< Yoshua 21 >

1 Basi viongozi wa jamaa ya Walawi, wakamwendea kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa jamaa nyingine za makabila ya Israeli
Les chefs de famille des Lévites s’approchèrent du sacrificateur Éléazar, de Josué, fils de Nun, et des chefs de famille des tribus des enfants d’Israël.
2 huko Shilo katika Kanaani na kuwaambia, “Bwana aliamuru kupitia Mose kuwa mtupe miji ya kuishi yenye sehemu za malisho kwa mifugo yetu.”
Ils leur parlèrent à Silo, dans le pays de Canaan, et dirent: L’Éternel a ordonné par Moïse qu’on nous donnât des villes pour habitation, et leurs banlieues pour notre bétail.
3 Hivyo kama vile Bwana alivyoamuru, Waisraeli wakawapa Walawi miji ifuatayo pamoja na sehemu zake za malisho kutoka urithi wao wenyewe.
Les enfants d’Israël donnèrent alors aux Lévites, sur leur héritage, les villes suivantes et leurs banlieues, d’après l’ordre de l’Éternel.
4 Kura ya kwanza ikaangukia Wakohathi, ukoo kwa ukoo. Walawi waliokuwa wazao wa kuhani Aroni walipewa miji kumi na mitatu kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini.
On tira le sort pour les familles des Kehathites; et les Lévites, fils du sacrificateur Aaron, eurent par le sort treize villes de la tribu de Juda, de la tribu de Siméon et de la tribu de Benjamin;
5 Wazao wengine waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za makabila ya Efraimu, Dani na nusu ya Manase.
les autres fils de Kehath eurent par le sort dix villes des familles de la tribu d’Éphraïm, de la tribu de Dan et de la demi-tribu de Manassé.
6 Wazao wa Gershoni walipewa miji kumi na mitatu kutoka koo za makabila ya Isakari, Asheri, Naftali na nusu ya Manase huko Bashani.
Les fils de Guerschon eurent par le sort treize villes des familles de la tribu d’Issacar, de la tribu d’Aser, de la tribu de Nephthali et de la demi-tribu de Manassé en Basan.
7 Wazao wa Merari, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na miwili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni.
Les fils de Merari, selon leurs familles, eurent douze villes de la tribu de Ruben, de la tribu de Gad et de la tribu de Zabulon.
8 Kwa hiyo Waisraeli wakawapa Walawi miji hii pamoja na sehemu zake za malisho, kama vile Bwana alivyokuwa ameamuru kupitia kwa Mose.
Les enfants d’Israël donnèrent aux Lévites, par le sort, ces villes et leurs banlieues, comme l’Éternel l’avait ordonné par Moïse.
9 Kutoka makabila ya Yuda na Simeoni waligawa miji ifuatayo kwa majina
Ils donnèrent de la tribu des fils de Juda et de la tribu des fils de Siméon les villes qui vont être nominativement désignées,
10 (miji hii walipewa wazao wa Aroni ambao walitokana na koo za Wakohathi wa Walawi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia):
et qui furent pour les fils d’Aaron d’entre les familles des Kehathites et des fils de Lévi, car le sort les avait indiqués les premiers.
11 Waliwapa Kiriath-Arba (yaani Hebroni), pamoja na sehemu zake za malisho zilizoizunguka, katika nchi ya vilima ya Yuda. (Arba alikuwa baba wa Anaki.)
Ils leur donnèrent Kirjath-Arba, qui est Hébron, dans la montagne de Juda, et la banlieue qui l’entoure: Arba était le père d’Anak.
12 Lakini mashamba na vijiji vilivyozunguka mji mkubwa walikuwa wamempa Kalebu mwana wa Yefune kuwa milki yake.
Le territoire de la ville et ses villages furent accordés à Caleb, fils de Jephunné, pour sa possession.
13 Kwa hiyo wazao wa kuhani Aroni wakapewa Hebroni (mji mkuu wa makimbilio kwa ajili ya yeyote aliyeshtakiwa kwa mauaji), Libna,
Ils donnèrent donc aux fils du sacrificateur Aaron la ville de refuge pour les meurtriers, Hébron et sa banlieue, Libna et sa banlieue,
14 Yatiri, Eshtemoa,
Jatthir et sa banlieue, Eschthemoa et sa banlieue,
15 Holoni, Debiri,
Holon et sa banlieue, Debir et sa banlieue,
16 Aini, Yuta na Beth-Shemeshi, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji tisa kutoka kwa makabila haya mawili.
Aïn et sa banlieue, Jutta et sa banlieue, et Beth-Schémesch et sa banlieue, neuf villes de ces deux tribus;
17 Kutoka kabila la Benyamini wakawapa Gibeoni, Geba,
et de la tribu de Benjamin, Gabaon et sa banlieue, Guéba et sa banlieue,
18 Anathothi na Almoni, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne.
Anathoth et sa banlieue, et Almon et sa banlieue, quatre villes.
19 Miji yote waliyopewa makuhani, wazao wa Aroni, ilikuwa kumi na mitatu, pamoja na sehemu zake za malisho.
Total des villes des sacrificateurs, fils d’Aaron: treize villes, et leurs banlieues.
20 Koo nyingine za Wakohathi, ambao pia ni Walawi, walipewa miji kutoka kabila la Efraimu:
Les Lévites appartenant aux familles des autres fils de Kehath eurent par le sort des villes de la tribu d’Éphraïm.
21 Katika nchi ya vilima ya Efraimu walipewa Shekemu (mji mkubwa wa makimbilio kwa yeyote anayeshtakiwa kwa mauaji) na Gezeri,
On leur donna la ville de refuge pour les meurtriers, Sichem et sa banlieue, dans la montagne d’Éphraïm, Guézer et sa banlieue,
22 Kibsaimu na Beth-Horoni, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne.
Kibtsaïm et sa banlieue, et Beth-Horon et sa banlieue, quatre villes;
23 Pia kutoka kabila la Dani wakapokea Elteke, Gibethoni,
de la tribu de Dan, Eltheké et sa banlieue, Guibbethon et sa banlieue,
24 Aiyaloni na Gath-Rimoni pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne
Ajalon et sa banlieue, et Gath-Rimmon et sa banlieue, quatre villes;
25 Kutoka nusu ya kabila la Manase, wakapokea Taanaki na Gath-Rimoni pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji miwili.
et de la demi-tribu de Manassé, Thaanac et sa banlieue, et Gath-Rimmon et sa banlieue, deux villes.
26 Miji yote hii kumi pamoja na sehemu zake za malisho ilipewa koo za Wakohathi zilizobaki.
Total des villes: dix, et leurs banlieues, pour les familles des autres fils de Kehath.
27 Koo za Walawi za Wagershoni walipewa: kutoka nusu ya kabila la Manase, Golani katika Bashani (mji mkuu wa makimbilio kwa yeyote aliyeshtakiwa kwa mauaji) na Beeshtera, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji miwili;
On donna aux fils de Guerschon, d’entre les familles des Lévites: de la demi-tribu de Manassé, la ville de refuge pour les meurtriers, Golan en Basan et sa banlieue, et Beeschthra et sa banlieue, deux villes;
28 kutoka kabila la Isakari walipewa, Kishioni, Daberathi,
de la tribu d’Issacar, Kischjon et sa banlieue, Dabrath et sa banlieue,
29 Yarmuthi na En-Ganimu, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne
Jarmuth et sa banlieue, et En-Gannim et sa banlieue, quatre villes;
30 kutoka kabila la Asheri walipewa, Mishali, Abdoni,
de la tribu d’Aser, Mischeal et sa banlieue, Abdon et sa banlieue,
31 Helkathi na Rehobu, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne.
Helkath et sa banlieue, et Rehob et sa banlieue, quatre villes;
32 Kutoka kabila la Naftali walipewa, Kedeshi katika Galilaya (mji wa makimbilio kwa ajili ya yeyote anayeshtakiwa kwa mauaji), Hamoth-Dori na Kartani, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji mitano.
et de la tribu de Nephthali, la ville de refuge pour les meurtriers, Kédesch en Galilée et sa banlieue, Hammoth-Dor et sa banlieue, et Karthan et sa banlieue, trois villes.
33 Miji yote ya koo za Wagershoni ilikuwa kumi na mitatu, pamoja na sehemu zake za malisho.
Total des villes des Guerschonites, selon leurs familles: treize villes et leurs banlieues.
34 Koo za Wamerari (Walawi waliobaki) walipewa: kutoka kabila la Zabuloni, Yokneamu, Karta,
On donna au reste des Lévites, qui appartenaient aux familles des fils de Merari: de la tribu de Zabulon, Jokneam et sa banlieue, Kartha et sa banlieue,
35 Dimna na Nahalali, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne;
Dimna et sa banlieue, et Nahalal et sa banlieue, quatre villes;
36 kutoka kabila la Reubeni walipewa Bezeri, Yahasa,
de la tribu de Ruben, Betser et sa banlieue, Jahtsa et sa banlieue,
37 Kedemothi na Mefaathi, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne;
Kedémoth et sa banlieue, et Méphaath et sa banlieue, quatre villes;
38 kutoka kabila la Gadi walipewa, Ramothi katika Gileadi (mji wa makimbilio kwa ajili ya yeyote anayeshtakiwa kwa ajili ya mauaji), Mahanaimu,
et de la tribu de Gad, la ville de refuge pour les meurtriers, Ramoth en Galaad et sa banlieue, Mahanaïm et sa banlieue,
39 Heshboni na Yazeri, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne.
Hesbon et sa banlieue, et Jaezer et sa banlieue, en tout quatre villes.
40 Miji yote waliyopewa koo za Wamerari, waliokuwa mabaki ya Walawi, ilikuwa ni kumi na miwili.
Total des villes qui échurent par le sort aux fils de Merari, selon leurs familles, formant le reste des familles des Lévites: douze villes.
41 Miji yote ya Walawi katika eneo lililoshikwa na Waisraeli lilikuwa arobaini na minane, pamoja na sehemu zake za malisho.
Total des villes des Lévites au milieu des propriétés des enfants d’Israël: quarante-huit villes, et leurs banlieues.
42 Kila mmoja wa miji hii ulikuwa na sehemu ya malisho kuuzunguka; ndivyo ilivyokuwa kwa miji hii yote.
Chacune de ces villes avait sa banlieue qui l’entourait; il en était de même pour toutes ces villes.
43 Kwa hiyo Bwana akawapa Israeli nchi yote aliyokuwa ameapa kuwapa baba zao, nao wakaimiliki na kukaa humo.
C’est ainsi que l’Éternel donna à Israël tout le pays qu’il avait juré de donner à leurs pères; ils en prirent possession et s’y établirent.
44 Bwana akawapa pumziko kila upande, kama vile alivyokuwa amewaapia baba zao, hakuna hata mmoja wa adui zao aliyeweza kusimama mbele yao, Bwana akawatia adui zao wote mikononi mwao.
L’Éternel leur accorda du repos tout alentour, comme il l’avait juré à leurs pères; aucun de leurs ennemis ne put leur résister, et l’Éternel les livra tous entre leurs mains.
45 Hakuna hata mojawapo ya ahadi nzuri ya Bwana kwa nyumba ya Israeli ambayo haikutimia; kila moja ilitimia.
De toutes les bonnes paroles que l’Éternel avait dites à la maison d’Israël, aucune ne resta sans effet: toutes s’accomplirent.

< Yoshua 21 >