< Mathayo 26 >

1 Yesu alipomaliza kusema hayo yote, akawaambia wanafunzi wake,
耶稣说完了这一切,就对门徒说:
2 “Kama mnavyojua, baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, naye Mwana wa Adamu atasalitiwa ili asulubiwe.”
“你们知道两天之后就是逾越节,人子将要被交给其他人,钉在十字架上。”
3 Basi viongozi wa makuhani na wazee wa watu wakakusanyika katika jumba la utawala la kuhani mkuu, jina lake Kayafa.
届时,祭司长和民间的长老会聚集在大祭司该亚法的官邸处,
4 Wakafanya shauri ili kumkamata Yesu kwa siri na kumuua.
他们商议如何用虚假的借口逮捕耶稣,把他杀害。
5 Lakini wakasema, “Isiwe wakati wa Sikukuu, kusitokee ghasia miongoni mwa watu.”
不过他们说:“不可在节日下手,免得引起民众暴动。”
6 Yesu alikuwa Bethania nyumbani mwa Simoni aliyekuwa na ukoma,
在伯大尼期间,耶稣住在曾患麻风的西门家里,
7 naye mwanamke mmoja akamjia akiwa na chupa ya marhamu yenye manukato ya thamani kubwa; akayamimina kichwani mwa Yesu alipokuwa ameketi mezani kula chakula.
有一个女人拿着一瓶珍贵的香膏前来,当耶稣坐着时,女人就把他倒在耶稣的头上。
8 Lakini wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Upotevu huu wote ni wa nini?
门徒看见了就很生气,说:“为什么这样浪费呢?
9 Manukato haya yangeuzwa kwa bei kubwa, na fedha hizo wakapewa maskini.”
这香膏可以卖很多钱,接济穷人。”
10 Yesu, akijua jambo hili, akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mwanamke? Yeye amenitendea jambo zuri sana.
耶稣知道了,就说:“何必为难这个女人呢?她为我做了一件美好之事。
11 Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini mimi hamtakuwa nami siku zote.
你们常与穷苦人在一起,但你们不会常与我在一起。
12 Alipomiminia haya manukato kwenye mwili wangu, amefanya hivyo ili kuniandaa kwa ajili ya maziko yangu.
她把这香膏浇在我身上,是为我的葬礼做准备。
13 Amin, nawaambia, mahali popote ulimwenguni ambapo hii Injili itahubiriwa, jambo hili alilolitenda huyu mwanamke litatajwa pia kwa ukumbusho wake.”
我告诉你们实话,这福音无论传到世界何处,这女人的行为都会被传讲,被后人所纪念。”
14 Kisha mmojawapo wa wale kumi na wawili, aitwaye Yuda Iskariote, alikwenda kwa viongozi wa makuhani
这时候,十二门徒中的一人,即加略人犹大,跑去见祭司长,说:
15 na kuuliza, “Mtanipa nini nikimtia Yesu mikononi mwenu?” Wakamlipa vipande thelathini vya fedha.
“如果我把他交给你们,付我多少钱?”他们给了他三十个银币。
16 Tangu wakati huo Yuda akawa anatafuta wakati uliofaa wa kumsaliti Yesu.
从那时候起,他就一直在找机会把耶稣交给他们。
17 Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wanafunzi walimjia Yesu wakamuuliza, “Unataka twende wapi ili tukuandalie mahali pa kula Pasaka?”
除酵节的第一天,门徒前来问耶稣:“我们应该在哪里为你预备逾越节的晚餐,请吩咐。”
18 Akajibu, “Nendeni kwa mtu fulani huko mjini, mkamwambie, ‘Mwalimu asema hivi: Saa yangu imekaribia. Nitaiadhimisha Pasaka pamoja na wanafunzi wangu katika nyumba yako.’”
耶稣说:“你们到城里去见一个人,对他说,老师说:‘我的时候快到了,我将要在你的房子中,和我的门徒守逾越节。’”
19 Hivyo wanafunzi wakafanya kama vile Yesu alivyokuwa amewaelekeza, nao wakaandaa Pasaka.
门徒照耶稣的指示去做,预备好了逾越节的晚餐。
20 Ilipofika jioni, Yesu alikuwa ameketi mezani pamoja na wale wanafunzi wake kumi na wawili.
到了晚上,耶稣和十二门徒一同吃晚餐。
21 Nao walipokuwa wakila, Yesu akasema, “Amin, nawaambia, mmoja wenu atanisaliti.”
用餐的过程中,耶稣说:“我告诉你们实话,你们中有一个人要出卖我。”
22 Wakahuzunika sana, wakaanza kumuuliza mmoja baada ya mwingine, “Je, ni mimi Bwana?”
众人非常沮丧,一个接一个地问他:“主啊,是我吗?”
23 Yesu akawaambia, “Yule aliyechovya mkono wake katika bakuli pamoja nami ndiye atakayenisaliti.
他回答:“那和我一同把手蘸在盘子里的人,就是要出卖我之人。
24 Mwana wa Adamu anaenda zake kama vile alivyoandikiwa. Lakini ole wake mtu yule amsalitiye Mwana wa Adamu. Ingekuwa heri kwake mtu huyo kama hangezaliwa!”
人子将如预言所述死去,他虽然会离世,但出卖人子的叛徒会面临祸端!这人如果没有生下来就好了。”
25 Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, akasema, “Je, ni mimi Rabi?” Yesu akajibu, “Naam, wewe mwenyewe umesema.”
出卖耶稣的犹大说:“拉比,是我吗?”他说:“这是你说的。”
26 Walipokuwa wanakula, Yesu akachukua mkate, akashukuru, akaumega, na kuwapa wanafunzi wake, akisema, “Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu.”
大家开始吃东西了,耶稣拿起饼,祝福后将饼掰开,递给门徒,说:“你们拿去吃吧,这是我的身体。”
27 Kisha akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, “Nyweni nyote katika kikombe hiki.
耶稣又拿起杯子,祝福后递给他们,说:“你们拿去喝吧,
28 Hii ndiyo damu yangu ya Agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.
这是我立约的血,血是为众人而流,让罪过得以救赎。
29 Lakini ninawaambia, tangu sasa sitakunywa tena katika uzao huu wa mzabibu, hadi siku ile nitakapounywa mpya pamoja nanyi katika Ufalme wa Baba yangu.”
我告诉你们,从今以后我不会再喝这葡萄酒,直到我和你们在我父的国度中喝新酒的那一天。”
30 Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda Mlima wa Mizeituni.
随后他们吟唱,然后离开去往橄榄山。
31 Kisha Yesu akawaambia, “Usiku huu, ninyi nyote mtaniacha, kwa maana imeandikwa: “‘Nitampiga mchungaji, nao kondoo wa hilo kundi watatawanyika.’
这时候耶稣对他们说:“今天晚上,你们都会放弃我,因为经文上记着:‘我要击打牧人,羊群就彻底散了。’
32 Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.”
我复活以后,要比你们先到加利利去。”
33 Petro akajibu, “Hata kama wote watakuacha, kamwe mimi sitakuacha.”
彼得对他说:“就算所有人都放弃你,我也绝不会放弃。”
34 Yesu akamjibu, “Amin, nakuambia, usiku huu, kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.”
耶稣对他说:“我告诉你实话,今天晚上鸡叫以前,你会有三次不认我。”
35 Lakini Petro akasisitiza, “Hata kama itabidi kufa pamoja nawe, sitakukana kamwe.” Nao wanafunzi wale wengine wote wakasema vivyo hivyo.
彼得对他说:“就算必须与你一同死,我也决不会不认你。”其他门徒也都这样说。
36 Kisha Yesu akaenda pamoja na wanafunzi wake mpaka kwenye bustani iitwayo Gethsemane, akawaambia, “Kaeni hapa, nami niende kule nikaombe.”
耶稣和门徒来到一个名叫客西马尼的地方。他对门徒说:“你们坐在这里,我要到那边去祷告。”
37 Akamchukua Petro pamoja na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuhuzunika na kufadhaika.
他带了彼得和西庇太的两个儿子一起去,感到痛苦难过。
38 Kisha Yesu akawaambia, “Moyo wangu umejawa na huzuni kiasi cha kufa. Kaeni hapa na mkeshe pamoja nami.”
他对他们说:“我感到非常悲哀,这感觉仿佛要杀了我,你们留在这里,和我一同守候。”
39 Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba akisema, “Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki na kiniondokee. Lakini si kama nipendavyo mimi, bali kama upendavyo wewe.”
他稍往前走几步,把脸俯伏在地上,祷告说:“我的父啊!如果可能,求你让这痛苦离开我,但不要管我的想法,只要照你的旨意。”
40 Kisha akarudi kwa wanafunzi wake, akawakuta wamelala. Akamuuliza Petro, “Je, ninyi hamkuweza kukesha pamoja nami hata kwa saa moja?
耶稣回到门徒那里,看见他们都睡着了,就对彼得说:“你们难道不能保持清醒,等我哪怕一小时吗?
41 Kesheni na mwombe, msije mkaingia majaribuni. Roho iko radhi, lakini mwili ni mdhaifu.”
清醒地进行祷告,以免被诱惑征服。你们心中虽然有意愿,但身体却是软弱的。”
42 Akaenda tena mara ya pili na kuomba, “Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, basi mapenzi yako yafanyike.”
他又再次走开,祷告说:“我父啊!如果这痛苦无法摆脱,一定要我饮下,就愿成全你的旨意。”
43 Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito.
他再回来的时候,看见门徒睡着了,因为他们十分疲倦。
44 Hivyo akawaacha akaenda zake tena mara ya tatu na kuomba akisema maneno yale yale.
他又离开他们,第三次去祷告,说了同样的话。
45 Kisha akarudi kwa wanafunzi wake, akawaambia, “Bado mmelala na kupumzika? Tazameni, saa imefika ambapo Mwana wa Adamu anasalitiwa na kutiwa mikononi mwa wenye dhambi.
然后他回到门徒那里,对他们说:“你们还在睡觉休息吗?看呐,时候到了,人子即将被交给罪人之手。
46 Inukeni, twende zetu! Tazameni, msaliti wangu yuaja!”
起来,我们走吧!出卖我的人来了。”
47 Alipokuwa bado anazungumza, Yuda, mmoja wa wale Kumi na Wawili, akafika. Alikuwa amefuatana na umati mkubwa wa watu wenye panga na marungu, waliokuwa wametumwa na viongozi wa makuhani na wazee wa watu.
耶稣还在说话之时,十二门徒中的犹大,带着一大群手拿刀棒之人赶来,他们都是由祭司长和民间长老派来。
48 Basi msaliti alikuwa amewapa hao watu ishara, kwamba: “Yule nitakayembusu ndiye. Mkamateni.”
叛徒和他们约了一个暗号,说:“我亲吻谁,谁就是耶稣,你们可以抓住他了。”
49 Mara Yuda akamjia Yesu na kumsalimu, “Salamu, Rabi!” Akambusu.
他立刻前来对耶稣说:“拉比,你好。”接着就亲吻他。
50 Yesu akamwambia, “Rafiki, fanya kile ulichokuja kufanya hapa.” Kisha wale watu wakasogea mbele, wakamkamata Yesu.
耶稣对他说:“朋友,你要做的事,就做吧!”于是那些人上前动手拿住耶稣,逮捕了他。
51 Ghafula mmoja wa wale waliokuwa na Yesu alipoona hivyo, akaushika upanga wake, akauchomoa na kumpiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio.
与耶稣同行的一人伸手拔出刀,砍了大祭司仆人一刀,削掉他的一只耳朵。
52 Ndipo Yesu akamwambia, “Rudisha upanga wako mahali pake, kwa maana wote watumiao upanga watakufa kwa upanga.
耶稣对他说:“把你的刀收回原处!凡动刀者必死于刀下。
53 Je, unadhani siwezi kumwomba Baba yangu naye mara moja akaniletea zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?
你知道吗?我可以求我父,他马上就会给我派超过十二个团的天使下来。
54 Lakini je, yale Maandiko yanayotabiri kwamba ni lazima itendeke hivi yatatimiaje?”
但如果这样,经文上预言必然发生之事,就无法应验。”
55 Wakati huo, Yesu akawaambia ule umati wa watu, “Je, mmekuja na panga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyangʼanyi? Siku kwa siku niliketi Hekaluni nikifundisha, mbona hamkunikamata?
这时,耶稣对众人说:“你们带着刀棒赶来,是把我当作危险的罪犯捉拿吗?我天天坐在殿里教导众人,你们却没有逮捕我。
56 Lakini haya yote yametukia ili maandiko ya manabii yapate kutimia.” Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha na kukimbia.
但这整件事却应验了先知书上所述。”之后,门徒都离开他逃跑了。
57 Wale waliokuwa wamemkamata Yesu wakampeleka kwa Kayafa, kuhani mkuu, mahali ambapo walimu wa sheria pamoja na wazee walikuwa wamekusanyika.
那些人逮捕了耶稣,把他押去见大祭司该亚法,宗教老师和长老都已经聚集在那里了。
58 Lakini Petro akamfuata kwa mbali hadi uani kwa kuhani mkuu. Akaingia ndani, akaketi pamoja na walinzi ili aone litakalotukia.
彼得远远跟着耶稣,进入大祭司的官邸,然后和差役坐在一起,想看看事情怎样了结。
59 Viongozi wa makuhani na Baraza la Wayahudi lote wakatafuta ushahidi wa uongo dhidi ya Yesu ili wapate kumuua.
祭司长和全体公议会成员都想找假证供来控告耶稣,想要把他处死。
60 Lakini hawakupata jambo lolote, ingawa mashahidi wengi wa uongo walijitokeza. Hatimaye wakajitokeza mashahidi wawili wa uongo
虽然有许多人前来作假证供,却找不着证据。最后有两个人前来说:
61 na kusema, “Huyu mtu alisema, ‘Ninaweza kulivunja Hekalu la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu.’”
“这人说过:‘我可以拆毁上帝的神庙,三日之内又把它建造起来。’”
62 Kisha kuhani mkuu akasimama na kumwambia Yesu, “Je, wewe hutajibu? Ni ushahidi gani hawa watu wanauleta dhidi yako?”
大祭司便站起来,对耶稣说:“你为什么不回答?这些人的证词,你有什么好辩解的?”
63 Lakini Yesu akakaa kimya. Ndipo kuhani mkuu akamwambia, “Nakuapisha mbele za Mungu aliye hai. Tuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu.”
耶稣沉默。大祭司又对他说:“以永生上帝之名,你要起誓,告诉我们你是不是弥赛亚,上帝的儿子?”
64 Yesu akajibu, “Wewe umenena. Lakini ninawaambia nyote: Siku za baadaye, mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija juu ya mawingu ya mbinguni.”
耶稣回答:“这只是你说的,我要告诉你们,从今以后,你们将看见人子,坐在至高者右边,驾着天上的云降临。”
65 Ndipo kuhani mkuu akararua mavazi yake na kusema, “Amekufuru! Tuna haja gani tena ya mashahidi zaidi? Tazama, sasa ninyi mmesikia hayo makufuru.
大祭司撕开他的衣服,说:“他说了亵渎之语,我们还需要什么证人呢?你们现在听见了这亵渎之言。
66 Uamuzi wenu ni gani?” Wakajibu, “Anastahili kufa.”
你们的裁定是什么?”他们回答:“他有罪,他该死。”
67 Kisha wakamtemea mate usoni na wengine wakampiga ngumi. Wengine wakampiga makofi
于是他们向他的脸上吐唾沫,用拳头打他,也有人用掌掴他,
68 na kusema, “Tutabirie, wewe Kristo! Ni nani aliyekupiga?”
说:“弥赛亚啊,向我们说预言吧!是谁打你呢?”
69 Wakati huu Petro alikuwa amekaa nje uani. Mtumishi mmoja wa kike akamjia na kumwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya.”
彼得坐在外面的院子里,有一个婢女走过来对他说:“你也是和加利利人耶稣一伙的。”
70 Lakini Petro akakana mbele yao wote akisema, “Sijui hilo usemalo.”
彼得却当众否认,说:“我不知道你说什么。”
71 Alipotoka nje kufika kwenye lango, mtumishi mwingine wa kike alimwona, akawaambia watu waliokuwepo, “Huyu mtu alikuwa pamoja na Yesu, Mnazareti.”
他回到庭院的门口,又有一个婢女看见他,对里面的人说:“这人和拿撒勒人耶稣是一伙的。”
72 Akakana tena kwa kiapo akisema, “Mimi simjui huyo!”
彼得再次否认,并且发誓说:“我不认识那个人。”
73 Baada ya muda mfupi, wale waliokuwa wamesimama pale wakamwendea Petro, wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana usemi wako ni kama wao.”
过了一会,站在外面的一人走过来对他说:“你的确是他们中的一员,一听你的口音就认出来了。”
74 Ndipo Petro akaanza kujilaani na kuwaapia, “Mimi simjui mtu huyo!” Papo hapo jogoo akawika.
彼得就发咒起誓说:“我不认识那个人。”此时忽然传来鸡叫。
75 Ndipo Petro akakumbuka lile neno Yesu alilokuwa amesema: “Kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.” Naye akaenda nje, akalia kwa majonzi.
彼得想起耶稣所说的话:“今天晚上鸡叫以前,你会有三次不认我。”于是他就跑出去痛哭。

< Mathayo 26 >