< Mika 1 >

1 Neno la Bwana lilimjia Mika, Mmoreshethi, wakati wa utawala wa Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda; ufunuo aliouona kuhusu Samaria na Yerusalemu.
דבר יהוה אשר היה אל מיכה המרשתי בימי יותם אחז יחזקיה מלכי יהודה--אשר חזה על שמרון וירושלם
2 Sikieni, enyi mataifa, enyi nyote, sikilizeni, ee dunia na wote mliomo ndani yake, ili Bwana Mwenyezi ashuhudie dhidi yenu, Bwana kutoka Hekalu lake takatifu.
שמעו עמים כלם הקשיבי ארץ ומלאה ויהי אדני יהוה בכם לעד אדני מהיכל קדשו
3 Tazama! Bwana anakuja kutoka mahali pake; anashuka na kukanyaga mahali palipoinuka juu pa dunia.
כי הנה יהוה יצא ממקומו וירד ודרך על במותי (במתי) ארץ
4 Milima inayeyuka chini yake na mabonde yanagawanyika kama nta mbele ya moto, kama maji yatiririkayo kasi kwenye mteremko.
ונמסו ההרים תחתיו והעמקים יתבקעו כדונג מפני האש כמים מגרים במורד
5 Yote haya ni kwa sababu ya kosa la Yakobo, ni kwa sababu ya dhambi za nyumba ya Israeli. Kosa la Yakobo ni lipi? Je, sio Samaria? Je, mahali pa juu pa Yuda pa kuabudia miungu ni nini? Je, sio Yerusalemu?
בפשע יעקב כל זאת ובחטאות בית ישראל מי פשע יעקב הלוא שמרון ומי במות יהודה הלוא ירושלם
6 “Kwa hiyo nitaufanya Samaria kuwa lundo la kokoto, mahali pa kuotesha mizabibu. Nitayamwaga mawe yake katika bonde na kuacha wazi misingi yake.
ושמתי שמרון לעי השדה למטעי כרם והגרתי לגי אבניה ויסדיה אגלה
7 Sanamu zake zote zitavunjwa vipande vipande; zawadi zake zote za Hekalu zitachomwa kwa moto; nitaharibu vinyago vyake vyote. Kwa kuwa alikusanya zawadi zake kutokana na ujira wa kahaba, nazo zitatumika tena kulipa mishahara ya kahaba.”
וכל פסיליה יכתו וכל אתנניה ישרפו באש וכל עצביה אשים שממה כי מאתנן זונה קבצה ועד אתנן זונה ישובו
8 Kwa ajili ya hili nitalia na kuomboleza; nitatembea bila viatu na tena uchi. Nitabweka kama mbweha na kuomboleza kama bundi.
על זאת אספדה ואילילה אילכה שילל (שולל) וערום אעשה מספד כתנים ואבל כבנות יענה
9 Kwa sababu jeraha lake halitibiki; limekuja Yuda. Limefika hasa kwenye lango la watu wangu, hata Yerusalemu kwenyewe.
כי אנושה מכותיה כי באה עד יהודה--נגע עד שער עמי עד ירושלם
10 Usiliseme hili huko Gathi; usilie hata kidogo. Huko Beth-le-Afra gaagaa mavumbini.
בגת אל תגידו--בכו אל תבכו בבית לעפרה עפר התפלשתי (התפלשי)
11 Piteni mkiwa uchi na wenye aibu, ninyi mkaao Shafiri. Wale waishio Saanani hawatatoka nje. Beth-Eseli iko katika maombolezo; kinga yake imeondolewa kwako.
עברי לכם יושבת שפיר עריה בשת לא יצאה יושבת צאנן--מספד בית האצל יקח מכם עמדתו
12 Wale waishio Marothi wanagaagaa kwa maumivu wakingoja msaada, kwa sababu maangamizi yamekuja kutoka kwa Bwana, hata katika lango la Yerusalemu.
כי חלה לטוב יושבת מרות כי ירד רע מאת יהוה לשער ירושלם
13 Enyi mkaao Lakishi, fungeni farasi kwenye magari ya vita. Mlikuwa chanzo cha dhambi kwa Binti Sayuni, kwa kuwa makosa ya Israeli yalikutwa kwako.
רתם המרכבה לרכש יושבת לכיש ראשית חטאת היא לבת ציון כי בך נמצאו פשעי ישראל
14 Kwa hiyo utaipa Moresheth-Gathi zawadi za kuagana. Mji wa Akzibu utaonyesha wazi udanganyifu kwa wafalme wa Israeli.
לכן תתני שלוחים על מורשת גת בתי אכזיב לאכזב למלכי ישראל
15 Nitawaleteeni atakayewashinda ninyi mnaoishi Maresha. Yeye aliye utukufu wa Israeli atakuja Adulamu.
עד הירש אבי לך יושבת מרשה עד עדלם יבוא כבוד ישראל
16 Nyoeni nywele zenu katika kuomboleza kwa ajili ya watoto wenu mnaowafurahia; jifanyieni upara kama tai, kwa kuwa watawaacha na kwenda uhamishoni.
קרחי וגזי על בני תענוגיך הרחבי קרחתך כנשר כי גלו ממך

< Mika 1 >