benyamini, Palti mwana wa Rafu;
Kutoka kabila la Benjamini, Paliti mwana wa Rafu;
10 kutoka kabila la Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi,
kutoka kabila ya Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi;
11 kutoka kabila la Manase (kabila la Yosefu), Gadi mwana wa Susi;
kutoka kabila la Yusufu (hiyo inamaanisha kutoka kabila la Manase), Gadi mwana wa Susi;
12 kutoka kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemali;
kutoka kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemalili;
13 kutoka kabila la Asheri, Sethuri mwana wa Mikaeli;
kutoka kabila Asheri, Setu mwana wa Mikaili;
14 kutoka kabila la Naftali, Nabi mwana wa Wofsi;
kutoka kabila la Naftali, Nabi mwana wa Vofisi;
15 kutoka kabila la Gadi, Geueli mwana wa Maki.
kutoka kabila la Gadi, Geuli mwana wa Machi.
16 Haya ndiyo majina ya watu ambao Mose aliwatuma kuipeleleza nchi. (Mose akampa Hoshea mwana wa Nuni jina Yoshua.)
Haya ndiyo majina ya wanaume ambao Musa aliwatuma kwenda kuipelelza ile nchi. Musa akamwita Hoshea mwana wa Nuni kwa jina la Joshua.
17 Mose alipowatuma wakaipeleleze Kanaani, alisema, “Pandeni kupitia Negebu, mwende mpaka nchi ya vilima.
Musa akawatuma kwenda kuipeleleza ile nchi ya Kanani. Naye akawaambia, “Mkaanzie Negebu hadi mahali pa milima.
18 Mwone nchi ni ya namna gani, na kama watu waishio humo wana nguvu au ni wadhaifu, iwapo ni wachache au wengi.
Kaipelelezeni nchi kujua ni nchi ya namna gani. Wachunguzeni watu wake, kama ni watu wenye nguvu au dhaifu, kama ni wachache au ni wengi.
19 Wanaishi katika nchi ya namna gani? Je, ni nzuri au mbaya? Wanaishi katika miji ya namna gani? Je, haina kuta au ngome?
Chunguzeni nchi hiyo wanayoishi ni nchi ya namna gani. Ni nzuri au mbaya? Miji yao ikoje? Je iko kama kambi au ni miji yenye ngome?
20 Ardhi iko aje? Ina rutuba au la? Je, kuna miti ndani yake au la? Jitahidini kadiri mwezavyo kuleta baadhi ya matunda ya nchi.” (Ulikuwa msimu wa kuiva zabibu za kwanza.)
Chunguzeni ni nchi ya namna gani, kama ni njema kwa mazao au la kama kuna miti au hapana. Mwe hodari mkalete sampuli za mazao ya nchi,” Sasa ni muda wa msimu wa malimbuko ya mizabibu.
21 Hivyo wakapanda na kuipeleleza nchi kutoka Jangwa la Sini hadi Rehobu, kuelekea Lebo-Hamathi.
Kwa hiyo wale wanaume wakaenda kuipeleleza ile nchi kutoka jangwa la Sini mpaka Rehobi, karibu na Lebo Hamati.
22 Wakapanda kupitia Negebu hadi wakafika Hebroni, mahali ambapo Ahimani, Sheshai na Talmai, wazao wa Anaki, waliishi. (Hebroni ulikuwa umejengwa miaka saba kabla ya mji wa Soani ulioko Misri.)
Walienda kutoka Negebu nao wakafika Hebroni. Ahimani, Sheshai, na Talmai, Uzao wa Anaki nao walikuweko, Sasa Hebroni ilikuwa imejengwa miaka saba iliyokuwa imepita kabla ya Zoani wa Misri.
23 Walipofika katika Bonde la Eshkoli, walivunja tawi lililokuwa na kishada kimoja cha zabibu. Wawili wao wakalichukua lile tawi kwenye mti, pamoja na komamanga na tini.
Nao walipofika katika bonde la Eshikoli, walikata matawi ya mizabibu lenye kishada cha zabibu. Na makundi mawili ya wapelelezi wakakibeba kwenye mti. Pia wakaleta makomamanga na mtini.
24 Eneo lile likaitwa Bonde la Eshkoli kwa sababu ya kile kishada cha zabibu ambacho Waisraeli walikikata huko.
Mahali pale paliitwa Eshikoli, kwa sababu ya kishada cha mizabibu ambacho wana wa Israeli walikata kule.
25 Mwishoni mwa siku arobaini wakarudi kutoka kuipeleleza nchi.
Baada ya siku arobaini, wakarudi kutoka kuipeleleza nchi.
26 Wakarudi kwa Mose, Aroni na jumuiya yote ya Waisraeli huko Kadeshi kwenye Jangwa la Parani. Hapo ndipo walipotoa habari kwao na kwa kusanyiko lote na kuwaonyesha matunda ya hiyo nchi.
Wakaja kwa Musa, Haruni na kwa watu wote wa Israeli katka jangwa la Parani, kule Kadeshi. Wakaleta taarifa kwao na kwa Waisraeli wote, na kuwaonyesha matunda ya nchi ile.
27 Wakampa Mose taarifa hii: “Tuliingia katika nchi uliyotutuma, nayo inatiririka maziwa na asali! Hili hapa tunda lake.
Wakamwambia Musa, “Tulifika katika ile nchi uliyotutuma. Kwa hakika ni nchi ya kutiririka maziwa na asali. Na baadhi ya matunda yake ni haya hapa.
28 Lakini watu wanaoishi huko ni wenye nguvu, na miji yao ina ngome na ni mikubwa sana. Huko tuliona hata wazao wa Anaki.
Hata hivyo, watu wanaoishi huko ni wenye nguvu. Miji yao ni mikubwa tena ina maboma. Pia tuliwaona wana wa Anaki huko.
29 Waamaleki wanaishi Negebu; Wahiti, Wayebusi na Waamori wanaishi katika nchi ya vilima; nao Wakanaani wanaishi karibu na bahari na kando ya Yordani.”
Waamaleki wanaishi Negebu. Wahiti, Wayebusi, na Waamori nao wanaishi katika milima ya hiyo nchi. Wakanaani wanaishi kando ya bahari na mto Yorodani.”
30 Kisha Kalebu akawanyamazisha watu mbele ya Mose na kusema, “Imetupasa kupanda na kuimiliki nchi, kwa maana hakika tunaweza kufanya hivyo.”
Kisha Kalebu akawatuliza watu waliokuwa mbele ya Musa, akasema, “Twendeni tukaiteke nyara hiyo nchi, kwa kuwa tuna uhakika wa kuikamata.”
31 Lakini watu waliokuwa wamepanda pamoja naye wakasema, “Hatuwezi kuwashambulia wale watu; wana nguvu kutuliko sisi.”
Lakini wale watu waliokuwa wameenda naye walisema, “Hatutaweza kuwashinda hao watu kwa kuwa wao ni hodari kuliko sisi.”
32 Wakaeneza taarifa mbaya miongoni mwa Waisraeli kuhusu nchi waliyoipeleleza. Wakasema, “Nchi tuliyoipeleleza hula watu waishio ndani yake. Watu wote tuliowaona huko ni majitu.
Kwa hiyo wakasambaza taarifa za kukatisha tamaa kwa Wana wa Israeli juu ya nchi ile waliyoipeleleza. Walisema, “Ile nchi tuliyoiona ni nchi inayowala watu wake. Watu wote tuliowaona ni watu warefu.
33 Tuliwaona Wanefili huko (wazao wa Anaki wanatokana na Wanefili.) Tulijiona kama panzi machoni petu wenyewe, nao ndivyo walivyotuona.”
Kule tuliiona majitu, wana wa uzao wa Anaki, ambao nii uzao wa majitu. Sisi tulionekana kama panzi machoni mwao tulipojilingsnisha nao, hivyo ndivyo tulivyoonekana machoni mwao pia.”

< Hesabu 13 >