< Nehemia 7 >
1 Baada ya ukuta kukamilika kujengwa upya na nikaweka milango, mabawabu wa lango, waimbaji, na Walawi waliteuliwa.
2 Nikamweka Hanani ndugu yangu kuwa kiongozi wa Yerusalemu, pamoja na Hanania jemadari wa ngome, kwa kuwa alikuwa mtu mwadilifu na mwenye kumcha Mungu kuliko watu wengine.
3 Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe mpaka jua litakapokuwa limepanda. Walinzi wa malango wakiwa bado kwenye zamu, waamuru wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake, na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.”
4 Mji ulikuwa mkubwa, tena wenye nafasi nyingi, lakini walikuwepo watu wachache ndani yake, nazo nyumba zilikuwa bado ni magofu.
5 Hivyo Mungu wangu akaweka moyoni mwangu kuwakusanya wakuu, maafisa na watu wa kawaida kwa ajili ya kuorodheshwa kulingana na jamaa zao. Nilikuta orodha ya vizazi ya wale waliokuwa wa kwanza kurudi toka utumwani. Haya ndiyo niliyokuta yameandikwa humo:
6 Hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake,
7 wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Azaria, Raamia, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispereti, Bigwai, Nehumu na Baana): Orodha ya wanaume wa Israeli ilikuwa:
8 wazao wa Paroshi 2,172
9 wazao wa Shefatia 372
10 wazao wa Ara 652
11 wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) 2,818
12 wazao wa Elamu 1,254
13 wazao wa Zatu 845
14 wazao wa Zakai 760
15 wazao wa Binui 648
16 wazao wa Bebai 628
17 wazao wa Azgadi 2,322
18 wazao wa Adonikamu 667
19 wazao wa Bigwai 2,067
20 wazao wa Adini 655
21 wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) 98
22 wazao wa Hashumu 328
23 wazao wa Besai 324
24 wazao wa Harifu 112
25 wazao wa Gibeoni 95
26 watu wa Bethlehemu na Netofa 188
27 watu wa Anathothi 128
28 watu wa Beth-Azmawethi 42
29 watu wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi 743
30 watu wa Rama na Geba 621
31 watu wa Mikmashi 122
32 watu wa Betheli na Ai 123
33 watu wa Nebo 52
34 wazao wa Elamu 1,254
35 wazao wa Harimu 320
36 wazao wa Yeriko 345
37 wazao wa Lodi, Hadidi na Ono 721
38 wazao wa Senaa 3,930
39 Makuhani: wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) 973
40 wazao wa Imeri 1,052
41 wazao wa Pashuri 1,247
42 wazao wa Harimu 1,017
43 Walawi: wazao wa Yeshua (kupitia Kadmieli kupitia jamaa ya Hodavia) 74
44 Waimbaji: wazao wa Asafu 148
45 Mabawabu wa malango: wazao wa Shalumu, Ateri, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai 138
46 Watumishi wa Hekalu: wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,
47 wazao wa Kerosi, Sia, Padoni,
48 wazao wa Lebana, Hagaba, Shalmai,
49 wazao wa Hanani, Gideli, Gahari,
50 wazao wa Reaya, Resini, Nekoda,
51 wazao wa Gazamu, Uza, Pasea,
52 wazao wa Besai, Meunimu, Nefusimu,
53 wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,
54 wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,
55 wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,
56 wazao wa Nesia na Hatifa.
57 Wazao wa watumishi wa Solomoni: wazao wa Sotai, Soferethi, Perida,
58 wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,
59 wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Amoni.
60 Watumishi wa Hekalu wote na wazao wa watumishi wa Solomoni 392
61 Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:
62 wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda 642
63 Na kutoka miongoni mwa makuhani: wazao wa Hobaya, Hakosi na Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).
64 Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani, kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi.
65 Kwa hiyo, mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.
66 Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360;
67 tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 245.
68 Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245
69 ngamia 435 na punda 6,720.
70 Baadhi ya viongozi wa jamaa walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala alikabidhi kwenye hazina darkoni 1,000 za dhahabu, mabakuli 50, na mavazi 530 kwa ajili ya makuhani.
71 Baadhi ya viongozi wa jamaa walikabidhi kwenye hazina darkoni 20,000 za dhahabu, na mane 2,200 za fedha kwa ajili ya kazi hiyo.
72 Jumla ya matoleo ya watu wengine yalikuwa ni darkoni 20,000 za dhahabu, mane 2,000 za fedha, na mavazi sitini na saba ya makuhani.
73 Makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji na watumishi wa Hekalu, pamoja na baadhi ya watu wengine na Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao wenyewe. Ilipotimia miezi saba, nao Waisraeli wakiwa tayari wanaishi katika miji yao,