< Marko 11 >
1 Walipokaribia Yerusalemu, wakafika Bethfage na Bethania katika Mlima wa Mizeituni. Yesu akawatuma wawili wa wanafunzi wake,
And when they were drawing near to Jerusalem and to Bethany, at the Mount of Olives, he sendeth forth two of his disciples,
2 akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu. Na hapo mtakapoingia kijijini, mtamkuta mwana-punda amefungwa hapo, ambaye hajapandwa na mtu bado. Mfungueni, mkamlete hapa.
and saith to them, Go to the village over against you; and immediately on entering it ye will find a colt tied, on which no man hath yet sat; loose and bring it.
3 Kama mtu yeyote akiwauliza, ‘Mbona mnamfungua?’ Mwambieni, ‘Bwana anamhitaji, na atamrudisha hapa baada ya muda mfupi.’”
And if any one say to you, Why do ye this? say, The Lord hath need of it, and will immediately send it back hither.
4 Wakaenda, wakamkuta mwana-punda amefungwa kando ya barabara, karibu na mlango wa nyumba.
And they went, and found the colt tied by the door without, on the street; and they loose it.
5 Walipokuwa wanamfungua, watu waliokuwa wamesimama karibu wakawauliza, “Mna maana gani mnapomfungua huyo mwana-punda?”
And some of those who were standing there said to them, What are ye about, loosing the colt?
6 Wakawajibu kama vile Yesu alivyokuwa amewaagiza, nao wale watu wakawaruhusu.
And they said to them as Jesus had commanded; and they let them go.
7 Kisha wakamleta huyo mwana-punda kwa Yesu na kutandika mavazi yao juu yake, naye akampanda.
And they bring the colt to Jesus, and put their garments on it; and he sat upon it.
8 Watu wengi wakatandaza mavazi yao barabarani, na wengine wakatandaza matawi waliyokuwa wamekata mashambani.
And many spread their garments on the road; and others boughs, having cut them from the fields.
9 Kisha wale waliokuwa wametangulia mbele na wale waliokuwa wakifuata nyuma wakapaza sauti, wakisema, “Hosana!” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!”
And they that went before, and they that followed, cried, Hosanna! Blessed is he that cometh in the name of the Lord!
10 “Umebarikiwa Ufalme unaokuja wa baba yetu Daudi!” “Hosana kwake yeye aliye juu!”
Blessed is the coming kingdom of our father David! Hosanna in the highest heavens!
11 Yesu akaingia Yerusalemu na kwenda Hekaluni. Akaangalia kila kitu kilichokuwamo, lakini kwa kuwa ilishakuwa jioni, akaenda zake Bethania pamoja na wale kumi na wawili.
And he entered Jerusalem, and the temple; and having looked round on all things, the evening being now come, he went out to Bethany, with the twelve.
12 Kesho yake walipokuwa wakitoka Bethania, Yesu alikuwa na njaa.
And on the morrow, when they had come from Bethany, he was hungry;
13 Akauona mtini kwa mbali, naye akaenda ili aone kama ulikuwa na matunda. Alipoufikia, akakuta una majani tu, kwa kuwa hayakuwa majira ya tini.
and seeing a fig-tree afar off having leaves, he went to see whether he might find anything on it; and on coming to it he found nothing but leaves; for the season of figs had not come.
14 Akauambia ule mti, “Tangu leo mtu yeyote asile kamwe matunda kutoka kwako.” Wanafunzi wake walimsikia akisema hayo. (aiōn )
And he answering said to it, Let no one eat fruit from thee henceforth for ever. And his disciples heard him. (aiōn )
15 Walipofika Yerusalemu, Yesu akaingia katika eneo la Hekalu, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakinunua na kuuza humo ndani. Akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilisha fedha, na pia viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa,
And they come to Jerusalem. And he went into the temple, and began to cast out those who sold and bought in the temple, and overturned the tables of the money-changers, and the seats of those who sold the doves;
16 wala hakumruhusu mtu yeyote kuchukua bidhaa kupitia ukumbi wa Hekalu.
and he suffered no one to carry any vessel through the temple.
17 Naye alipokuwa akiwafundisha, akasema, “Je, haikuandikwa kuwa: “‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote’? Lakini ninyi mmeifanya kuwa ‘pango la wanyangʼanyi.’”
And he taught, and said to them, Is it not written, “My house shall be called a house of prayer for all the nations? but ye have made it a den of robbers.”
18 Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria wakapata habari hizi, nao wakaanza kutafuta njia ya kumuua, kwa kuwa walikuwa wakimwogopa, kwa sababu umati wote ulikuwa unashangazwa na mafundisho yake.
And the chief priests and the scribes heard it, and sought how they might destroy him; for they feared him; because all the multitude was astonished at his teaching.
19 Ilipofika jioni, Yesu na wanafunzi wake wakatoka nje ya mji.
And when it became late, he went out of the city.
20 Asubuhi yake walipokuwa wakipita, wakauona ule mtini umenyauka kutoka juu hadi kwenye mizizi yake.
And in the morning, as they were passing by, they saw the fig-tree withered from the roots.
21 Petro akakumbuka na kumwambia Yesu, “Rabi, tazama! Ule mtini ulioulaani umenyauka!”
And Peter remembered and said to him, Rabbi, see! the fig-tree which thou didst curse is withered away.
22 Yesu akawajibu, “Mwaminini Mungu.
And Jesus answering saith to them, Have faith in God.
23 Amin, nawaambia, mtu yeyote atakayeuambia mlima huu, ‘Ngʼoka ukatupwe baharini,’ wala asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yametukia, atatimiziwa.
Truly do I say to you, that whoever shall say to this mountain, Be thou taken up, and cast into the sea, and shall not doubt in his heart, but shall believe that what he saith will come to pass, he shall have it.
24 Kwa sababu hiyo nawaambia, yoyote mtakayoyaomba mkisali, aminini ya kwamba mmeyapokea, nayo yatakuwa yenu.
Therefore I say to you, All things whatever ye pray for and ask, believe that ye have obtained, and ye shall have them.
25 Nanyi kila msimamapo kusali, sameheni mkiwa na neno na mtu, ili naye Baba yenu aliye mbinguni awasamehe ninyi makosa yenu. [
And when ye stand praying, forgive, if ye have aught against any one, that your Father who is in heaven may also forgive you your trespasses.
26 Lakini kama ninyi msiposamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]”
27 Wakafika tena Yerusalemu, na Yesu alipokuwa akitembea Hekaluni, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria pamoja na wazee wa watu wakamjia.
And they come again to Jerusalem. And as he was walking in the temple, there come to him the chief priests and the scribes and the elders;
28 Wakamuuliza, “Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Na ni nani aliyekupa mamlaka ya kufanya hayo?”
and they said to him, By what authority doest thou these things? or who gave thee this authority to do these things?
29 Yesu akawajibu, “Nitawauliza swali moja. Nijibuni, nami nitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.
And Jesus said to them, I will ask you one question; and answer me, and I will tell you by what authority I do these things.
30 Niambieni, je, ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni au kwa wanadamu?”
The baptism of John, was it from heaven, or from men? Answer me.
31 Wakahojiana wao kwa wao, wakisema, “Kama tukisema, ‘Ulitoka mbinguni,’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’
And they reasoned among themselves, saying, If we say, From heaven, he will say, Why then did ye not believe him?
32 Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’…” (Waliwaogopa watu, kwa sababu kila mtu aliamini kwamba Yohana alikuwa nabii wa kweli.)
But shall we say, From men? They feared the people; for all regarded John as truly a prophet.
33 Kwa hiyo wakamjibu Yesu, “Hatujui.” Naye Yesu akawaambia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.”
And they answered and said to Jesus, We do not know. And Jesus saith to them, Neither do I tell you by what authority I do these things.