< Yoshua 9 >

1 Basi ikawa wafalme wote waliokuwa magharibi mwa Yordani waliposikia juu ya haya yote, wale waliokuwa katika nchi ya vilima, upande wa magharibi mwa vilima na katika pwani yote ya hiyo Bahari Kuu, hadi kufikia Lebanoni (wafalme wa Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi),
Kisha wafalme wote walioishi ng'ambo ya mto Yordani katika nchi ya milima, na katika nchi za chini katika pwani za Bahari Kuu mbele ya Lebanoni - Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi -
2 wakajiunga pamoja ili kupigana vita dhidi ya Yoshua na Israeli.
hawa waliungana pamoja chini ya amri moja kuinua vita dhidi ya Yoshua na Israeli.
3 Hata hivyo, watu wa Gibeoni waliposikia juu ya hayo yote Yoshua aliyowatendea watu wa Yeriko na Ai,
Waliposikia wenyeji wa Gibeoni juu ya mambo aliyoyafanya Yoshua katika Yeriko na Ai,
4 nao wakaamua kufanya hila: Wakajifanya kama wajumbe wakiwa na punda waliobebeshwa mizigo wakiwa na magunia yaliyochakaa na viriba vya mvinyo vikuukuu vyenye nyufa zilizozibwa.
walipanga mpango wa udanganyifu. Walienda kama wajumbe. Walichukua magunia yaliyochakaa na kuyaweka juu ya punda. Walichukua pia viriba vilivyochakaa na kuchanika chanika na vilivyozibwa zibwa.
5 Walivaa miguuni mwao viatu vilivyoraruka na kushonwa kisha wakavaa nguo kuukuu. Chakula chao kilikuwa mkate uliokauka na kuingia koga.
Walivaa miguuni mwao viatu vilivyozeeka na kutoboka toboka, na walivaa nguo kuukuu, zilichanika chanika. Na mikate yote katika chombo ilikuwa mikavu na yenye uvundo.
6 Ndipo wakamwendea Yoshua kambini huko Gilgali wakamwambia yeye pamoja na watu wa Israeli, “Tumetoka katika nchi ya mbali, fanyeni mkataba nasi.”
Kisha wakamwendea Yoshua katika kambi huko Giligali na wakamwambia yeye pamoja wa watu wa Israeli wakisema, “
7 Basi watu wa Israeli wakawaambia hao Wahivi, “Lakini huenda mnakaa karibu nasi, twawezaje basi kufanya mapatano nanyi?”
Tumesafiri kutoka nchi ya mbali, basi fanyeni agano nasi.” Watu wa Israeli wakawaamba Wahivi, “Huenda mnaishi karibu nasi. Twawezeje kufanya agano nanyi?”
8 Wakamwambia Yoshua, “Sisi ni watumishi wako.” Yoshua akawauliza, “Ninyi ni nani, nanyi mnatoka wapi?”
Wakamwambia Yoshua, “Sisi ni watumishi wako.”Yoshua akawauliza, “Ninyi ni akina nani? Mnatokea wapi?
9 Nao wakamjibu: “Watumishi wako wametoka nchi ya mbali sana kwa ajili ya umaarufu wa Bwana Mungu wenu. Kwa kuwa tumesikia taarifa zake: hayo yote aliyofanya huko Misri,
Wakamwambia, “Watumishi wako wamekuja hapa kutokea nchi ya mbali, kwasababu ya jina la Yahweh Mungu wako. Tumesikia habari kumhusu na kuhusu kila kitu alichokifanya Misri -
10 pia yale yote aliyowatendea wafalme wawili wa Waamori mashariki ya Yordani; huyo Sihoni mfalme wa Heshboni na Ogu mfalme wa Bashani, aliyetawala huko Ashtarothi.
na kila kitu alichokifanya kwa wafalme wawili wa Waamori katika upande mwingine wa Yordani - kwa mfalme Sihoni wa Heshiboni, na kwa Ogu wa Bashani aliyekuwa katika Ashitarothi.
11 Basi wazee wetu na wale wote wanaoishi katika nchi yetu walituambia, ‘Chukueni chakula cha safari; nendeni mkakutane na watu hao na kuwaambia, “Sisi tu watumishi wenu, fanyeni mapatano nasi.”’
Wazee wetu na wenyeji wote wa nchi yetu walituambia,” Chukueni chakula mikononi mwenu kwa ajili ya safari. Nendeni mkakutane nao, na kisha muwambie, “Sisi ni watumishi wenu. Fanyeni agano pamoja nasi.”
12 Mkate huu wetu ulikuwa wa moto tulipoufunga siku tulipoanza safari kuja kwenu, lakini sasa angalia jinsi ulivyokauka na kuota ukungu.
Huu ni mkate wetu, ulikuwa wa moto tulipouchukua kutoka katika nyumba zetu katika siku ile tulipotoka kuja kwenu. Lakini sasa, tazama, imekuwa kavu na yenye ukungu.
13 Viriba hivi vya mvinyo vilikuwa vipya tulipovijaza, lakini ona jinsi vilivyo na nyufa. Nguo zetu na viatu vimechakaa kwa ajili ya safari ndefu.”
Viriba hivi vilikuwa vipya tulipovijaza, na tazama, sasa vinavuja. Nguo zetu na viatu vyetu vimechakaa na kuwa vikuukuu kwasababu ya safari ndefu.”
14 Basi watu wa Israeli wakavikagua vyakula vyao bila kupata shauri kutoka kwa Bwana.
kwahiyo, Waisraeli wakatwaa sehemu ya vyakula vyao, lakini walifanya hivyo bila ya kumwuliza Yahweh ili awaongoze.
15 Ndipo Yoshua akafanya mapatano ya amani pamoja nao kuwaacha waishi, nao viongozi wa kusanyiko wakathibitisha kwa kiapo.
Yoshua akafanya amani pamoja nao na kufanya agano pamoja nao ili waishi. Viongozi wa watu nao pia wakawaapia.
16 Siku ya tatu baada ya hao kufanya mapatano na Wagibeoni, Waisraeli wakapata habari kuwa hao watu ni jirani zao waliokuwa wanaishi karibu nao.
Siku tatu baada ya Waisraeli kufanya agano pamoja nao, waligundua kuwa walikuwa ni majirani zao na ya kwamba waliishi karibu nao.
17 Ndipo wana wa Israeli wakasafiri na siku ya tatu wakafika kwenye miji yao ya Gibeoni, Kefira, Beerothi na Kiriath-Yearimu.
Kisha watu wa Israeli walisafiri na kufika katika miji yao katika siku ya tatu. Miji yao ilikuwa Gibeoni, Kefira, Beerothi, na Kiriathi Yearimu.
18 Lakini Waisraeli hawakuwashambulia kwa kuwa viongozi wa kusanyiko walikuwa wamewaapia kwa Bwana, Mungu wa Israeli. Kusanyiko lote likanungʼunika dhidi ya hao viongozi,
Watu wa Israeli wahakushambulia kwasababu viongozi wao walikuwa wamewaapia mbele za Yahweh, Mungu wa Israeli. Waisraeli wote walikuwa wananung'unika kinyume na viongozi wao.
19 lakini viongozi wote wakawajibu, “Tumeshawaapia kwa Bwana, Mungu wa Israeli, kwa hiyo hatuwezi kuwagusa sasa.
Lakini viongozi wote waliawaambia watu wote wa Israeli, “Tumeapa kwa Yahweh, Mungu wa Israeli kwa ajili yao, na sasa hatuwezi kuwadhuru.
20 Hivi ndivyo tutakavyowafanyia: Tutawaacha waishi, ili ghadhabu isije juu yetu kwa kuvunja kiapo tulichowaapia.”
Hiki ndicho tutakachowafanyia: Tutawaacha waishi ili tuepuke ghadhabu ambayo yaweza kuja juu yetu kwasababu ya kiapo tulichowaapia.”
21 Wakaendelea kusema, “Waacheni waishi, lakini wawe wapasua kuni na wachota maji kwa ajili ya jamii yote.” Hivyo ahadi waliyoweka viongozi kwao ikawa hivyo.
Viongozi wakawaambia watu, “Waacheni waishi.” Hivyo Wagibeoni wakawa wakata kuni na wachota maji wa Waisraeli wote, kama vile viongozi walivyosema juu yao.
22 Kisha Yoshua akawaita Wagibeoni na kuwaambia, “Kwa nini mmetudanganya kwa kutuambia, ‘Tunaishi mbali nanyi,’ wakati ambapo ninyi mnaishi karibu nasi?
Yoshua aliwaita na kuwaambia, “Kwanini mlitudanya wakati mliposema, “Tuko mbali sana nanyi' wakati mnaishi hapa hapa miongoni mwetu?
23 Sasa mko chini ya laana: Daima mtakuwa wapasua kuni na wachota maji kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu.”
Na kwasababu hii, mmelaaniwa na baadhi yenu mtakuwa watumwa siku zote, wenye kukata kuni na kuchota maji kwa ajli ya nyumba ya Mungu wangu.”
24 Wakamjibu Yoshua, “Watumwa wako waliambiwa waziwazi jinsi Bwana Mungu wenu alivyomwamuru mtumishi wake Mose kuwapa ninyi nchi hii yote na kuwaangamiza wakazi wake wote toka mbele zenu. Kwa hiyo tuliogopa mno kwa ajili ya uhai wetu kwa sababu yenu, ndiyo maana tukafanya neno hili.
Walimjibu Yoshua na kusema, “Ni kwasababu watumishi wako waliambiwa kwamba Yahweh Mungu wenu alimwagiza Musa mtumishi wake kuwapa ninyi nchi yote, na kuwateteza wenyeji wote wa nchi mbele yenu - hivyo tuliogopa kwasababu yenu kwa ajili ya maisha yetu. Ndio maana tulifanya jambo hili.
25 Sasa tupo mikononi mwako. Tufanyieni lolote mnaloona kuwa jema na haki kwako.”
Tazama sasa, mnatumiliki chini ya utawala wenu. Chochote kilichochema na haki kwenu kutufanyia, fanyeni.”
26 Kwa hiyo Yoshua akawaokoa mikononi mwa Waisraeli, nao hawakuuawa.
Basi Yoshua aliwafanyia hivi: aliwaondoa katika mamlaka ya watu wa Israeli, na Waisraeli hawakuwaua.
27 Siku hiyo Yoshua akawafanya Wagibeoni wapasua kuni na wachota maji kwa ajili ya jamii na kwa ajili ya madhabahu ya Bwana mahali pale ambapo Bwana angepachagua. Hivyo ndivyo walivyo hadi hivi leo.
Siku hiyo Yoshua aliwafanya Wagibeoni kuwa wakata kuni na wachotaji wa maji kwa jamii, na kwa madhabahu ya Yahweh hadi leo katika sehemu ambayo Yahweh huichagua.

< Yoshua 9 >