< Mambo ya Walawi 25 >

1 Bwana akamwambia Mose katika Mlima Sinai,
Yahweh akazungumza na Musa kwenye Mlima wa Sinai, akisema,
2 “Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapoingia katika nchi ninayowapa ninyi, nchi yenyewe ni lazima ishike Sabato kwa ajili ya Bwana.
“Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, “Mtakapoingia katika nchi ambayo ninawapa, kisha hiyo nchi lazima ifanywe iwe ya kuishika Sabato kwa ajili ya Yahweh.
3 Kwa miaka sita mtapanda mazao katika mashamba yenu, nanyi kwa miaka sita mtaikata mizabibu yenu matawi na kuvuna mazao yake.
Ni lazima mtapanda mazao yenu kwa miaka sita, na kwa miaka sita mtaikatia matawi mizabibu yenu na kukusanya mazao yake.
4 Lakini mwaka wa saba nchi lazima iwe na Sabato ya mapumziko, Sabato kwa Bwana. Msipande mbegu katika mashamba yenu, wala msikate mizabibu yenu matawi.
Lakini katika mwaka wa saba, Sabato ya pumziko la utulivu kwa nchi itashikwa, ni Sabato kwa Yahweh. Hamtapanda mashamba yenu wala kuikatia mizabibu yenu matawi yake.
5 Msivune na kuweka akiba kinachoota chenyewe, wala kuvuna na kusindika zabibu ambayo hamkuhudumia mashamba yake. Nchi lazima iwe na mwaka wa mapumziko.
Hamtasimamia mavuno yoyote ya mazao ya mizabibu iliyojiotesha yenyewe katika mashamba yenu ya mizabibu isiyokatiwa matawi. Huu utakuwa mwaka wa pumziko lenye utulivu kwa ardhi.
6 Chochote nchi itoacho katika mwaka wa Sabato kitakuwa chakula chenu wenyewe, watumishi wenu wa kiume na wa kike, mfanyakazi aliyeajiriwa, na mkazi wa muda anayeishi miongoni mwenu,
Chochote ardhi isiyofanyiwa kazi itakachotoa wakati wa Sabato ndicho kitakuwa chakula chako. Wewe mwenyewe, watumwa wako wa kiume na wa kike, watumishi wako wa kuajiriwa na wageni wanaoishi pamoja nawe mnaweza kujikusanyia chakula.
7 vilevile malisho ya mifugo yenu na wanyama pori katika nchi yenu. Chochote nchi itakachozalisha kinaweza kuliwa.
Na wnyama wako wa kufugwa na wanyama pori waweze kula chochote ardhi itoacho.
8 “‘Hesabu Sabato saba za miaka, yaani miaka saba mara saba, ili Sabato saba za miaka utakuwa muda wa miaka arobaini na tisa.
Ni lazima kwenu kuhesabu Sabato saba za miaka, yaani, saba mara miaka saba, ikifanya jumla ya miaka arobaini na tisa.
9 Ndipo tarumbeta itapigwa kila mahali katika siku ya kumi ya mwezi wa saba. Katika Siku ya Upatanisho, piga tarumbeta katika nchi yako yote.
Kisha mtapiga sauti ya tarumbeta kila mahali katika siku ya kumi ya mwezi wa saba. Katika Siku ya Upatanisho ni lazima mtapiga tarumbeta katika nchi yenu yote.
10 Mwaka wa hamsini mtauweka wakfu na kutangaza uhuru katika nchi kwa wakazi wake wote. Itakuwa ni yubile kwenu; kila mmoja wenu atairudia mali ya jamaa yake, na kila mmoja kurudi kwenye ukoo wake.
Nanyi mtautenga mwaka wa hamsini kwa ajili ya Yahweh na mtatangaza uhuru katika nchi yote kwa wakazi wote. Kutakuwa na Yubile kwa ajili yenu, ambayo kwayo mali na watumwa ni lazima warejeshwe kwa familia zao.
11 Mwaka wa hamsini utakuwa yubile kwenu, msipande wala msivune kile kiotacho chenyewe, au kuvuna zabibu zisizohudumiwa.
Mwaka wa saba kutakuwa na Yubile kwenu. Hamtapanda wala kusimamia mavuno ya kijioteshacho chenyewe, na kukusanya kichipukacho kwenye mizabibu isiyokatiwa matawi.
12 Kwa kuwa ni yubile, nayo itakuwa takatifu kwenu; mtakula tu kile kilichotoka moja kwa moja mashambani.
Kwa sababu hiyo ni Yubile takatifu kwenu. Nanyi mtakula mazao yanayokua yenyewe kutoka mashambani.
13 “‘Katika huu Mwaka wa Yubile, kila mmoja atarudi kwenye mali yake mwenyewe.
Ni lazima muwarejeshe kila mmoja kwenye miliki yake katika mwaka huu wa Yubile.
14 “‘Ikiwa utauza ardhi kwa mmoja wa wazawa wa nchi yako, au ukinunua ardhi kutoka kwake, mmoja asimpunje mwingine.
Iwapo utauza ardhi yoyote ya jirani yako au kununua ardhi yake, ni shrti msipunjane au kutendeana kwa hila.
15 Utanunua ardhi kwa mzawa wa nchi yako kwa misingi ya hesabu ya miaka baada ya Yubile. Naye ataiuza kwako kwa misingi ya hesabu ya miaka iliyobaki kwa kuvuna mavuno.
Iwapo unanunua ardhi kutoka kwa jirani yako, zingatia idadi ya miaka na mazao ambayo yaweza kuvunwa mpaka mwaka wa Yubile nyingine. Jirani yako anayeuza ardhi ni lazima aihesabu miaka hiyo pia.
16 Miaka inapokuwa mingi, utaongeza bei, nayo miaka ikiwa michache, utapunguza bei, kwa sababu kile anachokuuzia kwa hakika ni hesabu ya mazao.
Miaka inapoongezeka mpaka Yubile nyingine, ataongeza thamani ya ardhi, na miaka inapokuwa michache kufikia Yubile nyingine atashusha thamani, kwa sababu idadi ya mavuno inahusiana na idadi ya miaka kabla ya Yubile nyingine.
17 Mmoja asimpunje mwingine, bali utamcha Mungu wako. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.
Msipunjane au kutendeana kwa hila, badala yake, yawapasa kumheshi Yahweh Mungu wenu.
18 “‘Fuateni amri zangu, mwe waangalifu kutii amri zangu, nanyi mtaishi salama katika nchi.
Kwa hiyo basi, ni lazima muyatii maagiza, kuzitunza sheria zangu na kuzitekeleza. Nanyi mtaishi katika nchi katika usalama.
19 Kisha nchi itazaa matunda yake, nanyi mtakula na kushiba na kuishi humo kwa salama.
Nayo nchi itawapa mavuno yake, nanyi mtakula matunda yenu na mtaishi humo salama.
20 Mwaweza kuuliza, “Tutakula nini katika mwaka wa saba ikiwa hatutapanda wala kuvuna mazao yetu?”
Labda mtasema, Tutakula nini katika mwaka wa saba? Tazama, hatuwezi kupanda wala kukusanya mazao yetu.”
21 Nitawapelekeeni baraka ya pekee katika mwaka wa sita, kwamba nchi itazalisha mazao ya kutosha kwa miaka mitatu.
Nitaiamru baraaka yangu ije juu yenu katika mwaka wa sita, nayo itatoa mavuno ya kutosha kwa miaka mitatu.
22 Mnapopanda mwaka wa nane, mtakula mavuno ya miaka iliyopita. Pia mtaendelea kuyala mazao hayo hadi mvune mavuno ya mwaka wa tisa.
Mtapanda katika mwaka wa nane na mtaendelea kula mazao ya miaka iliyopita na kutoka kwenye ghala la chakula. Mpaka mavuno ya mwaka wa tisa yatakapofika, mtaweza kula kutoka kwenye riziki iliyohifadhiwa katika miaka iliyopita
23 “‘Kamwe ardhi isiuzwe kwa mkataba wa kudumu, kwa sababu nchi ni mali yangu, nanyi ni wageni na wapangaji wangu.
Ardhi haitauzwa kwa mmiliki mpya wa kudumu, kwa sababu ardhi ni mali yangu. Ninyi nyote mu wageni na wakazi wa muda juu ya ardhi yangu.
24 Katika nchi yote mtakayoshika kuwa milki yenu, ni lazima mtoe ukombozi wa ardhi.
Ni lazima muitunze haki ya ukombozi kwa ajili ya ardhi yote mtakayoimiliki; itawapasa kuruhusu ardhi inunuliwe tena na familia ambayo wewe uliinunua hiyo ardhi kutoka kwao.
25 “‘Ikiwa mmoja wa wazawa wa nchi yako amekuwa maskini na akauza baadhi ya mali yake, ndugu yake wa karibu atakuja na kukomboa kile ndugu yako alichokiuza.
Iwapo Mwisraeli mwenzako anakuwa masikini na kwa sababu hiyo anauza baadhi ya miliki yake, kisha jamaa yake wa karibu anaweza kuja na kuikomboa hiyo miliki ambayo jamaa yake kaiuza kwako.
26 Iwapo mtu huyo hana jamaa wa karibu wa kukomboa mali hiyo kwa ajili yake, lakini yeye mwenyewe akafanikiwa na kupata mali itoshayo kuikomboa,
Iwapo mtu hana jamaa wa kuikomboa mali yake, lakini ikiwa kafanikiwa na anao uwezo wa kuikomboa,
27 ataamua tena thamani yake kwa miaka tangu alipoiuza, na kurudisha kiasi kilichobaki cha thamani kwa mtu ambaye alikuwa amemuuzia mali hiyo, naye ataweza kuirudia mali yake.
kisha atahesabu miaka tangu ardhi hiyo ilipouzwa na kurejesha kwa mtu aliyemuuzia fedha iliyosalia. Naye anaweza kuerejea kwenye miliki yake mwenyewe.
28 Lakini kama hatapata njia ya kumlipa mnunuzi, ile mali aliyouza itabaki kumilikiwa na mnunuzi mpaka Mwaka wa Yubile. Mali hiyo itarudishwa mwaka wa Yubile, naye ataweza kuirudia mali yake.
Lakini ikiwa hawezi kuirejesha kwake ardhi aliyoiuza, nayo hiyo ardhi aliyoiuza itabaki katika umiliki wa yule aliyeinunua mpaka mwaka wa Yubile. Kwenye mwaka wa Yubile, ardhi itarejeshwa kwa mtu aliyeiuza, naye mmiliki wa asili atarejea kwenye mali yake.
29 “‘Ikiwa mtu atauza nyumba iliyo ndani ya mji uliozungukwa kwa ukuta, yeye anayo haki ya kuikomboa mwaka mzima baada ya mauzo ya hiyo nyumba. Wakati huo anaweza kuikomboa.
Ikiwa mtu anauza nyumba iliyo kwenye mji uliozungushiwa ukuta, naye anaweza kuinunua tena ndani ya mwaka baada ya kuuzwa. kwa kuwa, kwa mwaka mzima atakuwa na haki ya ukombozi.
30 Ikiwa haikukombolewa kabla ya mwaka mmoja kamili kupita, nyumba iliyo ndani ya mji uliozungukwa kwa ukuta itakuwa mali ya kudumu ya mnunuzi na wazao wake. Haitarudishwa mwaka wa Yubile.
Kama nyumba hiyo haitakombolewa kabla ya mwaka mzima, ndipo hiyo nyumba iliyoko kwenye mji uliozungushiwa ukuta itakuwa mali ya kudumu ya yule aliyeinunua, katika vizazi vyote vya uzao wake. Nyumba hiyo haitakuwa ya kurejeshwa katika mwaka wa Yubile.
31 Lakini nyumba zilizo vijijini bila ya kuwa na kuta zilizozizunguka zitahesabiwa kama mashamba. Zinaweza kukombolewa, nazo zirudishwe katika mwaka wa Yubile.
Lakini nyumba za vijijini zisizokuwa na ukuta kuzizunguuka, zitahesabiwa kuwa shamba la nchi. Zaweza kukombolewa, na ni lazima zirejeshwe katika mwaka wa Yubile.
32 “‘Walawi siku zote wana haki ya kukomboa nyumba zao katika miji ya Walawi wanayoimiliki.
Hata hivyo, nyumba zinazomilikiwa na makuhani katika miji yao zaweza kukombelewa wakati wowote.
33 Kwa hiyo mali ya Mlawi inaweza kukombolewa, yaani nyumba iliyouzwa katika mji wowote wanaoushikilia itarudishwa mwaka wa Yubile, kwa sababu nyumba zilizo katika miji ya Walawi ni mali yao miongoni mwa Waisraeli.
Iwapo mmoja wa makuhani haikombowi nyumba iliyozwa, kisha nyumba hiyo iliyouzwa katika miji ilimo, ni lazima irejeshwe katika mwaka wa Yubile, kwa kuwa nyumba za miji ya makuhani ni mali yao miongoni mwa watu wa Israeli.
34 Lakini nchi ya malisho iliyo mali ya miji yao kamwe isiuzwe, ni milki yao ya kudumu.
Lakini yale mashamba yanayozunguka miji yao hayataweza kuuzwa kwa sababu hiyo ni mali ya kudumu ya Makuhani.
35 “‘Ikiwa mmoja wa wazawa wa nchi yako amekuwa maskini, naye akashindwa kujitegemeza mwenyewe katikati yako, msaidie kama vile ambavyo ungelimsaidia mgeni au kama mkazi wa muda, ili aweze kuendelea kuishi katikati yako.
Ikiwa mwananchi mwenzako anakuwa masikini, kiasi kwamba hawezi kujihudumia, nawe utalazimika kumsaidia kama vile ungemsaidia mgeni au mwingine yeyote kutoka nje aishie miongoni mwenu.
36 Usichukue riba wala faida yoyote kutoka kwake, bali utamwogopa Mungu wako, ili mzawa wa nchi yako aweze kuendelea kuishi katikati yako.
Usimtoze riba au kujaribu kunufaika kutoka kwake katika njia yoyote, bali mheshimu Mungu wako ili kwamba ndugu yako aendelee kuishi nawe.
37 Usimkopeshe fedha ili alipe na riba, wala usimuuzie chakula kwa faida.
Hutampa mkopo wa fedha na kumtoza riba, wala hutamuuzia chakula chako ili kupata faida.
38 Mimi ndimi Bwana Mungu wako, niliyekuleta kutoka nchi ya Misri nikupe nchi ya Kanaani, nami niwe Mungu wako.
Mimi ndimi Yahweh Mungu wako, aliye kuleta wewe kutoka nchi ya Misri, ili kwamba Nikupe nchi ya Kanaani, na kwamba niwe Mungu wako.
39 “‘Ikiwa mmoja wa wazawa wa nchi yako amekuwa maskini katikati yako, naye akajiuza kwako, usimfanye atumike kama mtumwa.
Iwapo mwananchi mwenzako atakuwa masikini na kujiuza mwenyewe kwako, hutamfanyisha kazi kama mtumwa.
40 Atatendewa kama mfanyakazi aliyeajiriwa, au kama mkazi wa muda katikati yako, naye atatumika mpaka Mwaka wa Yubile.
Mtendee kama mtumishi wa kuajiriwa. Ni lazima awe kama yule ahudumuye nawe kwa muda mpaka mwaka wa Yubile.
41 Ndipo yeye na watoto wake wataachiwa, naye atarudi kwa watu wa ukoo wake, na kwenye mali ya baba zake.
Kisha ataondoka kwako, yeye mwenyewe na watoto wake pamoja naye, na atarejea kwenye familia yake mwenyewe na kwenye miliki ya baba yake.
42 Kwa sababu Waisraeli ni watumishi wangu niliowaleta kutoka nchi ya Misri, kamwe wasiuzwe kama watumwa.
Kwa sababu wao ni watumishi wangu niliowaleta kutoka katika nchi ya Misri. Hawatauzwa kama watumwa.
43 Usiwatawale kwa ukatili, lakini utamcha Mungu wako.
Usitawale juu yao kwa ukatili, bali yakupasa kumheshimu Mungu wako.
44 “‘Watumwa wako wa kiume na wa kike watatoka katika mataifa yanayokuzunguka; kutoka kwao waweza kununua watumwa.
Kwa upande wa watumwa wako wakiume na watumwa wako wa kike, unaowezao kuwapata kutok kwa mataifa yanayokuzunguka, waweza kununua watumwa kutoka kwao.
45 Pia waweza kununua baadhi ya wakazi wa muda wanaoishi katikati yako, na jamaa ya koo zao waliozaliwa katika nchi yako, nao watakuwa mali yako.
Unaweza pia kununua watumwa kutoka kwa wageni wanaoishi miongoni mwenu, yaani, kutoka familia zao waliopamoja nawe, wale wtoto waliozaliwa katika nchi yako. Wanaweza kuwa mali yako.
46 Hao waweza kuwarithisha watoto wako kuwa urithi wao, na wanaweza kuwafanya watumwa maisha yao yote, lakini usiwatawale ndugu zako Waisraeli kwa ukatili.
Unaweza kuzalisha watumwa hao kama urithi kwa watoto wako baada yako, ili kuwamiliki kama mali. Kutoka kwao waweza kununua watumwa daima, lakini hamtawezi kutawala kwa ukali juu ya ndugu zenu walio miogoni mwa watu wa Israeli.
47 “‘Ikiwa mgeni au mkazi wa muda katikati yako atakuwa tajiri, na mmoja wa wazawa wa nchi yako akawa maskini, naye akajiuza kwa yule mgeni anayeishi katikati yako, au kwa mmoja wa jamaa wa koo za wageni,
Iwapo mgeni anayeishi nawe kwa muda anakuwa tajiri, na ikiwa mmoja wa Waisraeli amekuwa masikini na kujuza mwenyewe kwa familia ya mgeni, au kwa mtu fulani katika familia,
48 anayo haki ya kukombolewa baada ya kujiuza. Mmoja wa jamaa zake aweza kumkomboa:
baada ya Mwisraeli mwenzako kuwa amenunuliwa. Anaweza kurejeshwa kwa maliopo. Iwapo anaweza kurejeshwa. Mtu fulani katika familia yake anaweza kumkomboa.
49 Mjomba wake, au binamu yake, au yeyote aliye ndugu wa damu katika ukoo wake aweza kumkomboa. Au ikiwa atafanikiwa, anaweza kujikomboa mwenyewe.
Anaweza kuwa mjomba wake, au mjomba wa mwanawe, anayemkomboa yeye, au yeyote aliye ndugu yake wa karibu kutoka kwa ukoo wake. Au, iwapo ni mwenye mafanikio, anaweza kujikomboa mwenyewe.
50 Yeye na huyo aliyemnunua watahesabu muda kuanzia mwaka aliojiuza hadi Mwaka wa Yubile. Mahali pa kuanzia bei ya kuachiwa kwake itakadiriwa kwa ujira unaolipwa mfanyakazi aliyeajiriwa kwa idadi ya hiyo miaka.
Ni lazima apatane na mtu aliyemnunua, itawapasa kuhesabu miaka tangu mwaka aliojiuza kwa mnunuzi wake mpaka mwaka wa Yubile. Ile thamani ya ukombozi wake ihesabiwe kulingana na kiwango cha mshahara anaolipwa mtumishi aliyeajiriwa, kwa idadi ya miaka ambayo angeweza kuendelea kufanya kazi kwa yule aliyemnunua.
51 Ikiwa imebaki miaka mingi, ni lazima atalipia ukombozi wake fungu kubwa la bei iliyolipwa kumnunua yeye.
Endapo kutakuwa kungali na miaka mingi iliyobaki mpaka mwaka wa Yubile, atalazimika kulipa fungu kubwa la fedha kwa ajili ya ukombozi ambao ni uwino wa idadi ya miaka hiyo.
52 Ikiwa miaka iliyobaki ni michache kufikia Mwaka wa Yubile, atafanya hesabu yake, naye atalipa malipo yanayostahili kwa ajili ya ukombozi wake.
Iwapo kuna miaka michache tu iliyobaki mpaka mwaka wa Yubile, atapatana na aliyemnunua ili kuipitia idadi ya miaka iliyobaki mpaka Yubile, naye atalazimika kulipia ukombozi wake kulingana na idadi ya miaka.
53 Atatendewa kama mtu wa kuajiriwa mwaka hadi mwaka; lazima uone kwamba yule aliyemnunua hamtawali kwa ukatili.
Naye atatendewa kama mtu aliyeajiriwa mwaka kwa mwaka. Utahakikisha kwamba hatendewi kwa ukali.
54 “‘Hata ikiwa hakukombolewa kwa njia mojawapo ya hizi, yeye na watoto wake wataachiwa katika Mwaka wa Yubile,
Iwapo hakukombolewa katika njia hizi, basi atatumika mpaka mwaka wa Yubile, yeye pamoja na watoto wake.
55 kwa maana Waisraeli ni mali yangu kama watumishi. Wao ni watumishi wangu, niliowatoa kutoka nchi ya Misri. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.
Kwangu mimi watu wa Israeli ni watumishi. Wao ni watumishi wangu ambao Niliwatoa katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.

< Mambo ya Walawi 25 >