< Waamuzi 12 >

1 Watu wa Efraimu wakaita majeshi yao, wakavuka kwenda Zafoni, wakamwambia Yefta, “Kwa nini mmekwenda kupigana na Waamoni bila kutuita ili twende pamoja nawe? Basi tutaichoma moto nyumba yako, pamoja nawe ukiwa ndani yake.”
Watu wa Efraimu walitoka pamoja; nao wakapitia Zafoni, wakamwambia Yeftha, Kwa nini umetangulia kupigana na wana wa Amoni, wala hukutuita twende pamoja nawe? Tutachoma nyumba yako.
2 Yefta akajibu, “Mimi na watu wangu tulikuwa na ugomvi mkubwa na Waamoni, hata ingawa niliwaita hamkuniokoa katika mkono wao.
Yeftha akawaambia, Mimi na watu wangu tulikuwa katika vita kubwa na wana wa Amoni. Nilipokuita, hukuniokoa kutoka kwao.
3 Nilipoona kuwa hamkunipa msaada nikauhatarisha uhai wangu na nikavuka kupigana na Waamoni. Naye Bwana akanipatia ushindi dhidi yao. Sasa kwa nini mnanijia leo ili kupigana nami?”
Nilipoona ya kuwa hamkuniokoa, nikaweka uhai wangu na nguvu yangu mwenyewe, na kupita kipita ili kupigana na wana wa Amoni, na Bwana alinipa ushindi. Kwa nini mmekuja kupigana nami leo?”
4 Ndipo Yefta akakusanya watu wa Gileadi pamoja na kupigana na Efraimu. Wagileadi wakawashinda Efraimu, kwa kuwa Waefraimu walisema, “Ninyi Wagileadi ni watoro mliotoroka toka Efraimu na Manase.”
Yeftha akawakusanya watu wote wa Gileadi na akapigana na Efraimu. Watu wa Gileadi waliwaangamiza wana wa Efraimu kwa sababu walisema, “Ninyi Wagileadi ni wakimbizi katika Efraimu-katika Efraimu na Manase.”
5 Wagileadi wakaviteka vivuko vya Yordani dhidi ya hao Waefraimu, kisha ilikuwa yeyote yule aliyenusurika katika Efraimu aliposema, “Niache nivuke,” hao watu wa Gileadi walimuuliza, “Je wewe ni Mwefraimu?” Kama alijibu “Hapana,”
Wagileadi waliteketeza ngome za Yordani zinaelekea Efraimu. Ikiwa yeyote kati ya waliopona wa Efraimu akisema, Nipe ruhusa niende juu ya mto; watu wa Gileadi wakamwambia, “Je, wewe ni Mwefraimu?” Ikiwa akasema, “Hapana,”
6 walimwambia, “Sawa, sema ‘Shibolethi.’” Iwapo alitamka, “Sibolethi,” kwa sababu hakuweza kutamka hilo neno sawasawa, walimkamata na kumuua hapo kwenye vivuko vya Yordani. Waefraimu 42,000 waliuawa wakati huo.
basi watamwambia, Sema Shiboleth. Na kama akisema 'Sibboleth' (kwa maana hakuweza kutamka neno hilo kwa usahihi), Wagileadi watamkamata na kumwua kwenye mabwawa ya Yordani. Waefraimu elfu arobaini waliuawa wakati huo.
7 Yefta akawa mwamuzi wa Waisraeli kwa muda wa miaka sita. Basi Yefta akafa, akazikwa katika mmojawapo wa miji ya Gileadi.
Yeftha alikuwa mwamuzi juu ya Israeli kwa miaka sita. Ndipo Yeftha Mgileadi akafa, akazikwa katika moja ya miji ya Gileadi.
8 Baada yake, Ibzani wa Bethlehemu akawa mwamuzi wa Israeli.
Baada yake, Ibzani wa Bethlehemu akawa mwamuzi juu ya Israeli.
9 Alikuwa na wana thelathini na binti thelathini. Akawaoza binti zake kwa watu wengine nje ya ukoo wake, na kuwatwalia wanawe wanawake thelathini toka nje ya ukoo wake. Ibzani akawa mwamuzi wa Israeli kwa muda wa miaka saba.
Alikuwa na wana thelathini. Aliwapeleka binti thelathini katika ndoa, naye akaleta binti thelathini kutoka nje kwa ajili ya wanawe, Alikuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka saba.
10 Ibzani akafa, akazikwa huko Bethlehemu.
Ibzani alikufa na kuzikwa huko Bethlehemu.
11 Baada yake Eloni, Mzabuloni, akawa mwamuzi wa Israeli, naye akawaamua kwa muda wa miaka kumi.
Baada yake, Eloni wa Zabuloni akawa mwamuzi juu ya Israeli. Akawaamua Israeli kwa miaka kumi.
12 Kisha Eloni akafa, akazikwa katika Aiyaloni, katika nchi ya Zabuloni.
Eloni wa Zabuloni akafa, akazikwa huko Aiyaloni katika nchi ya Zabuloni.
13 Baada yake, Abdoni mwana wa Hileli, Mpirathoni, akawa mwamuzi wa Israeli.
Baada ya huyo, Abdoni mwana wa Hileli, Mpirathoni, akawa mwamuzi juu ya Israeli.
14 Naye akazaa wana arobaini na wana wa wanawe thelathini waliopanda punda sabini. Akawa mwamuzi wa Israeli kwa muda wa miaka minane.
Alikuwa na wana arobaini na wajukuu thelathini. Walikuwa wakipanda punda sabini, naye akawaamua Israeli kwa miaka nane.
15 Ndipo Abdoni mwana wa Hileli, Mpirathoni, akafa, naye akazikwa huko Pirathoni katika Efraimu, katika nchi ya vilima ya Waamaleki.
Abdoni mwana wa Hileli, Mpirathoni, akafa, akazikwa huko Pirathoni katika nchi ya Efraimu, katika kilima cha Waamaleki.

< Waamuzi 12 >