< Marko 6 >
1 Yesu akaondoka huko na kwenda mji wa kwao, akiwa amefuatana na wanafunzi wake.
耶穌離開那裏,來到自己的家鄉;門徒也跟從他。
2 Ilipofika siku ya Sabato, akaanza kufundisha katika sinagogi, na wengi waliomsikia wakashangaa. Nao wakauliza, “Mtu huyu ameyapata wapi mambo haya yote? Tazama ni hekima ya namna gani hii aliyopewa? Tazama matendo ya miujiza ayafanyayo kwa mikono yake!
到了安息日,他在會堂裏教訓人。眾人聽見,就甚希奇,說:「這人從哪裏有這些事呢?所賜給他的是甚麼智慧?他手所做的是何等的異能呢?
3 Huyu si yule seremala, mwana wa Maria? Na ndugu zake si Yakobo, Yose, Yuda na Simoni? Dada zake wote si tuko nao hapa kwetu?” Nao wakachukizwa sana kwa ajili yake, wakakataa kumwamini.
這不是那木匠嗎?不是馬利亞的兒子雅各、約西、猶大、西門的長兄嗎?他妹妹們不也是在我們這裏嗎?」他們就厭棄他。
4 Yesu akawaambia, “Nabii hakosi heshima isipokuwa katika mji wake mwenyewe, na miongoni mwa jamaa na ndugu zake, na nyumbani kwake.”
耶穌對他們說:「大凡先知,除了本地、親屬、本家之外,沒有不被人尊敬的。」
5 Hakufanya miujiza yoyote huko isipokuwa kuweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache na kuwaponya.
耶穌就在那裏不得行甚麼異能,不過按手在幾個病人身上,治好他們。
6 Naye akashangazwa sana kwa jinsi wasivyokuwa na imani. Kisha Yesu akawa anakwenda kutoka kijiji kimoja hadi kingine akifundisha.
他也詫異他們不信,就往周圍鄉村教訓人去了。
7 Akawaita wale kumi na wawili, akawatuma wawili wawili, na kuwapa mamlaka kutoa pepo wachafu.
耶穌叫了十二個門徒來,差遣他們兩個兩個地出去,也賜給他們權柄,制伏污鬼;
8 Akawaagiza akisema, “Msichukue chochote kwa ajili ya safari isipokuwa fimbo tu. Msichukue mkate, wala mkoba, wala fedha kwenye mikanda yenu.
並且囑咐他們:「行路的時候不要帶食物和口袋,腰袋裏也不要帶錢,除了柺杖以外,甚麼都不要帶;
9 Vaeni viatu, lakini msivae nguo ya ziada.”
只要穿鞋,也不要穿兩件褂子」;
10 Akawaambia, “Mkiingia kwenye nyumba yoyote, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo.
又對他們說:「你們無論到何處,進了人的家,就住在那裏,直到離開那地方。
11 Kama mahali popote hawatawakaribisha wala kuwasikiliza, mtakapoondoka huko, kungʼuteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.”
何處的人不接待你們,不聽你們,你們離開那裏的時候,就把腳上的塵土跺下去,對他們作見證。」
12 Kwa hiyo wakatoka na kuhubiri kwamba inawapasa watu kutubu na kuacha dhambi.
門徒就出去傳道,叫人悔改,
13 Wakatoa pepo wachafu wengi, wakawapaka wagonjwa wengi mafuta na kuwaponya.
又趕出許多的鬼,用油抹了許多病人,治好他們。
14 Mfalme Herode akasikia habari hizi, kwa maana jina la Yesu lilikuwa limejulikana sana. Watu wengine walikuwa wakisema, “Yohana Mbatizaji amefufuliwa kutoka kwa wafu, ndiyo sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.”
耶穌的名聲傳揚出來。希律王聽見了,就說:「施洗的約翰從死裏復活了,所以這些異能由他裏面發出來。」
15 Wengine wakasema, “Yeye ni Eliya.” Nao wengine wakasema, “Yeye ni nabii, kama mmojawapo wa wale manabii wa zamani.”
但別人說:「是以利亞。」又有人說:「是先知,正像先知中的一位。」
16 Lakini Herode aliposikia habari hizi, akasema, “Huyo ni Yohana Mbatizaji, niliyemkata kichwa, amefufuliwa kutoka kwa wafu!”
希律聽見卻說:「是我所斬的約翰,他復活了。」
17 Kwa kuwa Herode alikuwa ameagiza kwamba Yohana Mbatizaji akamatwe, afungwe na kutiwa gerezani. Alifanya hivi kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake, ambaye Herode alikuwa amemwoa.
先是希律為他兄弟腓力的妻子希羅底的緣故,差人去拿住約翰,鎖在監裏,因為希律已經娶了那婦人。
18 Yohana alikuwa amemwambia Herode, “Si halali kwako kuwa na mke wa ndugu yako.”
約翰曾對希律說:「你娶你兄弟的妻子是不合理的。」
19 Kwa hiyo Herodia alikuwa amemwekea Yohana kinyongo akataka kumuua. Lakini hakuweza,
於是希羅底懷恨他,想要殺他,只是不能;
20 kwa sababu Herode alimwogopa Yohana akijua kwamba ni mtu mwenye haki na mtakatifu, hivyo akamlinda. Herode alifadhaika sana alipomsikia Yohana, lakini bado alipenda kumsikiliza.
因為希律知道約翰是義人,是聖人,所以敬畏他,保護他,聽他講論,就多照着行,並且樂意聽他。
21 Mfalme Herode alifanya karamu kubwa wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwake. Akawaalika maafisa wake wakuu, majemadari wa jeshi na watu mashuhuri wa Galilaya. Hatimaye Herodia alipata wasaa aliokuwa akiutafuta.
有一天,恰巧是希律的生日,希律擺設筵席,請了大臣和千夫長,並加利利作首領的。
22 Binti yake Herodia alipoingia na kucheza, akamfurahisha Herode pamoja na wageni wake walioalikwa chakulani. Mfalme Herode akamwambia yule binti, “Niombe kitu chochote utakacho, nami nitakupa.”
希羅底的女兒進來跳舞,使希律和同席的人都歡喜。王就對女子說:「你隨意向我求甚麼,我必給你。」
23 Tena akamwahidi kwa kiapo, akamwambia, “Chochote utakachoomba nitakupa, hata kama ni nusu ya ufalme wangu.”
又對她起誓說:「隨你向我求甚麼,就是我國的一半,我也必給你。」
24 Yule binti akatoka nje, akaenda kumuuliza mama yake, “Niombe nini?” Mama yake akamjibu, “Omba kichwa cha Yohana Mbatizaji.”
她就出去對她母親說:「我可以求甚麼呢?」她母親說:「施洗約翰的頭。」
25 Yule binti akarudi haraka kwa mfalme, akamwambia, “Nataka unipe sasa hivi kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia.”
她就急忙進去見王,求他說:「我願王立時把施洗約翰的頭放在盤子裏給我。」
26 Mfalme akasikitika sana, lakini kwa sababu alikuwa ameapa viapo mbele ya wageni wake, hakutaka kumkatalia.
王就甚憂愁;但因他所起的誓,又因同席的人,就不肯推辭,
27 Mara mfalme akatuma askari mmojawapo wa walinzi wake kukileta kichwa cha Yohana. Akaenda na kumkata Yohana kichwa humo gerezani,
隨即差一個護衛兵,吩咐拿約翰的頭來。護衛兵就去,在監裏斬了約翰,
28 akakileta kichwa chake kwenye sinia na kumpa yule msichana, naye yule msichana akampa mama yake.
把頭放在盤子裏,拿來給女子,女子就給她母親。
29 Wanafunzi wa Yohana walipopata habari hizi, wakaja na kuuchukua mwili wake, wakauzika kaburini.
約翰的門徒聽見了,就來把他的屍首領去,葬在墳墓裏。
30 Wale mitume wakakusanyika kwa Yesu na kumpa taarifa ya mambo yote waliyokuwa wamefanya na kufundisha.
使徒聚集到耶穌那裏,將一切所做的事、所傳的道全告訴他。
31 Basi kwa kuwa watu wengi mno walikuwa wakija na kutoka, hata wakawa hawana nafasi ya kula, Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Twendeni peke yetu mahali pa faragha, mpate kupumzika.”
他就說:「你們來,同我暗暗地到曠野地方去歇一歇。」這是因為來往的人多,他們連吃飯也沒有工夫。
32 Hivyo wakaondoka kwa mashua peke yao, wakaenda mahali pasipo na watu.
他們就坐船,暗暗地往曠野地方去。
33 Lakini watu wengi waliowaona wakiondoka, wakawatambua, nao wakaenda haraka kwa miguu kutoka miji yote, nao wakatangulia kufika.
眾人看見他們去,有許多認識他們的,就從各城步行,一同跑到那裏,比他們先趕到了。
34 Yesu alipofika kando ya bahari, aliona makutano makubwa ya watu, akawahurumia kwa maana walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Kwa hiyo akaanza kuwafundisha mambo mengi.
耶穌出來,見有許多的人,就憐憫他們,因為他們如同羊沒有牧人一般,於是開口教訓他們許多道理。
35 Mchana ulipokuwa umeendelea sana, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, nazo saa zimekwenda sana.
天已經晚了,門徒進前來,說:「這是野地,天已經晚了,
36 Waage watu ili waende mashambani na vijijini jirani, wakajinunulie chakula.”
請叫眾人散開,他們好往四面鄉村裏去,自己買甚麼吃。」
37 Lakini Yesu akawajibu, “Ninyi wapeni chakula.” Wakamwambia, “Je, twende tukanunue mikate ya dinari 200 ili tuwape watu hawa wale?”
耶穌回答說:「你們給他們吃吧。」門徒說:「我們可以去買二十兩銀子的餅給他們吃嗎?」
38 Akawauliza, “Kuna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie.” Walipokwisha kujua wakarudi, wakamwambia, “Kuna mikate mitano na samaki wawili.”
耶穌說:「你們有多少餅,可以去看看。」他們知道了,就說:「五個餅,兩條魚。」
39 Kisha Yesu akawaamuru wawaketishe watu makundi makundi kwenye majani,
耶穌吩咐他們,叫眾人一幫一幫地坐在青草地上。
40 nao wakaketi kwenye makundi ya watu mia mia na wengine hamsini hamsini.
眾人就一排一排地坐下,有一百一排的,有五十一排的。
41 Yesu akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi wake ili wawagawie wale watu wote. Pia akawagawia wote wale samaki wawili.
耶穌拿着這五個餅,兩條魚,望着天祝福,擘開餅,遞給門徒,擺在眾人面前,也把那兩條魚分給眾人。
42 Watu wote wakala, wakashiba.
他們都吃,並且吃飽了。
43 Nao wanafunzi wake wakakusanya vipande vilivyosalia vya mikate na samaki, wakajaza vikapu kumi na viwili.
門徒就把碎餅碎魚收拾起來,裝滿了十二個籃子。
44 Idadi ya wanaume waliokula walikuwa 5,000.
吃餅的男人共有五千。
45 Mara Yesu akawaambia wanafunzi wake waingie kwenye mashua watangulie kwenda Bethsaida, wakati yeye alikuwa akiwaaga wale makutano.
耶穌隨即催門徒上船,先渡到那邊伯賽大去,等他叫眾人散開。
46 Baada ya kuwaaga wale watu, akaenda mlimani kuomba.
他既辭別了他們,就往山上去禱告。
47 Ilipofika jioni, ile mashua ilikuwa imefika katikati ya bahari, na Yesu alikuwa peke yake katika nchi kavu.
到了晚上,船在海中,耶穌獨自在岸上;
48 Akawaona wanafunzi wake wanahangaika na kupiga makasia kwa nguvu, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Yesu akawaendea wanafunzi wake, akiwa anatembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita,
看見門徒因風不順,搖櫓甚苦。夜裏約有四更天,就在海面上走,往他們那裏去,意思要走過他們去。
49 lakini walipomwona akitembea juu ya maji, wakadhani ni mzimu. Wakapiga yowe,
但門徒看見他在海面上走,以為是鬼怪,就喊叫起來;
50 kwa sababu wote walipomwona waliogopa. Mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope!”
因為他們都看見了他,且甚驚慌。耶穌連忙對他們說:「你們放心!是我,不要怕!」
51 Akapanda ndani ya mashua nao, na ule upepo ukakoma! Wakashangaa kabisa,
於是到他們那裏,上了船,風就住了;他們心裏十分驚奇。
52 kwa kuwa walikuwa hawajaelewa kuhusu ile mikate. Mioyo yao ilikuwa migumu.
這是因為他們不明白那分餅的事,心裏還是愚頑。
53 Walipokwisha kuvuka, wakafika nchi ya Genesareti, wakatia nanga.
既渡過去,來到革尼撒勒地方,就靠了岸,
54 Mara waliposhuka kutoka mashua yao, watu wakamtambua Yesu.
一下船,眾人認得是耶穌,
55 Wakaenda katika vijiji vyote upesi, wakawabeba wagonjwa kwenye mikeka ili kuwapeleka mahali popote waliposikia kuwa Yesu yupo.
就跑遍那一帶地方,聽見他在何處,便將有病的人用褥子抬到那裏。
56 Kila mahali Yesu alipokwenda, iwe vijijini, mijini au mashambani, watu waliwaweka wagonjwa wao masokoni. Wakamwomba awaruhusu hao wagonjwa waguse japo upindo wa vazi lake. Nao wote waliomgusa waliponywa.
凡耶穌所到的地方,或村中,或城裏,或鄉間,他們都將病人放在街市上,求耶穌只容他們摸他的衣裳繸子;凡摸着的人就都好了。