< Mika 1 >
1 Neno la Bwana lilimjia Mika, Mmoreshethi, wakati wa utawala wa Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda; ufunuo aliouona kuhusu Samaria na Yerusalemu.
Hili ni neno la Yahwe ambalo lilikuja kwa Mika Mmorashti katika siku za Yotahamu, Ahazi, na Hezekeia, mfalme wa Yuda, lile neno aliloliona kuhusiana na Samaria na Yerusalemu.
2 Sikieni, enyi mataifa, enyi nyote, sikilizeni, ee dunia na wote mliomo ndani yake, ili Bwana Mwenyezi ashuhudie dhidi yenu, Bwana kutoka Hekalu lake takatifu.
Sikilizeni, ninyi watu wote. Sikilizeni, dunia, na vyote vilivyomo kwenye dunia. Acheni Yahwe ashuhudiwe dhidi yenu, Bwana kutoka kwenye hekalu lake takatifu.
3 Tazama! Bwana anakuja kutoka mahali pake; anashuka na kukanyaga mahali palipoinuka juu pa dunia.
Tazama, Yahwe anakuja kutoka mahali pake; atashuka chini na kupakanyaga mahali pa juu katika dunia.
4 Milima inayeyuka chini yake na mabonde yanagawanyika kama nta mbele ya moto, kama maji yatiririkayo kasi kwenye mteremko.
Milima itayeyuka chini yake; mabonde yatapasuka vipande vipande kama mshumaa mbele ya moto, kama maji ambayo yamemwagika chini ya mteremko mkali.
5 Yote haya ni kwa sababu ya kosa la Yakobo, ni kwa sababu ya dhambi za nyumba ya Israeli. Kosa la Yakobo ni lipi? Je, sio Samaria? Je, mahali pa juu pa Yuda pa kuabudia miungu ni nini? Je, sio Yerusalemu?
Haya yote ni kwasababu ya uasi wa Yakobo, na kwasababu ya dhambi za nyumba ya Israeli. Je sababu ilikuwa nini kwa uasi wa Yakobo? Je ilikuwa Samaria? Je sababu ilikuwa nini kwa mahali pa juu pa Yuda? Je haiukuwa Yerusalemu?
6 “Kwa hiyo nitaufanya Samaria kuwa lundo la kokoto, mahali pa kuotesha mizabibu. Nitayamwaga mawe yake katika bonde na kuacha wazi misingi yake.
“Nitaifanya Samaria rundo la uharibifu katika shamba, kama eneo la kupandia mizabibu. Nitayavuta mawe ya jengo lake kwenda kwenye bonde; Nitaifunua misingi yake.
7 Sanamu zake zote zitavunjwa vipande vipande; zawadi zake zote za Hekalu zitachomwa kwa moto; nitaharibu vinyago vyake vyote. Kwa kuwa alikusanya zawadi zake kutokana na ujira wa kahaba, nazo zitatumika tena kulipa mishahara ya kahaba.”
Sanamu zake zote za kuchonga zitapondwa vipande vipande; na zawadi zake zote zitachomwa moto. Kwa kuwa zawadi zake za ukahaba amezikusanya, na kama malipo ya ukahaba yatarudi.”
8 Kwa ajili ya hili nitalia na kuomboleza; nitatembea bila viatu na tena uchi. Nitabweka kama mbweha na kuomboleza kama bundi.
Kwa sababu hii nitalia na kuomboleza; nitaenda peku peku na uchi; Nitaomboleza kama mbeha na kuomboleza kama bundi.
9 Kwa sababu jeraha lake halitibiki; limekuja Yuda. Limefika hasa kwenye lango la watu wangu, hata Yerusalemu kwenyewe.
Kwa kuwa jeraha lake haliponi, kwa kuwa imefika kwa Yuda. Imefikia lango la watu wangu, hadi Yerusalemu.
10 Usiliseme hili huko Gathi; usilie hata kidogo. Huko Beth-le-Afra gaagaa mavumbini.
Msiache kuwambia kuhusu katika Gathi; msilie tena. Katika Bethi Leafra nabiringisha mwenyewe kwenye mavumbi.
11 Piteni mkiwa uchi na wenye aibu, ninyi mkaao Shafiri. Wale waishio Saanani hawatatoka nje. Beth-Eseli iko katika maombolezo; kinga yake imeondolewa kwako.
Piteni karibu na, makao ya Shafiri, katika uchi na aibu. Makazi ya Zaanani hayatatoka nje. Maombolezo ya Beth Ezeli, kwa ajili ya ulinzi yamechukuliwa.
12 Wale waishio Marothi wanagaagaa kwa maumivu wakingoja msaada, kwa sababu maangamizi yamekuja kutoka kwa Bwana, hata katika lango la Yerusalemu.
Kwa kuwa wakaaji wa Marothi hungoja habari njema, kwa sababu hofu, kwa sababu msiba umetoka kwa Yahwe hadi kwenye malango ya Yerusalemu.
13 Enyi mkaao Lakishi, fungeni farasi kwenye magari ya vita. Mlikuwa chanzo cha dhambi kwa Binti Sayuni, kwa kuwa makosa ya Israeli yalikutwa kwako.
Wfuungeni lijamu farasi wakokote gari la farasi, makazi ya Lakishi. Wewe Lakishi, ulikuwa mwanzo wa dhambi kwa binti Sayuni, kwa kuwa makosa ya Israeli yalionekana kwako.
14 Kwa hiyo utaipa Moresheth-Gathi zawadi za kuagana. Mji wa Akzibu utaonyesha wazi udanganyifu kwa wafalme wa Israeli.
Hivyo utaipa zawadi ya kuagia Moreshethi Gathi; mji wa Akzibu utawavunja moyo wafalme wa Israeli.
15 Nitawaleteeni atakayewashinda ninyi mnaoishi Maresha. Yeye aliye utukufu wa Israeli atakuja Adulamu.
Tena nitaleta ushindi kwako, makazi ya Maresha; uzuri wa Israeli utakuja Adulamu.
16 Nyoeni nywele zenu katika kuomboleza kwa ajili ya watoto wenu mnaowafurahia; jifanyieni upara kama tai, kwa kuwa watawaacha na kwenda uhamishoni.
Kata kipara chako na kata nywele zako kwa ajili ya watoto ambao unaowafurahisha. Fanya kipara chako mwenyewe kama tai, kwa ajili ya watoto wako watakao kwenda utumwani kutoka kwako