< Mathayo 22 >

1 Yesu akasema nao tena kwa mifano, akawaambia,
Yesu alisema nao tena kwa kutumia mifano:
2 “Ufalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme mmoja aliyemwandalia mwanawe karamu ya arusi.
“Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme aliyemwandalia mwanawe karamu ya arusi.
3 Akawatuma watumishi wake kuwaita wale waliokuwa wamealikwa karamuni, lakini wakakataa kuja.
Basi, akawatuma watumishi kuwaita walioalikwa waje arusini, lakini walioalikwa hawakutaka kufika.
4 “Kisha akawatuma watumishi wengine akisema, ‘Waambieni wale walioalikwa kwamba nimeandaa chakula. Nimekwisha kuchinja mafahali wangu na vinono, karamu iko tayari. Karibuni kwa karamu ya arusi.’
Akawatuma tena watumishi wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa: karamu yangu iko tayari sasa; fahali wangu na ng'ombe wanono wamekwisha chinjwa; kila kitu ni tayari, njoni arusini.
5 “Lakini hawakuzingatia, wakaenda zao: huyu shambani mwake na mwingine kwenye biashara zake.
Lakini wao hawakujali, wakaenda zao; mmoja shambani kwake, mwingine kwenye shughuli zake,
6 Wengine wao wakawakamata wale watumishi wake, wakawatesa na kuwaua.
na wengine wakawakamata wale watumishi wakawatukana, wakawaua.
7 Yule mfalme akakasirika sana, akapeleka jeshi lake likawaangamiza wale wauaji na kuuteketeza mji wao kwa moto.
Yule mfalme akakasirika, akawatuma askari wake wakawaangamize wauaji hao na kuuteketeza mji wao.
8 “Kisha akawaambia watumishi wake, ‘Karamu ya arusi imeshakuwa tayari, lakini wale niliowaalika hawakustahili kuja.
Kisha akawaambia watumishi wake: Karamu ya arusi iko tayari kweli, lakini walioalikwa hawakustahili.
9 Kwa hiyo nendeni katika njia panda mkamwalike karamuni yeyote mtakayemwona.’
Basi, nendeni kwenye barabara na wowote wale mtakaowakuta waiteni waje arusini.
10 Wale watumishi wakaenda barabarani, wakawakusanya watu wote waliowaona, wema na wabaya. Ukumbi wa arusi ukajaa wageni.
Wale watumishi wakatoka, wakaenda njiani, wakawaleta watu wote, wabaya na wema. Nyumba ya arusi ikajaa wageni.
11 “Lakini mfalme alipoingia ndani ili kuwaona wageni, akamwona mle mtu mmoja ambaye hakuwa amevaa vazi la arusi.
“Mfalme alipoingia kuwaona wageni, akamwona mtu mmoja ambaye hakuvaa mavazi ya arusi.
12 Mfalme akamuuliza, ‘Rafiki, uliingiaje humu bila vazi la arusi?’ Yule mtu hakuwa na la kusema.
Mfalme akamwuliza, Rafiki, umeingiaje hapa bila vazi la arusi? Lakini yeye akakaa kimya.
13 “Ndipo mfalme akawaambia watumishi wake, ‘Mfungeni mikono na miguu mkamtupe nje, kwenye giza. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.’
Hapo mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni miguu na mikono mkamtupe nje gizani; huko atalia na kusaga meno.”
14 “Kwa maana walioitwa ni wengi, lakini walioteuliwa ni wachache.”
Yesu akamaliza kwa kusema, “Wengi wamealikwa, lakini wachache wameteuliwa.”
15 Ndipo Mafarisayo wakatoka nje wakaandaa mpango wa kumtega Yesu katika maneno yake.
Kisha, Mafarisayo wakaenda zao, wakashauriana jinsi ya kumnasa Yesu kwa maneno yake.
16 Wakatuma wanafunzi wao kwake pamoja na Maherode. Nao wakasema, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwadilifu na unafundisha njia ya Mungu katika kweli bila kuyumbishwa na mtu wala kuonyesha upendeleo.
Basi, wakawatuma wafuasi wao pamoja na wafuasi wa kikundi cha Herode. Wakamwuliza, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu, na kwamba wafundisha njia ya Mungu kwa uaminifu; humwogopi mtu yeyote, maana cheo cha mtu si kitu kwako.
17 Tuambie basi, wewe unaonaje? Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la?”
Haya, twambie maoni yako. Je, ni halali au la, kulipa Kaisari?”
18 Lakini Yesu, akijua makusudi yao mabaya, akawaambia, “Enyi wanafiki, kwa nini mnajaribu kunitega?
Lakini Yesu alitambua uovu wao, akawaambia, “Enyi
19 Nionyesheni hiyo sarafu inayotumika kwa kulipia kodi.” Wakamletea dinari.
Nionyesheni fedha ya kulipia kodi.” Nao wakamtolea sarafu ya fedha. sarafu ya fedha.
20 Naye akawauliza, “Sura hii ni ya nani? Na maandishi haya ni ya nani?”
Basi, Yesu akawauliza, “Sura na chapa hii ni ya nani?”
21 Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.” Basi Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.”
Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.” Hapo Yesu akawaambia, “Basi, mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari, na Mungu yaliyo yake Mungu.”
22 Waliposikia hili, wakashangaa. Hivyo wakamwacha, wakaenda zao.
Waliposikia hivyo wakashangaa; wakamwacha, wakaenda zao.
23 Siku hiyo hiyo Masadukayo, wale wasemao kwamba hakuna ufufuo wa wafu, wakamjia Yesu na kumuuliza swali, wakisema,
Siku hiyo, baadhi ya Masadukayo walimwendea Yesu. Hao ndio wale wasemao kwamba wafu hawafufuki.
24 “Mwalimu, Mose alisema, ‘Kama mtu akifa bila kuwa na watoto, ndugu yake inampasa amwoe huyo mjane ili ampatie watoto huyo nduguye aliyekufa.’
Basi, wakamwambia, “Mwalimu, Mose alisema mtu aliyeoa akifa bila kuacha watoto, lazima ndugu yake amwoe huyo mama mjane, amzalie ndugu yake watoto.
25 Basi palikuwa na ndugu saba miongoni mwetu. Yule wa kwanza akaoa mke, naye akafa, na kwa kuwa hakuwa na watoto, akamwachia nduguye yule mjane.
Sasa, hapa petu palikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa kisha akafa bila kujaliwa watoto, akamwachia ndugu yake huyo mke wake mjane.
26 Ikatokea vivyo hivyo kwa yule ndugu wa pili, na wa tatu, hadi wote saba.
Ikawa vivyo hivyo kwa ndugu wa pili, na wa tatu, mpaka wa saba.
27 Hatimaye, yule mwanamke naye akafa.
Baada ya ndugu hao wote kufa, akafa pia yule mama.
28 Sasa basi, siku ya ufufuo, yeye atakuwa mke wa nani miongoni mwa wale ndugu saba, kwa kuwa wote walikuwa wamemwoa huyo mwanamke?”
Je, siku wafu watakapofufuka mama huyo atakuwa mke wa nani miongoni mwa wale ndugu saba? Maana Wote saba walimwoa.”
29 Yesu akawajibu, “Mwapotoka kwa sababu hamjui Maandiko wala uweza wa Mungu.
Yesu akawajibu, “Kweli mmekosea kwa sababu hamjui Maandiko Matakatifu wala nguvu ya Mungu!
30 Wakati wa ufufuo, watu hawataoa wala kuolewa, bali watakuwa kama malaika wa mbinguni.
Maana wafu watakapofufuliwa hawataoa wala kuolewa, watakuwa kama malaika mbinguni.
31 Lakini kuhusu ufufuo wa wafu, hamjasoma kile Mungu alichowaambia, kwamba,
Lakini kuhusu suala la wafu kufufuka, hamjasoma yale aliyowaambieni Mungu?
32 ‘Mimi ni Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo’? Yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai.”
Aliwaambia, Mimi ni Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo! Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai.”
33 Ule umati wa watu uliposikia hayo, ulishangaa sana kwa mafundisho yake.
Ule umati wa watu uliposikia hivyo ukayastaajabia mafundisho yake.
34 Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazisha Masadukayo, Mafarisayo wakakusanyika pamoja.
Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazisha Masadukayo, wakakutana pamoja.
35 Mmoja wao, mtaalamu wa sheria, akamuuliza swali ili kumjaribu, akisema,
Mmoja wao, mwanasheria, akamwuliza Yesu kwa kumjaribu,
36 “Mwalimu, ni amri ipi katika Sheria iliyo kuu kuliko zote?”
“Mwalimu, ni amri ipi iliyo kuu katika Sheria ya Mose?”
37 Yesu akamjibu, “‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’
Yesu akamjibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na kwa akili yako yote.
38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
Hii ndiyo amri kuu ya kwanza.
39 Nayo ya pili ni kama hiyo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’
Ya pili inafanana na hiyo: Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe.
40 Amri hizi mbili ndizo msingi wa Sheria na Manabii.”
Sheria yote ya Mose na mafundisho ya manabii vinategemea amri hizi mbili.”
41 Wakati Mafarisayo walikuwa wamekusanyika pamoja, Yesu akawauliza,
Mafarisayo walipokusanyika pamoja, Yesu aliwauliza,
42 “Mnaonaje kuhusu Kristo? Yeye ni mwana wa nani?” Wakamjibu, “Yeye ni mwana wa Daudi.”
“Ninyi mwaonaje juu ya Kristo? Je, ni mwana wa nani?” Wakamjibu, “Wa Daudi.”
43 Akawaambia, “Inakuwaje basi kwamba Daudi, akinena kwa kuongozwa na Roho, anamwita Kristo ‘Bwana’? Kwa maana asema,
Yesu akawaambia, “Basi, inawezekanaje kwamba kwa nguvu ya Roho Mtakatifu Daudi anamwita yeye Bwana? Maana alisema:
44 “‘Bwana alimwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.”’
Bwana alimwambia Bwana wangu: keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.
45 Kama basi Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ awezaje kuwa mwanawe?”
Basi, ikiwa Daudi anamwita Kristo Bwana, anawezaje kuwa mwanawe?”
46 Hakuna mtu aliyeweza kumjibu Yesu neno. Tena tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu kumuuliza tena maswali.
Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumjibu neno. Na tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu tena kumwuliza swali.

< Mathayo 22 >