< Hesabu 13 >

1 Bwana akamwambia Mose,
And there the Lord spoke to Moses, saying:
2 “Watume baadhi ya watu wakaipeleleze nchi ya Kanaani, ambayo ninawapa Waisraeli. Kutoka kwa kila kabila la baba zao, tuma mmoja wa viongozi wao.”
Send men to view the land of Chanaan, which I will give to the children of Israel, one of every tribe, of the rulers.
3 Hivyo kwa agizo la Bwana Mose akawatuma kutoka Jangwa la Parani. Wote walikuwa viongozi wa Waisraeli.
Moses did what the Lord had commanded, sending from the desert of Pharan, principal men, whose names are these:
4 Haya ndiyo majina yao: kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri;
Of the tribe of Ruben, Sammua the son of Zechur.
5 kutoka kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori;
Of the tribe of Simeon, Saphat the son of Hurl.
6 kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune;
Of the tribe of Juda, Caleb the son of Jephone.
7 kutoka kabila la Isakari, Igali mwana wa Yosefu;
Of the tribe of Issachar, Igal the son of Joseph.
8 kutoka kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni;
Of the tribe of Ephraim, Osee the son of Nun.
9 kutoka kabila la Benyamini, Palti mwana wa Rafu;
Of the tribe of Benjamin, Phalti the son of Raphu.
10 kutoka kabila la Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi,
Of the tribe of Zabulon, Geddiel the son of Sodi.
11 kutoka kabila la Manase (kabila la Yosefu), Gadi mwana wa Susi;
Of the tribe of Joseph, of the sceptre of Manasses, Gaddi the son of Susi.
12 kutoka kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemali;
Of the tribe of Dan, Ammiel the son of Gemalli.
13 kutoka kabila la Asheri, Sethuri mwana wa Mikaeli;
Of the tribe of Aser, Sthur the son of Michael.
14 kutoka kabila la Naftali, Nabi mwana wa Wofsi;
Of the tribe of Nephtali, Nahabi the son of Vapsi.
15 kutoka kabila la Gadi, Geueli mwana wa Maki.
Of the tribe of Gad, Guel the son of Machi.
16 Haya ndiyo majina ya watu ambao Mose aliwatuma kuipeleleza nchi. (Mose akampa Hoshea mwana wa Nuni jina Yoshua.)
These are the names of the men, whom Moses sent to view the land: and he called Osee the son of Nun, Josue.
17 Mose alipowatuma wakaipeleleze Kanaani, alisema, “Pandeni kupitia Negebu, mwende mpaka nchi ya vilima.
And Moses sent them to view the land of Chanaan, and said to them: Go you up by the south side. And when you shall come to the mountains,
18 Mwone nchi ni ya namna gani, na kama watu waishio humo wana nguvu au ni wadhaifu, iwapo ni wachache au wengi.
View the land, of what sort it is: and the people that are the inhabitants thereof, whether they be strong or weak: few in number or many:
19 Wanaishi katika nchi ya namna gani? Je, ni nzuri au mbaya? Wanaishi katika miji ya namna gani? Je, haina kuta au ngome?
The land itself, whether it be good or bad: what manner of cities, walled or without walls:
20 Ardhi iko aje? Ina rutuba au la? Je, kuna miti ndani yake au la? Jitahidini kadiri mwezavyo kuleta baadhi ya matunda ya nchi.” (Ulikuwa msimu wa kuiva zabibu za kwanza.)
The ground, fat or barren, woody or without trees. Be of good courage, and bring us of the fruits of the land. Now it was the time when the first ripe grapes are fit to be eaten.
21 Hivyo wakapanda na kuipeleleza nchi kutoka Jangwa la Sini hadi Rehobu, kuelekea Lebo-Hamathi.
And when they were gone up, they viewed the land from the desert of Sin, unto Rohob as you enter into Emath.
22 Wakapanda kupitia Negebu hadi wakafika Hebroni, mahali ambapo Ahimani, Sheshai na Talmai, wazao wa Anaki, waliishi. (Hebroni ulikuwa umejengwa miaka saba kabla ya mji wa Soani ulioko Misri.)
And they went up at the south side, and came to Hebron, where were Achiman and Sisai and Tholmai the sons of Enac. For Hebron was built seven years before Tanis the city of Egypt.
23 Walipofika katika Bonde la Eshkoli, walivunja tawi lililokuwa na kishada kimoja cha zabibu. Wawili wao wakalichukua lile tawi kwenye mti, pamoja na komamanga na tini.
And going forward as far as the torrent of the cluster of grapes, they cut off a branch with its cluster of grapes, which two men carried upon a lever. They took also of the pomegranates and of the figs of that place:
24 Eneo lile likaitwa Bonde la Eshkoli kwa sababu ya kile kishada cha zabibu ambacho Waisraeli walikikata huko.
Which was called Nehelescol, that is to say, the torrent of the cluster of grapes, because from thence the children of Israel had carried a cluster of grapes.
25 Mwishoni mwa siku arobaini wakarudi kutoka kuipeleleza nchi.
And they that went to spy out the land returned after forty days, having gone round all the country,
26 Wakarudi kwa Mose, Aroni na jumuiya yote ya Waisraeli huko Kadeshi kwenye Jangwa la Parani. Hapo ndipo walipotoa habari kwao na kwa kusanyiko lote na kuwaonyesha matunda ya hiyo nchi.
And came to Moses and Aaron and to all the assembly of the children of Israel to the desert of Pharan, which is in Cades. And speaking to them and to all the multitude, they shewed them the fruits of the land:
27 Wakampa Mose taarifa hii: “Tuliingia katika nchi uliyotutuma, nayo inatiririka maziwa na asali! Hili hapa tunda lake.
And they related and said: We came into the land to which thou sentest us, which in very deed floweth with milk and honey as may be known by these fruits:
28 Lakini watu wanaoishi huko ni wenye nguvu, na miji yao ina ngome na ni mikubwa sana. Huko tuliona hata wazao wa Anaki.
But it hath very strong inhabitants, and the cities are great and walled. We saw there the race of Enac.
29 Waamaleki wanaishi Negebu; Wahiti, Wayebusi na Waamori wanaishi katika nchi ya vilima; nao Wakanaani wanaishi karibu na bahari na kando ya Yordani.”
Amalec dwelleth in the south, the Hethite and the Jebusite and the Amorrhite in the mountains: but the Chanaanite abideth by the sea and near the streams of the Jordan.
30 Kisha Kalebu akawanyamazisha watu mbele ya Mose na kusema, “Imetupasa kupanda na kuimiliki nchi, kwa maana hakika tunaweza kufanya hivyo.”
In the mean time Caleb, to still the murmuring of the people that rose against Moses, said: Let us go up and possess the land, for we shall be able to conquer it.
31 Lakini watu waliokuwa wamepanda pamoja naye wakasema, “Hatuwezi kuwashambulia wale watu; wana nguvu kutuliko sisi.”
But the others, that had been with him, said: No, we are not able to go up to this people, because they are stronger than we.
32 Wakaeneza taarifa mbaya miongoni mwa Waisraeli kuhusu nchi waliyoipeleleza. Wakasema, “Nchi tuliyoipeleleza hula watu waishio ndani yake. Watu wote tuliowaona huko ni majitu.
And they spoke ill of the land, which they had viewed, before the children of Israel, saying: The land which we have viewed, devoureth its inhabitants: the people, that we beheld, are of a tall stature.
33 Tuliwaona Wanefili huko (wazao wa Anaki wanatokana na Wanefili.) Tulijiona kama panzi machoni petu wenyewe, nao ndivyo walivyotuona.”
There we saw certain monsters of the sons of Enac, of the giant kind: in comparison of whom, we seemed like locusts.

< Hesabu 13 >