< Mambo ya Walawi 8 >

1 Bwana akamwambia Mose,
Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
2 “Waletee Aroni na wanawe mavazi yao, mafuta ya upako, fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kondoo dume wawili na kikapu chenye mikate iliyotengenezwa bila chachu.
“Walete Aroni na wanawe pamoja naye, mavazi na mafuta ya upako, fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kondoo dume wawili, na kikapu cha mkate usio na hamira.
3 Kisha kusanya mkutano wote kwenye ingilio la Hema la Kukutania.”
Ita kusanyiko lote kwenye ingilio la hema la kukutania.”
4 Mose akafanya kama Bwana alivyomwagiza, na mkutano ukakusanyika kwenye ingilio la Hema la Kukutania.
Kwa hiyo Musa akafanya kama Yahweh alivyomwamru, nalo kusanyiko lilikuja pamoja mbele ya ingilio la hema la kukutania. Kisha Musa akaliambia kusanyiko,
5 Mose akaliambia kusanyiko, “Hili ndilo Bwana ameagiza lifanyike.”
“Hivi ndivyo alivyotuamru Yahweh tutende.”
6 Kisha Mose akamleta Aroni na wanawe mbele, akawaosha kwa maji.
Musa akamleta Aroni na wanawe na kuwaosha kwa maji.
7 Akamvika Aroni koti, akamfunga mshipi, akamvika joho na kumvalisha kisibau. Pia akafunga kisibau juu yake na kukifunga kiunoni mwake kwa mshipi wake uliosokotwa kwa ustadi.
Akamvika Aroni kanzu ya ndani yenye urefu wa kufika magotini na kumfunga ukumbuu kiunoni mwake, akamvika joho la nje lenye mikono mirefu na kumvika kile kizibao chenye vipande viwili tumboni na mgongoni na kukifunga kuzunguka kiunoni mwake kwa mshipi uliosokotwa kwa ustadi na kukikaza mwilini mwake.
8 Akaweka kifuko cha kifuani juu yake, na kuweka Urimu na Thumimu kwenye hicho kifuko.
Kisha Musa akaweka kifuko kifuani mwa Aroni, na ndani ya kifuko hicho akaweka Urimu na Thumimu.
9 Kisha akamvika Aroni kilemba kichwani pake, akaweka lile bamba la dhahabu, yaani ile taji takatifu, upande wa mbele wa kilemba, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
Na kisha akamfunga kiremba kichwani, na juu ya kiremba kwa mbele, akaweka bamba la dhahabu; liwe taji takatifu, kama Yahweh alivyomwamru yeye.
10 Ndipo Mose akachukua mafuta ya upako na kuipaka maskani na kila kitu kilichokuwamo ndani yake, kisha akaviweka wakfu.
Musa akayatwaa hayo mafuta ya upako, akalipaka lile hema la kukutania na kila kitu kilichokuwamo ndani yake na kuvitenga kwa ajili ya Yahweh.
11 Akanyunyiza baadhi ya mafuta juu ya madhabahu mara saba, akaipaka madhabahu mafuta na vyombo vyake vyote pamoja na sinia na kinara chake, ili kuviweka wakfu.
Akayanyunyiza hayo mafuta juu ya madhabahu mara saba, na kisha akaipaka mafuta hiyo madhabahu na vyombo vyake vyote, na sinia la kunawia na kitako chake ili kuvitenga wa ajili ya Yahweh.
12 Akamimina sehemu ya hayo mafuta ya upako kichwani mwa Aroni, akamtia mafuta ili kumweka wakfu.
Akamimina sehemu ya mafuta ya upako juu ya kichwa cha Aroni na kisha akampaka mafuta ili kumtenga.
13 Kisha akawaleta wana wa Aroni mbele, akawavika makoti, akawafunga mishipi na kuwavika vilemba, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
Musa akawaleta wana wa Aroni na kuwavika kila mmoja kanzu ya ndani yenye urefu wa kufika magotini. Kila mmoja wao akamfunga kwa ukumbuu kiunoni mwake na kuwafunga vitambaa vya kitani kichwani pao, kama vile Yahweh alivyokuwa amemru Musa.
14 Kisha akamtoa fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, nao Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa chake.
Musa akamleta huyo fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, naye Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha fahali ambaye wamemelete kwa ajili ya sadaka ya dhambi.
15 Mose akamchinja yule fahali na akachukua sehemu ya hiyo damu, kisha kwa kidole chake akaitia kwenye pembe zote za madhabahu ili kutakasa madhabahu. Akaimwaga damu iliyobaki chini ya madhabahu. Kwa hiyo akayaweka wakfu ili kufanya upatanisho kwa ajili ya madhabahu.
Musa akamchinja, na kisha akachukua sehemu ya damu yake kwa kidole chake na kuiweka juu ya mpembe za madhabahu, akaitakasa hiyo madhabahu, na kuitenga kwa Mungu, ambapo kwa kufanya hivyo, aliisababisha madhabahu kuwa sehemu ya kufaa kwa kufanyia upatanisho.
16 Pia Mose akachukua mafuta yote yanayozunguka sehemu za ndani, mafuta yanayofunika ini, figo zote mbili pamoja na mafuta yake, akayateketeza juu ya madhabahu.
Akachukua mafuta yote yaliyokuwa sehemu za ndani, kile kiwambo cha ini, zile figo mbili pamoja na mafuta yake, Musa akaichoma hiyo nyama yote juu ya madhabahu.
17 Lakini fahali, ikiwa pamoja na ngozi yake na nyama yake na sehemu zake za ndani na matumbo, akaiteketeza nje ya kambi, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
Lakini yule fahali, ngozi yake, nyama yake na kinyesi chake, akavichoma nje ya kambi, kama vile Yehweh alivyokuwa amemwamru yeye.
18 Kisha Mose akamleta kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, naye Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa chake.
Musa akamleta yule konndoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, naye Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha huyo kondoo.
19 Ndipo Mose akamchinja yule kondoo dume na kunyunyiza damu yake pande zote za madhabahu.
Musa akamchinja kondoo na kuinyunyizia damu yake kila upande wa madhabahu.
20 Mose akamkata yule kondoo dume vipande vipande na kukiteketeza kichwa, vile vipande na yale mafuta.
Naye akamkatakata kondoo vipande vipande na akakiteketeza kichwa chake pamoja na vile vipande na mafuta.
21 Kisha akamsafisha sehemu za ndani na miguu kwa maji, na kumteketeza yule kondoo dume mzima juu ya madhabahu kuwa sadaka ya kuteketezwa, harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
Akaziosha kwa maji zile sehemu za ndani pamoja na miguu na akamteketeza kandoo mzima juu ya madhabahu. Ilikuwa ni dhabihu ya kuteketezwa na ilitoa harufu ya kupendeza, sadaka iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamru Musa.
22 Kisha akaleta kondoo dume mwingine, ndiye kondoo dume kwa ajili ya kuwaweka wakfu, naye Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa chake.
Kisha Musa akamleta yule kondoo dume mwingine, kondoo wa kuwekwa wakfu, naye Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha kondoo.
23 Mose akamchinja yule kondoo dume, akaichukua sehemu ya damu yake na kuipaka juu ya ncha ya sikio la kuume la Aroni, na juu ya kidole gumba cha mkono wake wa kuume na juu ya kidole kikubwa cha mguu wake wa kuume.
Aroni akamchinja, naye Musa akachukua sehemu ya damu na kuiweka kwenye ncha ya sikio la Aroni la kulia, juu ya dole gumba la mkono wake wa kulia, na kwenye kidole kikumbwa cha mguu wake wa kulia.
24 Pia Mose akawaleta hao wana wa Aroni mbele, akaipaka sehemu ya hiyo damu kwenye ncha za masikio yao ya kuume, juu ya vidole gumba vya mikono yao ya kuume, na juu ya vidole vikubwa vya miguu yao ya kuume. Kisha akanyunyiza damu pande zote za madhabahu.
Akawaleta wana wa Aroni, naye akaweka sehemu ya damu ya kondoo yule kwenye ncha ya sikio lao la kulia, kwenye dole gumba lao cha mkono wa kulia na kwenye kidole chao kikubwa cha mguu wa kulia. Kisha Musa akainyunyiza damu ya huyo kila upande wa madhabahu
25 Akachukua mafuta ya mnyama, mafuta ya mkia, mafuta yote yanayozunguka sehemu za ndani, mafuta yanayofunika ini, figo zote mbili pamoja na mafuta yake, na paja la kulia.
Naye akayatwaa yale mafuta, mafuta ya mkiani, mafuta liyolikuwa sehemu za ndani, na mafuta yafunikayo ini, zile figo mbili pamoja na mafuta yake na paja la kulia.
26 Kisha kutoka kwenye kikapu cha mikate iliyotengenezwa bila chachu, kilichokuwa mbele za Bwana, akachukua andazi moja, na jingine lililotengenezwa kwa mafuta, na mkate mwembamba; akaviweka hivi vyote juu ya mafungu ya mafuta ya mnyama, na juu ya lile paja la kulia.
Akachukua mkate mmoja kutoka kwenye kikapu cha mikate isiyo na hamira ambayoo ilikuwa mbele za Yahweh, akatwaa mkate moja usio na hamira, na mkate mmoja ulioandaliwa kwa mafuta, na mkate mwemba wa kaki na akaiweka juu ya mafuta na juu ya paja la kulia la kondoo.
27 Akaviweka hivi vyote mikononi mwa Aroni na wanawe, na kuviinua mbele za Bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa.
Akaiweka yote mikoni mwa Aroni na katika mikono ya wanawe na kuitikisa mbele za Yahweh kuwa sadaka ya kutikiswa
28 Kisha Mose akavichukua kutoka mikononi mwao na kuviteketeza juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kuwa sadaka ya kuwekwa wakfu, harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.
Kisha Musa akaichukua mikate hiyo kutoka mikononi mwao na kuiteketeza juu ya madhabahu kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Zilikuwa ni sadaka ya kuwekwa wakfu na ilitoa harufu ya kupendeza. Ilikuwa sadaka iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto.
29 Kisha akachukua kidari, kilicho fungu la Mose la kondoo dume kwa ajili ya kuwekwa wakfu, na kukiinua mbele za Bwana kama sadaka ya kuinuliwa, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
Musa akakichukua kidari na kukitikisa kuwa sadaka ya kutikiswa kwa Yahweh. Ilikuwa ni mgao wa Musa wa kondoo wa kuwekewa mikono kwa makuhani, Kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru yeye.
30 Kisha Mose akachukua sehemu ya mafuta ya upako, na sehemu ya damu kutoka kwenye madhabahu, na kuvinyunyiza juu ya Aroni na mavazi yake, na juu ya wanawe na mavazi yao. Kwa hiyo akamweka Aroni na mavazi yake wakfu, pamoja na wanawe na mavazi yao.
Musa akatwaa sehemu ya mafuta ya upako na damu iliyokuwa juu ya madhabahu; naye akayanyunyiza haya juu ya nguo za Aroni, juu ya nguo zake mwenyewe na juu ya nguo za wana wa Aruni waliokua pamoja naye. Kwa njia hii alimtenga Aroni na nguo zake, na wanawe na nguo zao kwa ajili ya Yahweh.
31 Kisha Mose akamwambia Aroni na wanawe, “Pika hiyo nyama kwenye ingilio la Hema la Kukutania, na uile hapo pamoja na mkate kutoka kwenye kikapu cha sadaka ya kuweka wakfu, kama nilivyoagiza, nikisema, ‘Aroni na wanawe wataila.’
Kwa hiyo Musa akawambia Aruni na wanawe, “Ipikeni nyama mbele ya ingilio la hema la kukutania, na hapo mtaila pamoja na mkate ulio kwenye kikapu cha kuwekwa wakfu, kama ilivyoamriwa, kusema, 'Aroni na wanawe wataila.'
32 Kisha teketeza nyama na mikate iliyobaki.
Masalio yoyote ya nyama na mikate utayateketeza kwa moto.
33 Msitoke kwenye ingilio la Hema la Kukutania kwa muda wa siku saba, mpaka siku zenu za kuwekwa wakfu ziwe zimetimia, kwa kuwa muda wenu wa kuwekwa wakfu utakuwa siku saba.
Na hamtatoka kwenye ingilio la hema la kukutania kwa muda wa siku saba, hata zitakapotimia siku za kuwekwa mikono kwenu. Kwa kuwa kwa muda wa siku saba, Yahweh atawaweka wakfu.
34 Lile lililofanyika leo liliagizwa na Bwana ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.
Kilichotendeka siku hii— Yahweh ndiye amekiamru kitendekeke ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.
35 Lazima mkae kwenye ingilio la Hema la Kukutania usiku na mchana kwa siku saba, na kufanya lile Bwana analolitaka, ili kwamba msife; kwa kuwa hilo ndilo nililoamriwa.”
Mtakaa kwenye ingilio la hema la kukutania mchana na usiku siku saba, nanyi ishikeni amri ya Yahweh ili msije mkafa, kwa sababu hivi ndivyo ilivyoamriwa.
36 Kwa hiyo Aroni na wanawe wakafanya kila kitu Bwana alichoamuru kupitia kwa Mose.
Kwa hiyo Aroni na wanawe wakafanya mambo yote ambayo Yahweh alikuwa amewaamru kwa kinywa cha Musa.

< Mambo ya Walawi 8 >