< Nehemia 11 >

1 Basi viongozi wa watu walikaa Yerusalemu, nao watu wale wengine walipiga kura ili kuleta mtu mmoja kati ya watu kumi aje kuishi Yerusalemu, mji mtakatifu, nao wengine tisa waliobaki wakae katika miji yao wenyewe.
Viongozi wa watu waliishi Yerusalemu, na watu wengine walipiga kura ili kuleta mmoja kati ya watu kumi kuishi Yerusalemu, mji mtakatifu, na wengine tisa walibakia katika miji mingine.
2 Watu waliwasifu wale wote waliojitolea kuishi Yerusalemu.
Na watu wakawabariki wote waliojitoa kwa hiari kuishi Yerusalemu.
3 Hawa ndio viongozi wa majimbo waliokuja kuishi Yerusalemu (baadhi ya Waisraeli, makuhani, Walawi, watumishi wa Hekalu, na wazao wa watumishi wa Solomoni waliendelea kuishi katika miji ya Yuda, kila mmoja katika milki yake mwenyewe katika miji mbalimbali,
Hawa ndio viongozi wa mkoa ambao waliishi Yerusalemu. Hata hivyo, katika miji ya Yuda kila mtu aliishi katika nchi yake mwenyewe, ikiwa ni pamoja na Waisraeli, makuhani, Walawi, watumishi wa hekalu, na wazao wa watumishi wa Sulemani.
4 ambapo watu wengine kutoka Yuda na Benyamini waliishi Yerusalemu). Kutoka wazao wa Yuda: Athaya mwana wa Uzia, mwana wa Zekaria, mwana wa Amaria, mwana wa Shefatia, mwana wa Mahalaleli, mzao wa Peresi.
Katika Yerusalemu waliishi baadhi ya wana wa Yuda na baadhi ya wana wa Benyamini. Watu wa Yuda walikuwa pamoja na Athaya, mwana wa Uzia, mwana wa Zekaria, mwana wa Amaria, mwana wa Shefatia, mwana wa Mahalaleli, mwana wa Peresi.
5 Naye Maaseya mwana wa Baruku, mwana wa Kolhoze, mwana wa Hazaya, mwana wa Adaya, mwana wa Yoyaribu, mwana wa Zekaria, mzao wa Mshiloni.
Na Maaseya, mwana wa Baruki, mwana wa Kolhoze, mwana wa Hazaya, mwana wa Adaya, mwana wa Yoyaribu, mwana wa Zakaria, mwana wa Mshelani, alikuwa mwana wa Baruki.
6 Wazao wa Peresi walioishi Yerusalemu walikuwa 468, watu wenye uwezo.
Wana wote wa Peresi waliokaa Yerusalemu walikuwa 468. Walikuwa masujaa.
7 Kutoka wazao wa Benyamini: Salu mwana wa Meshulamu, mwana wa Yoedi, mwana wa Pedaya, mwana wa Kolaya, mwana wa Maaseya, mwana wa Ithieli, mwana wa Yeshaya
Hao ndio wana wa Benyamini, Salu, mwana wa Meshulamu, mwana wa Yoedi, mwana wa Pedaya, mwana wa Kolaya, mwana wa Maaseva, mwana wa Ithieli, mwana wa Yehaya.
8 na wafuasi wake, Gabai na Salai watu 928.
Na baada yake, Gabai na Salai, watu 928.
9 Yoeli mwana wa Zikri alikuwa afisa wao mkuu, naye Yuda mwana wa Hasenua alikuwa msimamizi juu ya Mtaa wa Pili katika mji.
Yoeli mwana wa Zikri alikuwa mwangalizi wao; na Yuda mwana wa Hasenua alikuwa mkuu wa pili juu ya mji.
10 Kutoka makuhani: Yedaya, mwana wa Yoyaribu, Yakini,
Kutoka kwa makuhani Yedaya, mwana wa Yoyaribu, Yakini,
11 Seraya mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu, msimamizi katika nyumba ya Mungu,
Seraya mwana wa Hilikia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayoti, mwana wa Ahitubu, mkuu wa nyumba ya Mungu,
12 pamoja na wenzao waliofanya kazi hekaluni: watu 822. Adaya mwana wa Yerohamu, mwana wa Pelalia, mwana wa Amsi, mwana wa Zekaria, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya,
na wenzake waliofanya kazi ya ukoo, watu 822. na Adaya mwana wa Yerohamu, mwana wa Pelalia, mwana wa Amzi, ​​mwana wa Zekaria, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya.
13 na wenzao, waliokuwa viongozi wa jamaa: watu 242. Amashisai mwana wa Azareli, mwana wa Azai, mwana wa Meshilemothi, mwana wa Imeri,
Nao walikuwa washirika wake waliokuwa wakuu wa jamaa, wanaume 242, na Maasai mwana wa Azareli, mwana wa Azai, mwana wa Meshilemothi, mwana wa Imeri;
14 na wenzao waliokuwa wenye uwezo: watu 128. Afisa wao mkuu alikuwa Zabdieli mwana wa Hagedolimu.
na ndugu zao, 128 wapiganaji wenye ujasiri, wenye ujasiri; Waziri wao aliyeongoza alikuwa Zabdieli, mwana wa Hageoli.
15 Kutoka Walawi: Shemaya mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, mwana wa Buni;
Na Walawi Shemaya mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, mwana wa Buni,
16 Shabethai na Yozabadi, viongozi wawili wa Walawi, ambao walisimamia kazi za nje za nyumba ya Mungu;
na Shabethai, na Yozabadi, ambao walikuwa ni viongozi wa Walawi, waliosimamia kazi za nje ya nyumba ya Mungu.
17 Matania mwana wa Mika, mwana wa Zabdi, mwana wa Asafu, kiongozi aliyeongoza kutoa shukrani na maombi; Bakbukia aliyekuwa msaidizi wake kati ya wenzake; na Abda mwana wa Shamua, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni.
Alikuwepo Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zakri, mwana wa Asafu, aliyekuwa mkurugenzi aliyeanza shukrani kwa sala, na Bakbukia, wa pili miongoni mwa ndugu zake, na Abda mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni.
18 Jumla ya Walawi waliokaa katika mji mtakatifu walikuwa watu 284.
Katika mji wote mtakatifu walikuwa Walawi 284.
19 Mabawabu: Akubu, Talmoni na wenzao, waliolinda malango: watu 172.
Walinzi wa malango Akubu, Talmoni, na washirika wao, ambao waliolinda milango, wanaume 172.
20 Waisraeli waliosalia, pamoja na makuhani na Walawi, walikuwa katika miji yote ya Yuda, kila mmoja katika urithi wa baba yake.
Na wale waliosalia wa Israeli, na makuhani, na Walawi, walikuwa katika miji yote ya Yuda. Kila mtu aliishi katika milki yake mwenyewe.
21 Watumishi wa Hekalu waliishi katika kilima cha Ofeli. Siha na Gishpa walikuwa wasimamizi wao.
Wafanyakazi wa hekalu waliishi Ofeli, na Siha na Gishpa walikuwa wakiwaongoza.
22 Afisa mkuu wa Walawi huko Yerusalemu alikuwa Uzi mwana wa Bani, mwana wa Hashabia, mwana wa Matania, mwana wa Mika. Uzi alikuwa mmoja wa wazao wa Asafu, waliokuwa waimbaji wenye kuwajibika kwa ajili ya huduma ya nyumba ya Mungu.
Mtawala mkuu juu ya Walawi waliokuwa wakitumikia Yerusalemu alikuwa Uzi mwana wa Bani, mwana wa Hashabia, mwana wa Matania, mwana wa Mika, wa wana wa Asafu, ambao walikuwa waimbaji wa kazi katika nyumba ya Mungu.
23 Waimbaji walikuwa chini ya amri za mfalme, ambazo pia ziliratibu shughuli zao za kila siku.
Walikuwa chini ya maagizo kutoka kwa mfalme na maagizo imara yalitolewa kwa waimbaji kila siku inavyohitajika.
24 Pethahia mwana wa Meshezabeli, mmoja wa wazao wa Zera mwana wa Yuda, alikuwa mwakilishi wa mfalme katika mambo yote kuhusu mahusiano na watu.
Pethahia mwana wa Meshezabeli, mwana wa Zera, mwana wa Yuda, alikuwa upande wa mfalme kwa habari zote za watu.
25 Kuhusu vijiji na mashamba yake, baadhi ya watu wa Yuda waliishi Kiriath-Arba na makazi yaliyokizunguka, katika Diboni na makazi yake, katika Yekabzeeli na vijiji vyake,
Kuhusu vijiji na mashamba yao, baadhi ya watu wa Yuda wakakaa Kiriath-arba, na vijiji vyake, na Diboni, na vijiji vyake, na Yekabzeeli na vijiji vyake.
26 katika Yeshua, katika Molada, katika Beth-Peleti,
Wakaishi katika Yeshua, Molada, Beth-Peleti,
27 katika Hasar-Shuali, katika Beer-Sheba na makazi yake,
Hazar-Shuali, Beersheba na vijiji vyake.
28 katika Siklagi, katika Mekona na makazi yake,
Nao wakakaa Siklagi, na Mekona, na vijiji vyake,
29 katika En-Rimoni, katika Sora, katika Yarmuthi,
Enrimoni, Sora, Yarmuthi,
30 Zanoa, Adulamu na vijiji vyake, katika Lakishi na mashamba yake, na katika Azeka na makazi yake. Hivyo walikuwa wakiishi kuanzia Beer-Sheba mpaka Bonde la Hinomu.
Zanoa, Adulamu, na vijiji vyake, na Lakishi, na mashamba yake, na Azeka, na vijiji vyake. Basi wakakaa kutoka Beer-sheba mpaka bonde la Hinomu.
31 Wazao wa Wabenyamini kutoka Geba waliishi Mikmashi, Aiya, Betheli na makazi yake,
Watu wa Benyamini pia walikuwa wakiishi kutoka Geba, kwenda Mikmashi na Aiya, na Beth-eli na vijiji vyake.
32 katika Anathothi, Nobu na Anania,
Waliishi Anathothi, Nobu, Anania,
33 katika Hazori, Rama na Gitaimu,
Hazori, Rama, Gitaimu,
34 katika Hadidi, Seboimu na Nebalati,
Hadidi, Seboimu, Nebalati,
35 katika Lodi na Ono, na katika Bonde la Mafundi.
Lodi, na Ono, bonde la wafundi.
36 Baadhi ya makundi ya Walawi wa Yuda waliishi huko Benyamini.
Walawi wengine waliishi Yuda wengine Benyamini.

< Nehemia 11 >