< Waamuzi 15 >

1 Baada ya kitambo kidogo, wakati wa mavuno ya ngano, Samsoni akachukua mwana-mbuzi, kwenda kumzuru mkewe. Akasema, “Nataka kuingia chumbani kwa mke wangu.” Lakini baba yake huyo mwanamke hakumruhusu kuingia.
Baada ya siku kadhaa, wakati wa mavuno ya ngano, Samsoni akachukua mbuzi mdogo akaenda kumtembelea mkewe. Akajiambia mwenyewe, “Nitaenda kwenye chumba cha mke wangu.” Lakini baba yake hakumruhusu aingie.
2 Huyo baba mkwe wake akamwambia, “Nilikuwa na hakika kwamba ulimkataa, hivyo mimi nikampa rafiki yako. Je, mdogo wake wa kike si mzuri zaidi kuliko yeye? Mchukue huyo badala yake.”
Baba yake akasema, “Nilidhani umemchukia, hivyo nikampatia rafiki yako. Dada yake mdogo ni mzuri kuliko yeye, Mchukue badala yake.”
3 Samsoni akawaambia, “Wakati huu, nitakapowadhuru Wafilisti, sitakuwa na lawama.”
Samsoni akawaambia, 'Wakati huu sitakuwa na hatia juu ya Wafilisti wakati nikiwaumiza.'
4 Hivyo Samsoni akatoka akawakamata mbweha 300 na kuwafunga wawili wawili kwa mikia yao kila mmoja kwa mwingine. Kisha akafungia mwenge wa moto, kwenye mikia ya kila jozi moja ya mbweha aliyokuwa ameifunga,
Samsoni akaenda na kukamata mbweha mia tatu akawafunga pamoja kila jozi, mkia hadi mkia. Kisha akachukua taa na kuzifunga katikati ya kila mkia.
5 akawasha ile mienge na kuwaachia wale mbweha katika mashamba ya Wafilisti ya nafaka zilizosimamishwa katika matita. Akateketeza matita ya nafaka zilizosimama, pamoja na mashamba ya mizabibu na viunga vya mizeituni.
Alipokwisha kuviwasha moto vienge, akawaachia mbweha katika nafaka za Wafilisti zilizosimama, nao wakawasha moto nafaka zote zilizopandwa, na nafaka iliyosimama shambani, pamoja na mashamba ya mizabibu na mizeituni.
6 Ndipo Wafilisti wakauliza, “Ni nani aliyetenda jambo hili?” Wakaambiwa, “Ni Samsoni, yule mkwewe Mtimna, kwa sababu alimchukua mkewe akampa mwenzake.” Hivyo Wafilisti wakapanda wakamteketeza kwa moto yeye huyo mwanamke pamoja na baba yake.
Wafilisti waliuliza, “Ni nani aliyefanya hili?” Wakaambiwa, “Samsoni, mkwe wa Mtimna alifanya hivyo kwa sababu Mtimna alimchukua mke wa Samsoni akampa rafiki yake.” Basi Wafilisti wakamwendea wakamchoma kwa moto yeye na baba yake.
7 Samsoni akawaambia, “Kwa kuwa mmetenda hivyo, hakika sitatulia mpaka niwe nimelipiza kisasi juu yenu.”
Samsoni akawaambia, “Ikiwa ndivyo mnavyofanya, nitalipiza kisasi juu yenu, na baada ya hayo, nitaacha.”
8 Akawashambulia kwa ukali kwa mapigo makuu na kuwaua watu wengi sana. Kisha akateremka na kukaa katika ufa kwenye mwamba wa Etamu.
Kisha akawakata vipande vipande, paja na mguu, kwa kuwauwa sana. Kisha akashuka chini akaishi katika pango katika mwamba wa Etamu.
9 Wafilisti wakapanda na kupiga kambi huko Yuda na kuenea huko Lehi.
Ndipo Wafilisti wakaja, wakajitahidi kupigana vita huko Yuda, wakaanzisha jeshi lao huko Lehi.
10 Watu wa Yuda wakawauliza, “Kwa nini mmekuja kupigana nasi?” Wakawajibu, “Tumekuja ili kumkamata Samsoni na kumtenda kama alivyotutendea.”
Watu wa Yuda wakasema, “Kwa nini mmekuja kutupiga?” Wakasema, “Tunashambulia ili tuweze kumkamata Samsoni, na tumtendee kama alivyotutendea.”
11 Ndipo watu 3,000 toka Yuda walipoteremka na kwenda kwenye ufa wa mwamba huko Etamu, na kumwambia Samsoni, “Je, hujatambua kuwa Wafilisti wanatutawala? Ni nini hiki ulichotutendea?” Akawajibu, “Mimi nimewatendea tu kile walichonitendea.”
Kisha watu elfu tatu wa Yuda wakashuka hata kwenye pango la Eatamu, wakamwambia Samsoni, “Je, hujui kwamba Wafilisti hutawala juu yetu? Je! umetutendea nini?” Samsoni akawaambia, “Kwa kadili walivyonitendea mimi, vivyo hivyo nimewatendea wao.”
12 Wakamwambia, “Tumekuja kukufunga na kukutia mikononi mwa Wafilisti.” Samsoni akawaambia, “Niapieni kuwa hamtaniua ninyi wenyewe.”
Wakamwambia Samsoni, “Tumeshuka kukufunga na kukutia mikononi mwa Wafilisti.” Samsoni akawaambia, “Niapieni kwamba hamtaniua ninyi wenyewe.”
13 Wakamjibu, “Sisi hatutakuua, bali tutakufunga tu na kukutia mikononi mwao.” Basi wakamfunga kwa kamba mbili mpya. Wakamchukua toka huko kwenye ufa katika mwamba.
Wakamwambia, “La, tutakufunga tu kwa kamba na kukupeleka kwao. Tunakuahidi sisi hatutakuua.” Kisha wakamfunga na kamba mbili mpya na kumleta kutoka kwenye mwamba.
14 Alipokaribia Lehi, Wafilisti wakamjia wakipiga kelele. Roho wa Bwana akamjia juu yake kwa nguvu. Kamba zilizomfunga mikono yake zikawa kama kitani iliyochomwa kwa moto, na vifungo vyake vikaanguka chini toka mikononi mwake.
Alipofika Lehi, Wafilisti walipiga kelele walipokutana naye. Kisha Roho wa Bwana akaja juu yake kwa nguvu. Kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitambaa cha kuteketezwa, na zikaanguka mikononi mwake.
15 Ndipo akaona mfupa mpya wa taya la punda, akanyoosha mkono, akauchukua na kuua nao Wafilisti wapatao 1,000.
Samsoni alipata mfupa mbichi wa taya ya punda, naye akaichukua na kuua watu elfu kwa mfupa huo.
16 Ndipo Samsoni akasema, “Kwa taya la punda malundo juu ya malundo. Kwa taya la punda nimeua watu 1,000.”
Samsoni akasema, “Kwa taya ya punda, chungu juu ya chungu, na njaa ya punda nimewaua watu elfu.”
17 Alipomaliza kusema, akautupa ule mfupa wa taya; na mahali pale pakaitwa Ramath-Lehi.
Samsoni alipomaliza kuzungumza, akatupa taya, na akaita mahali pale Ramath Lehi.
18 Kwa kuwa alikuwa amesikia kiu sana, akamlilia Bwana akisema, “Umempa mtumishi wako ushindi huu mkuu. Je, sasa nife kwa kiu na kuangukia mikononi mwa hawa watu wasiotahiriwa?”
Samsoni alikuwa na kiu sana akamwita Bwana na kusema, “Umempa mtumishi wako ushindi mkubwa. Lakini sasa nitakufa kwa kiu na kuanguka mikononi mwa wale wasiootahiriwa?”
19 Bwana akafunua shimo huko Lehi, pakatoka maji. Samsoni alipoyanywa, nguvu zikamrudia na kuhuika. Hivyo chemchemi ile ikaitwa En-Hakore, nayo iko mpaka leo huko Lehi.
Na Mungu akapafungua mahali pa shimo palipo katika Lehi, na maji yakatoka. Alipokunywa, nguvu zake zikarejea na akahuishwa. Kwa hiyo aliita jina la mahali hapo Enhakore, na ni huko Lehi hadi leo.
20 Samsoni akawa mwamuzi wa Waisraeli katika siku za Wafilisti kwa muda wa miaka ishirini.
Samsoni alikuwa mwamuzi wa Israeli katika siku za Wafilisti kwa miaka ishirini.

< Waamuzi 15 >