< Mathayo 25 >

1 “Wakati huo, Ufalme wa Mbinguni utakuwa kama wanawali kumi waliochukua taa zao na kwenda kumlaki bwana arusi.
Then the kingdom of heaven will be like ten virgins, who took their lamps, and went out to meet the bridegroom.
2 Watano wao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara.
And five of them were foolish, and five wise.
3 Wale wapumbavu walichukua taa zao lakini hawakuchukua mafuta ya akiba,
For the foolish took their lamps, and took no oil with them.
4 lakini wale wenye busara walichukua taa zao na mafuta ya akiba kwenye vyombo.
But the wise took oil in their vessels with their lamps.
5 Bwana arusi alipokawia kuja wale wanawali wote wakasinzia na kulala.
And as the bridegroom tarried, they all slumbered and slept.
6 “Usiku wa manane pakawa na kelele: ‘Tazameni, huyu hapa bwana arusi! Tokeni nje mkamlaki!’
But at midnight there was a cry, Lo! the bridegroom! go out to meet him.
7 “Ndipo wale wanawali wote wakaamka na kuzitengeneza taa zao.
Then all those virgins arose, and trimmed their lamps.
8 Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara, ‘Tupatieni mafuta yenu kidogo; taa zetu zinazimika.’
And the foolish said to the wise, Give us of your oil, for our lamps are going out.
9 “Lakini wale wenye busara wakawajibu, ‘Sivyo, hayatutoshi sisi na ninyi pia. Afadhali mwende kwa wauzao mkajinunulie mafuta yenu.’
But the wise answered, saying, Perhaps there will not be enough for us and you; go rather to those who sell, and buy for yourselves.
10 “Nao walipokuwa wakienda kununua mafuta, bwana arusi akafika. Wale wanawali waliokuwa tayari wakaingia ndani pamoja naye kwenye karamu ya arusi na mlango ukafungwa.
And while they went to buy, the bridegroom came; and they who were ready went in with him to the wedding; and the door was shut.
11 “Baadaye wale wanawali wengine nao wakaja, wakaita, ‘Bwana! Bwana! Tufungulie mlango!’
Afterward came also the other virgins, saying, Lord, lord, open to us.
12 “Lakini yeye bwana arusi akawajibu, ‘Amin, amin nawaambia, siwajui ninyi!’
But he answering said, Truly do I say to you, I know you not,
13 “Kwa hiyo kesheni, kwa sababu hamjui siku wala saa.
Watch, therefore, for ye know not the day nor the hour.
14 “Tena, Ufalme wa Mbinguni ni kama mtu aliyetaka kusafiri, naye akawaita watumishi wake na kuweka mali yake kwenye uangalizi wao.
For it will be as when a man going abroad called his own servants, and intrusted to them his property;
15 Mmoja akampa talantatano, mwingine talanta mbili, na mwingine talanta moja. Kila mmoja alipewa kwa kadiri ya uwezo wake. Kisha yeye akasafiri.
and to one he gave five talents, to another two, and to another one, to each according to his ability, and went abroad.
16 Yule aliyepewa talanta tano akaenda mara moja akafanya nazo biashara akapata talanta nyingine tano zaidi.
He that had received the five talents went immediately and traded with the same, and gained five talents more.
17 Yule aliyepewa talanta mbili akafanya vivyo hivyo, akapata nyingine mbili zaidi.
In like manner, he that had received the two gained two more.
18 Lakini yule mtumishi aliyekuwa amepokea talanta moja, alikwenda akachimba shimo ardhini na kuificha ile fedha ya bwana wake.
But he that had received the one went and dug in the earth, and hid his lord's money.
19 “Baada ya muda mrefu, yule bwana wa wale watumishi akarudi na kufanya hesabu nao.
And after a long time the lord of those servants cometh, and reckoneth with them.
20 Yule mtumishi aliyepokea talanta tano akaja, akaleta nyingine tano zaidi. Akasema, ‘Bwana uliweka kwenye uangalizi wangu talanta tano. Tazama, nimepata faida ya talanta tano zaidi.’
And he that had received the five talents came and brought five talents more, saying, Lord, thou intrustedst to me five talents; see, I have gained five talents more.
21 “Bwana wake akamwambia, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache; nami nitakuweka kuwa msimamizi wa vitu vingi. Njoo ushiriki katika furaha ya bwana wako!’
His lord said to him, Well done, good and faithful servant! thou hast been faithful over a little, I will place thee in charge of much; enter into the joy of thy lord.
22 “Yule mwenye talanta mbili naye akaja. Akasema, ‘Bwana, uliweka kwenye uangalizi wangu talanta mbili. Tazama nimepata hapa talanta mbili zaidi.’
He also that had received the two talents came and said, Lord, thou intrustedst to me two talents; see, I have gained two talents more.
23 “Bwana wake akajibu, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache; nami nitakuweka kuwa msimamizi wa vitu vingi. Njoo ushiriki katika furaha ya bwana wako!’
His lord said to him, Well done, good and faithful servant! thou hast been faithful over a little, I will place thee in charge of much; enter into the joy of thy lord.
24 “Kisha yule mtumishi aliyepokea talanta moja akaja, akasema, ‘Bwana, nilijua kwamba wewe ni mtu mgumu, unayevuna mahali usipopanda na kukusanya mahali usipotawanya mbegu.
Then he also that had received the one talent came and said, Lord, I knew thee to be a hard man, reaping where thou didst not sow, and gathering where thou didst not scatter seed;
25 Kwa hiyo niliogopa, nikaenda, nikaificha talanta yako ardhini. Tazama, hii hapa ile iliyo mali yako.’
and I was afraid, and went and hid thy talent in the earth. See! thou hast thine own.
26 “Bwana wake akajibu, ‘Wewe mtumishi mwovu na mvivu! Ulijua kwamba ninavuna mahali nisipopanda na kukusanya mahali nisipotawanya mbegu.
But his lord answered and said to him, Wicked and slothful servant! Didst thou know that I reap where I sowed not, and gather where I did not scatter seed?
27 Vyema basi, ingekupasa kuweka fedha yangu kwa watoa riba, ili nirudipo, nichukue ile iliyo yangu na faida yake.
Thou oughtest then to have put my money with the money-dealers, and on my coming I should have received mine own with interest.
28 “‘Basi mnyangʼanyeni hiyo talanta, mkampe yule mwenye talanta kumi.
Take therefore the talent from him, and give it to him who hath the ten talents.
29 Kwa maana kila mtu aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyangʼanywa.
For to every one that hath will be given, and he will have abundance; but from him that hath not, even that which he hath will be taken away.
30 Nanyi mtupeni huyo mtumishi asiyefaa nje, kwenye giza, mahali ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.’
And cast out the unprofitable servant into the outer darkness; there will be wailing and gnashing of teeth.
31 “Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake na malaika wote watakatifu pamoja naye, ndipo atakapoketi juu ya kiti cha enzi cha utukufu wake.
And when the Son of man shall come in his glory, and all the angels with him, then will he sit on the throne of his glory,
32 Mataifa yote watakusanyika mbele zake, naye atawatenga kama mchungaji anavyotenga kondoo na mbuzi.
and before him will be gathered all the nations; and he will separate men one from another, as a shepherd separateth the sheep from the goats;
33 Atawaweka kondoo upande wake wa kuume, na mbuzi upande wake wa kushoto.
and he will set the sheep on his right hand, and the goats on the left.
34 “Ndipo Mfalme atawaambia wale walioko upande wake wa kuume, ‘Njooni, ninyi mliobarikiwa na Baba yangu; urithini Ufalme ulioandaliwa kwa ajili yenu tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
Then will the king say to those on his right hand, Come, ye blessed by my Father, inherit the kingdom prepared for you from the foundation of the world.
35 Kwa maana nilikuwa na njaa mkanipa chakula, nilikuwa na kiu mkaninywesha, nilikuwa mgeni mkanikaribisha,
For I was hungry, and ye gave me food; I was thirsty, and ye gave me drink; I was a stranger, and ye took me in;
36 nilikuwa uchi mkanivika, nilikuwa mgonjwa mkanitunza, nami nilikuwa kifungoni mkaja kunitembelea.’
naked, and ye clothed me; I was sick, and ye visited me; I was in prison, and ye came to me.
37 “Ndipo wale wenye haki watakapomjibu, ‘Bwana, ni lini tulikuona ukiwa na njaa tukakulisha, au ukiwa na kiu tukakunywesha?
Then will the righteous answer him, saying, Lord, when saw we thee hungry, and fed thee? or thirsty, and gave thee drink?
38 Lini tulikuona ukiwa mgeni tukakukaribisha, au ukiwa uchi tukakuvika?
and when saw we thee a stranger, and took thee in? or naked, and clothed thee?
39 Tena ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa tukakutunza, au ukiwa kifungoni tukakutembelea?’
or when did we see thee sick, or in prison, and come to thee?
40 “Naye Mfalme atawajibu, ‘Amin nawaambia, kwa jinsi mlivyomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.’
And the king will answer and say to them, Truly do I say to you, Inasmuch as ye did it to one of the least of these my brethren, ye did it to me.
41 “Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, ‘Ondokeni kwangu, ninyi mliolaaniwa, nendeni kwenye moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya ibilisi na malaika zake. (aiōnios g166)
Then will he say also to those on the left hand, Depart from me, ye cursed, into the everlasting fire, which is prepared for the Devil and his angels. (aiōnios g166)
42 Kwa maana nilikuwa na njaa hamkunipa chakula, nilikuwa na kiu hamkuninywesha,
For I was hungry, and ye gave me no food; I was thirsty, and ye gave me no drink;
43 nilikuwa mgeni nanyi hamkunikaribisha, nilikuwa uchi hamkunivika, nilikuwa mgonjwa hamkunitunza, na nilikuwa gerezani nanyi hamkuja kunitembelea.’
I was a stranger, and ye took me not in; naked, and ye clothed me not; sick, and in prison, and ye visited me not.
44 “Ndipo wao pia watajibu, ‘Bwana ni lini tulikuona ukiwa na njaa au kiu, au ukiwa mgeni au uchi, au ukiwa mgonjwa na kifungoni na hatukukuhudumia?’
Then will they also answer, saying, Lord, when saw we thee hungry, or thirsty, or a stranger, or naked, or sick, or in prison, and did not minister to thee?
45 “Naye atawajibu, ‘Amin nawaambia, kwa jinsi ambavyo hamkumtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, hamkunitendea mimi.’
Then will he answer them, saying, Truly do I say to you, Inasmuch as ye did it not to one of the least of these, ye did it not to me.
46 “Ndipo hawa watakapoingia kwenye adhabu ya milele, lakini wale wenye haki wataingia katika uzima wa milele.” (aiōnios g166)
And these will go away into everlasting punishment; but the righteous into everlasting life. (aiōnios g166)

< Mathayo 25 >