< Maombolezo 5 >

1 Kumbuka, Ee Bwana, yaliyotupata, tazama, nawe uione aibu yetu.
Kumbuka, Yahweh, yaliyo tutokea na uone aibu yetu.
2 Urithi wetu umegeuziwa kwa wageni, na nyumba zetu kwa wageni.
Urithi wetu umegeuziwa kwa wageni; nyumba zetu kwa wageni.
3 Tumekuwa yatima wasio na baba, mama zetu wamekuwa kama wajane.
Tumekuwa yatima, bila baba, na mama zetu ni kama wajane.
4 Ni lazima tununue maji tunayokunywa, kuni zetu zapatikana tu kwa kununua.
Lazima tulipe fedha kwa maji tunayo kunywa, na tulipe fedha kupata mbao zetu.
5 Wanaotufuatilia wapo kwenye visigino vyetu, tumechoka na hakuna pumziko.
Hao wanakuja kwetu wamekaribia nyuma yetu; tumechoka na hatuwezi pata mapumziko.
6 Tumejitolea kwa Misri na Ashuru tupate chakula cha kutosha.
Tumejitoa kwa Misri na kwa Assiria tupate chakula cha kutosha.
7 Baba zetu walitenda dhambi na hawapo tena, na sisi tunachukua adhabu yao.
Baba zetu walifanya dhambi, na hawapo tena, na tumebeba dhambi zao.
8 Watumwa wanatutawala na hakuna wa kutuokoa mikononi yao.
Watumwa walitutawala, na hakuna wa kutuokoa na mikono yao.
9 Tunapata chakula chetu kwa kuhatarisha maisha yetu kwa sababu ya upanga jangwani.
Tunapata mkate wetu pale tunapo hatarisha maisha, kwasababu ya upanga wa nyikani.
10 Ngozi yetu ina joto kama tanuru, kwa sababu ya fadhaa itokanayo na njaa.
Ngozi zetu zimekuwa na moto kama jiko kwasababu ya joto la njaa.
11 Wanawake wametendwa jeuri katika Sayuni, na mabikira katika miji ya Yuda.
Wanawake wanabakwa Sayuni, na mabikra katika mji wa Yuda.
12 Wakuu wametungikwa juu kwa mikono yao, wazee hawapewi heshima.
Watoto wa mfalme wamenyongwa na mikono yao, na hakuna heshima inayoonyeshwa kwa wazee.
13 Vijana wanataabika kwenye mawe ya kusagia, wavulana wanayumbayumba chini ya mizigo ya kuni.
Wanaume vijana wanalizimishwa kusaga mbegu kwa jiwe la kusagia, na wavulana wanajikwa chini ya vifurushi vya kuni.
14 Wazee wameondoka langoni la mji, vijana wameacha kuimba nyimbo zao.
Wazee wameacha lango la mji, na vijana wameacha miziki.
15 Furaha imeondoka mioyoni mwetu, kucheza kwetu kumegeuka maombolezo.
Furaha ya moyo imekoma na kucheza kwetu kumegeuka kilio.
16 Taji imeanguka kutoka kichwani petu. Ole wetu, kwa maana tumetenda dhambi!
Taji limeanguka kichwani mwetu; ole wetu, kwa kuwa tumetenda dhambi!
17 Kwa sababu hiyo, mioyo yetu inazimia, kwa sababu ya hayo, macho yetu yamefifia,
Kwa kuwa moyo wetu umekuwa unaumwa, na machozi yetu ya fifia, kwa vitu hivi macho yetu yanafifia
18 kwa ajili ya Mlima Sayuni, ambao unakaa ukiwa, nao mbweha wanatembea juu yake.
maana Mlima Sayuni umelala ukiwa, mbwa wa mitaani wacheza juu yake.
19 Wewe, Ee Bwana unatawala milele, kiti chako cha enzi chadumu kizazi hadi kizazi.
Lakini wewe, Yahweh, unatawala milele, na utaketi katika kiti chako cha enzi vizazi na vizazi. Kwanini unatusahau milele?
20 Kwa nini watusahau siku zote? Kwa nini umetuacha kwa muda mrefu?
Kwanini unatutelekeza kwa siku nyingi?
21 Turudishe kwako mwenyewe, Ee Bwana, ili tupate kurudi. Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale,
Turejeshe kwako, Yahweh, na sisi tutarejea. Fanya upya siku zetu kama zilivyo kuwa hapo zamani -
22 isipokuwa uwe umetukataa kabisa na umetukasirikia pasipo kipimo.
vinginevyo labda uwe umetukataa na una hasira kwetu kupita kiasi.

< Maombolezo 5 >