< Hesabu 10 >

1 Bwana akamwambia Mose:
The LORD spoke to Moses, saying,
2 “Tengeneza tarumbeta mbili za fedha ya kufua, uzitumie kwa kuita jumuiya pamoja na wakati wa kuvunja makambi ili kuondoka.
“Make two trumpets of silver. You shall make them of beaten work. You shall use them for the calling of the congregation and for the journeying of the camps.
3 Tarumbeta zote mbili zikipigwa, jumuiya yote itakusanyika mbele yako katika ingilio la Hema la Kukutania.
When they blow them, all the congregation shall gather themselves to you at the door of the Tent of Meeting.
4 Kama tarumbeta moja tu ikipigwa, viongozi, yaani wakuu wa koo za Israeli, ndio watakaokusanyika mbele yako.
If they blow just one, then the princes, the heads of the thousands of Israel, shall gather themselves to you.
5 Wakati mlio wa kujulisha hatari ukipigwa, makabila yaliyo na makambi upande wa mashariki yataondoka.
When you blow an alarm, the camps that lie on the east side shall go forward.
6 Ukisikika mlio wa pili wa jinsi hiyo, walioko kwenye makambi ya kusini wataondoka. Mlio huo wa kujulisha hatari utakuwa ishara ya kuondoka.
When you blow an alarm the second time, the camps that lie on the south side shall go forward. They shall blow an alarm for their journeys.
7 Ili kukusanya kusanyiko, piga tarumbeta zote, lakini siyo kwa mlio wa kujulisha hatari.
But when the assembly is to be gathered together, you shall blow, but you shall not sound an alarm.
8 “Wana wa Aroni, makuhani, ndio watakaopiga hizo tarumbeta. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yenu na kwa vizazi vijavyo.
“The sons of Aaron, the priests, shall blow the trumpets. This shall be to you for a statute forever throughout your generations.
9 Wakati mtakapopigana vita katika nchi yenu wenyewe dhidi ya adui anayewaonea, piga tarumbeta kwa mlio wa kujulisha hatari. Ndipo utakumbukwa na Bwana Mungu wenu na kuokolewa kutoka kwa adui zenu.
When you go to war in your land against the adversary who oppresses you, then you shall sound an alarm with the trumpets. Then you will be remembered before the LORD your God, and you will be saved from your enemies.
10 Pia nyakati za furaha yenu, yaani sikukuu zenu zilizoamriwa na sikukuu za Mwezi Mwandamo, mtapiga tarumbeta juu ya sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za amani, nazo zitakuwa ukumbusho kwa ajili yenu mbele za Mungu wenu. Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.”
“Also in the day of your gladness, and in your set feasts, and in the beginnings of your months, you shall blow the trumpets over your burnt offerings, and over the sacrifices of your peace offerings; and they shall be to you for a memorial before your God. I am the LORD your God.”
11 Katika siku ya ishirini ya mwezi wa pili wa mwaka wa pili, wingu liliinuka kutoka juu ya maskani ya Ushuhuda.
In the second year, in the second month, on the twentieth day of the month, the cloud was taken up from over the tabernacle of the covenant.
12 Ndipo Waisraeli wakaondoka kutoka Jangwa la Sinai wakasafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine mpaka wingu lilipotua katika Jangwa la Parani.
The children of Israel went forward on their journeys out of the wilderness of Sinai; and the cloud stayed in the wilderness of Paran.
13 Waliondoka kwa mara ya kwanza kwa agizo la Bwana kupitia kwa Mose.
They first went forward according to the commandment of the LORD by Moses.
14 Vikosi vya kambi ya Yuda vilitangulia kwanza chini ya alama yao. Nashoni mwana wa Aminadabu alikuwa kiongozi wao.
First, the standard of the camp of the children of Judah went forward according to their armies. Nahshon the son of Amminadab was over his army.
15 Nethaneli mwana wa Suari alikuwa kiongozi wa kabila la Isakari,
Nethanel the son of Zuar was over the army of the tribe of the children of Issachar.
16 naye Eliabu mwana wa Heloni alikuwa kiongozi wa kabila la Zabuloni.
Eliab the son of Helon was over the army of the tribe of the children of Zebulun.
17 Ndipo Maskani iliposhushwa, nao wana wa Gershoni na wana wa Merari ambao waliibeba wakaondoka.
The tabernacle was taken down; and the sons of Gershon and the sons of Merari, who bore the tabernacle, went forward.
18 Vikosi vya kambi ya Reubeni vilifuata, chini ya alama yao. Elisuri mwana wa Shedeuri alikuwa kiongozi wao.
The standard of the camp of Reuben went forward according to their armies. Elizur the son of Shedeur was over his army.
19 Shelumieli mwana wa Surishadai aliongoza kikosi cha kabila la Simeoni,
Shelumiel the son of Zurishaddai was over the army of the tribe of the children of Simeon.
20 naye Eliasafu mwana wa Deueli aliongoza kikosi cha kabila la Gadi.
Eliasaph the son of Deuel was over the army of the tribe of the children of Gad.
21 Kisha Wakohathi wakaondoka, wakichukua vitu vitakatifu. Maskani ilikuwa isimamishwe kabla wao hawajafika.
The Kohathites set forward, bearing the sanctuary. The others set up the tabernacle before they arrived.
22 Vikosi vya kambi ya Efraimu vilifuata, chini ya alama yao. Elishama mwana wa Amihudi alikuwa kiongozi wao.
The standard of the camp of the children of Ephraim set forward according to their armies. Elishama the son of Ammihud was over his army.
23 Gamalieli mwana wa Pedasuri aliongoza kikosi cha kabila la Manase,
Gamaliel the son of Pedahzur was over the army of the tribe of the children of Manasseh.
24 naye Abidani mwana wa Gideoni alikuwa kiongozi wa kikosi cha kabila la Benyamini.
Abidan the son of Gideoni was over the army of the tribe of the children of Benjamin.
25 Mwishowe, kama kikosi cha nyuma cha ulinzi wa vikosi vyote, vikosi vya kambi ya Dani viliondoka chini ya alama yao. Ahiezeri mwana wa Amishadai alikuwa kiongozi wao.
The standard of the camp of the children of Dan, which was the rear guard of all the camps, set forward according to their armies. Ahiezer the son of Ammishaddai was over his army.
26 Pagieli mwana wa Okrani aliongoza kikosi cha kabila la Asheri,
Pagiel the son of Ochran was over the army of the tribe of the children of Asher.
27 naye Ahira mwana wa Enani aliongoza kikosi cha kabila la Naftali.
Ahira the son of Enan was over the army of the tribe of the children of Naphtali.
28 Huu ndio ulikuwa utaratibu wa kuondoka wa vikosi vya Waisraeli walipokuwa wanaondoka.
Thus were the travels of the children of Israel according to their armies; and they went forward.
29 Basi Mose akamwambia Hobabu mwana wa Reueli, Mmidiani, mkwewe Mose, “Tunaondoka kwenda mahali ambapo Bwana amesema ‘Nitawapa ninyi mahali hapo.’ Twende pamoja nasi tutakutendea mema, kwa maana Bwana ameahidi mambo mema kwa Israeli.”
Moses said to Hobab, the son of Reuel the Midianite, Moses’ father-in-law, “We are journeying to the place of which the LORD said, ‘I will give it to you.’ Come with us, and we will treat you well; for the LORD has spoken good concerning Israel.”
30 Akajibu, “Hapana, sitakwenda; nitarudi kwenye nchi yangu mwenyewe na watu wangu mwenyewe.”
He said to him, “I will not go; but I will depart to my own land, and to my relatives.”
31 Lakini Mose akasema, “Tafadhali usituache. Wewe unajua mahali ambapo yatupasa kupiga kambi jangwani, nawe unaweza kuwa macho yetu.
Moses said, “Do not leave us, please; because you know how we are to encamp in the wilderness, and you can be our eyes.
32 Ikiwa utafuatana nasi, tutashirikiana nawe mema yoyote tutakayopewa na Bwana.”
It shall be, if you go with us—yes, it shall be—that whatever good the LORD does to us, we will do the same to you.”
33 Hivyo waliondoka kutoka mlima wa Bwana, nao wakasafiri kwa siku tatu. Sanduku la Agano la Bwana liliwatangulia kwa zile siku tatu ili kuwatafutia mahali pa kupumzika.
They set forward from the Mount of the LORD three days’ journey. The ark of the LORD’s covenant went before them three days’ journey, to seek out a resting place for them.
34 Wingu la Bwana lilikuwa juu yao wakati wa mchana walipoondoka kambini.
The cloud of the LORD was over them by day, when they set forward from the camp.
35 Wakati wowote Sanduku lilipoondoka, Mose alisema, “Ee Bwana, inuka! Watesi wako na watawanyike; adui zako na wakimbie mbele zako.”
When the ark went forward, Moses said, “Rise up, LORD, and let your enemies be scattered! Let those who hate you flee before you!”
36 Wakati wowote Sanduku liliposimama, alisema, “Ee Bwana, rudi, kwa maelfu ya Waisraeli wasiohesabika.”
When it rested, he said, “Return, LORD, to the ten thousands of the thousands of Israel.”

< Hesabu 10 >