< Malaki 4 >

1 “Hakika siku inakuja, itawaka kama tanuru. Wote wenye kiburi na kila mtenda mabaya watakuwa mabua makavu, na siku ile inayokuja itawawasha moto,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. “Hakuna mzizi wala tawi litakalosalia kwao.
Tazama, siku inakuja, inaka kama tanuru, ambayo wote wenye kiburi na waharifu watakuwa mabua. siku inakuja itawachoma,” asema Bwana wa Majeshi, “siku hiyo itaondoa mzizi au shina.
2 Bali kwenu ninyi mnaoliheshimu Jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mabawa yake. Nanyi mtatoka nje na kurukaruka kama ndama aliyeachiwa kutoka zizini.
Lakini kwenu mnaoliogopa jina langu, jua la haki litawaangazia na uponyaji katika mbawa zake. Mtarukaruka kama ndama zizini.
3 Kisha ninyi mtawakanyaga waovu, nao watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu siku ile nitakayofanya mambo haya,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.
Na waovu wote mtawakanyaga chini, watakuwa majivu chini ya nyazo za miguu yenu siku hiyo nitatenda,”asema Bwana wa Majeshi.
4 “Kumbukeni sheria ya mtumishi wangu Mose, amri na sheria nilizompa huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote.
Kumbukeni kutii sheria za mtumishi wangu Musa, mmri na sheria nilizomwamuru huko Horebu, kwa Israel wote.
5 “Tazama, nitawapelekea nabii Eliya kabla ya kuja siku ile iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana.
Tazama, nitamtuma Eliya nabii mbele ya siku kuu na yenye kutisha ya kuja kwa Bwana.
6 Ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, la sivyo nitakuja na kuipiga nchi kwa laana.”
Atarudisha moyo wa baba kwa watoto, na mioyo ya watoto kwa baba zao; ili kwamba nisije nikaiangamiza nchi kwa uharibifu wote.”

< Malaki 4 >