< Mambo ya Walawi 3 >
1 “‘Kama sadaka ya mtu ni sadaka ya amani, naye akatoa ngʼombe kutoka kundi, akiwa dume au jike, atamleta mnyama asiye na dosari mbele za Bwana.
“When you want to give a peace offering and you offer an animal from a herd of cattle, whether male or female, you must present one without any defects before the Lord.
2 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka yake na kumchinja penye ingilio la Hema la Kukutania. Ndipo makuhani wana wa Aroni watanyunyiza damu yake pande zote za madhabahu.
Put your hand on the head of the offering and kill it at the entrance to the Tent of Meeting. Then Aaron's sons the priests will sprinkle the blood on all sides of the altar.
3 Kutoka kwenye hiyo sadaka ya amani ataleta sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto: mafuta yote ya mnyama yafunikayo sehemu za ndani, ama yanayoungana na hizo sehemu za ndani,
From the peace offering you are to bring a food offering to the Lord: all the fat that covers the insides,
4 figo zote pamoja na mafuta yote yanayozizunguka karibu na kiuno na yale yanayofunika ini, ambayo atayaondoa pamoja na figo.
both kidneys with the fat on them by the loins, and the best part of the liver, which you are to remove together with the kidneys.
5 Kisha wana wa Aroni wataiteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa iliyoko juu ya kuni zinazowaka, kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.
Aaron's sons are to burn this on the altar on top of the burnt offering that is on the burning wood, as a food offering, to be accepted by the Lord.
6 “‘Kama akitoa kondoo au mbuzi kutoka kundi kama sadaka ya amani kwa Bwana, atamtoa dume au jike asiye na dosari.
When you want to give a peace offering and you offer an animal from a flock of sheep or goats, either male or female, you must present one without any defects before the Lord.
7 Kama akimtoa mwana-kondoo, atamleta mbele za Bwana.
If you are giving a lamb as your offering, you must present it before the Lord.
8 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka yake, naye atamchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Aroni watanyunyiza damu yake kwenye madhabahu pande zote.
Put your hand on the head of the offering and kill it in front of the Tent of Meeting. Then Aaron's sons the priests will sprinkle the blood on all sides of the altar.
9 Kutoka kwenye hiyo sadaka ya amani ataleta dhabihu iliyotolewa kwa Bwana kwa moto: mafuta yake, mafuta yote ya mkia uliokatwa karibu na uti wa mgongo, mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani au yale yanayounganika nazo,
From the peace offering you are to bring a food offering to the Lord made up of its fat: the whole fat tail removed from close to the tailbone, all the fat that covers the insides,
10 figo mbili pamoja na mafuta yanayozizunguka yaliyo karibu na kiuno na yale yanayofunika ini, ambayo atayatoa pamoja na figo.
both kidneys with the fat on them by the loins, and the best part of the liver, which you are to remove together with the kidneys.
11 Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu kama chakula, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.
Then the priest is to burn this on the altar as a food offering, a food offering to the Lord.
12 “‘Kama sadaka yake ni mbuzi, ataileta mbele za Bwana.
If your offering is a goat, you are to present it before the Lord.
13 Ataweka mkono wake juu ya kichwa chake na kumchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Aroni watanyunyiza damu yake kwenye madhabahu pande zote.
Put your hand on its head and kill it in front of the Tent of Meeting. Then Aaron's sons the priests will sprinkle the blood on all sides of the altar.
14 Kutokana na ile sadaka anayotoa, atatoa sadaka hii kwa Bwana kwa moto: mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani na yale yanayoungana nazo,
From your offering you are to present a food offering to the Lord made up of all the fat that covers the insides,
15 figo zote mbili pamoja na mafuta yaliyo juu yake karibu na kiuno na yanayofunika ini, ambayo atayaondoa pamoja na figo.
both kidneys with the fat on them by the loins, and the best part of the liver, which you are to remove together with the kidneys.
16 Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu kama chakula, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri. Mafuta yote ya mnyama ni ya Bwana.
Then the priest is to burn this on the altar as a food offering, an offering to the Lord using fire. All the fat is for the Lord.
17 “‘Hii ni kanuni ya kudumu kwa vizazi vijavyo, popote muishipo: Msile mafuta yoyote ya mnyama wala damu.’”
You must not eat any fat or any blood. This regulation is for all time and for all future generations everywhere you live.”