< Yoshua 4 >

1 Wakati taifa lote lilipokwisha kuvuka Mto Yordani, Bwana akamwambia Yoshua,
Watu wote walipokwisha kuvuka Yordani, Yahweh akamwambia Yoshua,
2 “Chagua watu kumi na wawili miongoni mwa watu, kila kabila mtu mmoja,
“Chagueni wenyewe watu waume kumi na wawili, mmoja katika kila kabila.
3 nawe uwaambie wachukue mawe kumi na mawili katikati ya Mto Yordani, palepale makuhani waliposimama, wayachukue na kuyaweka mahali mtakapokaa usiku huu wa leo.”
Wape agizo hilo: 'Chukueni mawe kumi na mbili kutoka katikati ya Yordani mahali wanaposimama makuhani katika nchi kavu, na wayalete na kuyaweka chini katika sehemu ambapo mtalala usiku wa leo.
4 Basi Yoshua akawaita watu kumi na wawili ambao alikuwa amewachagua kutoka miongoni mwa Waisraeli, mtu mmoja kutoka kila kabila,
Kisha Yoshua akawaita wanaume kumi na wawili ambao aliwachagua kutoka katika makabila ya Israeli, mmoja kutoka kila kabila.
5 naye akawaambia, “Mtangulie mbele ya Sanduku la Bwana Mungu wenu, mwende katikati ya Mto Yordani. Kila mmoja wenu atainua jiwe begani mwake, kufuatana na hesabu ya makabila ya Waisraeli,
Yoshua akawaambia, “Nendeni mbele za sanduku la Yahweh Mungu wenu katikati ya Yordani. Kila mmoja wenu achukue jiwe moja mabegani mwake, kulingana na hesabu ya makabila ya watu wa Israeli.
6 kuwa kama ishara katikati yenu. Siku zijazo, wakati watoto wenu watakapowauliza, ‘Ni nini maana ya mawe haya?’
Hii itakuwa ni ishara miongoni mwenu kwa ajili yenu wakati watoto wenu watakapowauliza katika siku zijazo, 'Nini maana ya mawe haya kwenu?'
7 waambieni kwamba maji ya Mto Yordani yaliyokuwa yakitiririka yalitindika mbele ya Sanduku la Agano la Bwana. Wakati lilipovuka Yordani, maji ya Yordani yalitindika. Mawe haya yatakuwa kumbukumbu kwa watu wa Israeli milele.”
Ndipo mtakapowaambia, 'Maji ya Yordani yalitengwa mbele ya sanduku la Yahweh. Lililpopitishwa katika Yordani, maji ya Yordani yalisimamishwa. Hivyo, mawe haya yatakuwa kumbukumbu kwa watu wa Israeli milele.'”
8 Hivyo Waisraeli wakafanya kama Yoshua alivyowaagiza. Wakachukua mawe kumi na mawili kutoka katikati ya Mto Yordani, kulingana na hesabu ya kabila za Waisraeli kama Bwana alivyomwambia Yoshua, nao wakayabeba hadi kambini mwao, mahali walipoyatua chini.
Watu waisraeli walifanya kama Yoshua alivyowaagiza, na walichukua mawe kumi na mbili kutoka katikati ya Yordani, kama Yahweh alivyomwambia Yoshua, walipangwa sawa sawa na hesabu ya makabila ya watu wa Israeli. Waliyachukua mawe mpaka mahali walipolala na wakayaweka chini huko.
9 Yoshua akayasimamisha yale mawe kumi na mawili ambayo yalikuwa katikati ya Mto Yordani, mahali pale ambapo miguu ya makuhani waliobeba Sanduku la Agano iliposimama. Nayo yako huko mpaka leo.
Kisha Yoshua akayapanga mawe kumi na mbili katikati ya Yordani, katika sehemu ambapo ilisimama miguu ya makuhani waliolichukua sanduku la agano. Na kumbukumbu hiyo ipo hadi leo.
10 Makuhani waliobeba lile Sanduku walibakia wakiwa wamesimama katikati ya Mto Yordani mpaka kila kitu Bwana alichomwamuru Yoshua kilipokuwa kimefanywa na watu, sawasawa na vile Mose alivyokuwa amemwamuru Yoshua. Watu wakafanya haraka kuvuka,
Makuhani waliolichukua sanduku walisimama katikati ya Yordani mpaka pale kila kitu ambacho Yahweh alimwamuru Yoshua kuwaambia watu kilipokamilika, sawa sawa na yote ambayo Musa alimwagiza Yoshua. Watu walifanya haraka na wakavuka.
11 na mara tu watu wote walipokwisha kuvuka, Sanduku la Bwana na makuhani wakavuka watu wakiwa wanatazama.
Wakati watu wote walipokwisha kuvuka, sanduku la Yahweh pamoja na makuhani walivuka mbele za watu.
12 Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase wakavuka mbele ya Waisraeli, wakiwa wamevaa silaha, kama Mose alivyowaamuru.
Kabila la Rubeni, kabila la Gadi, na nusu ya kabila la Manase walipita kama jeshi mbele ya watu wa Israeli, kama ambavyo Musa alivyowaambia.
13 Kiasi cha watu 40,000 waliojiandaa kwa vita walivuka mbele za Bwana hadi nchi tambarare za Yeriko kwa ajili ya vita.
Yapata watu watu elfu arobaini walioandaliwa kwa vita walipita mbele za Yahweh, kwa ajili ya vita katika uwanda wa Yeriko.
14 Siku ile Bwana akamtukuza Yoshua mbele ya Israeli yote, nao wakamheshimu siku zote za maisha yake, kama vile walivyomheshimu Mose.
Katika siku hiyo Yahweh alimfanya Yoshua kuwa mkuu katika macho ya watu wote wa Israeli. Walimheshimu - kama walivyomheshimu Musa - siku zake zote.
15 Basi Bwana akamwambia Yoshua,
Kisha Yahweh akamwambia Yoshua,
16 “Waamuru hao makuhani wanaolibeba Sanduku la Ushuhuda, wapande kutoka ndani ya Mto Yordani.”
“Waamuru makuhani wanaolibeba sanduku la ushuhuda watoke katika Yordani.”
17 Kwa hiyo Yoshua akawaamuru hao makuhani akisema, “Pandeni kutoka ndani ya Mto Yordani.”
Hivyo Yoshua akawaamuru makuhani, '' pandeni mtoke Yordani.”
18 Nao makuhani wakapanda kutoka ndani ya Mto Yordani wakilibeba hilo Sanduku la Agano la Bwana. Mara tu walipoiweka miguu yao penye kingo, nje ya mto, maji ya Yordani yakarudi kufurika kama ilivyokuwa kabla.
Wakati makuhani wenye kulibeba sanduku la agano la Yahweh walitoka katikati ya Yordani, na nyayo za miguu yao ilikuwa imeinuliwa katika nchi kavu, kisha maji ya Yordani yalirudi katika sehemu zake na kujaa hadi katika kingo zake kama ilivyokuwa siku nne zilizopita.
19 Siku ya kumi ya mwezi wa kwanza watu walipanda kutoka Yordani na kupiga kambi huko Gilgali, kwenye mpaka wa mashariki ya Yeriko.
Katika siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, watu walikwea kutoka Yordani. Wakakaa huko Gilgali, mashariki mwa Yeriko.
20 Naye Yoshua akayasimamisha huko Gilgali yale mawe kumi na mawili ambayo walikuwa wameyachukua katikati ya Mto Yordani.
Mawe kumi na mawili ambayo yalichukuliwa katika Yordani, Yoshuua aliyasimamisha hapo Gilgali.
21 Akawaambia Waisraeli, “Wazao wenu watakapowauliza baba zao siku zijazo wakisema, ‘Mawe haya maana yake ni nini?’
Aliwaambia watu wa Israeli, “wakati watoto wenu watakapowauliza baba zao katika wakai ujao, 'Mawe haya ni ya nini?'
22 Basi waambieni, ‘Israeli ilivukia mahali pakavu katika Mto Yordani.’
Waambieni watoto wenu, 'Hapa ndipo Waisraeli walivuka Yordani katika nchi kavu.
23 Kwa maana Bwana Mungu wenu alikausha maji ya Yordani mbele yenu, hadi mlipomaliza kuvuka. Bwana Mungu wenu alifanya haya kwa Mto Yordani sawasawa na kile alichoifanyia Bahari ya Shamu wakati alipoikausha mbele yetu hadi tulipomaliza kuvuka.
Yahweh Mungu wenu aliyakausha maji ya Yordani, mpaka hapo Yahweh Mungu wako aliyoyafanya katika bahari ya mianzi, ambayo aliikausha kwa ajili yetu ili tupite juu yakes,
24 Alifanya hivi ili kwamba mataifa yote ya dunia yapate kujua kuwa mkono wa Bwana ni wenye nguvu, na ili kwamba kila wakati mpate kumcha Bwana Mungu wenu.”
ili kwamba watu wote wa nchi wajue kwamba mkono wa Yahweh ni nguvu, na kwamba mtamweshimu Yahweh Mungu wenu milele.''

< Yoshua 4 >