< Yoshua 19 >
1 Kura ya pili ikaangukia kabila la Simeoni, ukoo kwa ukoo. Urithi wao ulikuwa ndani ya eneo la Yuda.
为西缅支派的人,按着宗族,拈出第二阄。他们所得的地业是在犹大人地业中间。
2 Ulijumuisha: Beer-Sheba (au Sheba), Molada,
他们所得为业之地就是:别是巴(或名示巴)、摩拉大、
3 Hasar-Shuali, Bala, Esemu,
哈萨·书亚、巴拉、以森、
4 Eltoladi, Bethuli, Horma,
伊利多拉、比土力、何珥玛、
5 Siklagi, Beth-Markabothi, Hasar-Susa,
洗革拉、伯·玛加博、哈萨·苏撒、
6 Beth-Lebaothi na Sharuheni; hii ilikuwa miji kumi na mitatu pamoja na vijiji vyake.
伯·利巴勿、沙鲁险,共十三座城,还有属城的村庄;
7 Pia Aini, Rimoni, Etheri, na Ashani; hii ilikuwa miji minne na vijiji vyake,
又有亚因、利门、以帖、亚珊,共四座城,还有属城的村庄;
8 pamoja na vijiji vyote vinavyoizunguka miji hii mpaka Baalath-Beeri (ambayo ndiyo Rama iliyo katika Negebu). Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Simeoni ukoo kwa ukoo.
并有这些城邑四围一切的村庄,直到巴拉·比珥,就是南地的拉玛。这是西缅支派按着宗族所得的地业。
9 Urithi wa Wasimeoni ulitolewa kutoka fungu la Yuda, kwa kuwa fungu la Yuda lilikuwa kubwa kuliko walivyohitaji. Hivyo kabila la Simeoni lilipewa urithi wao ndani ya eneo la Yuda.
西缅人的地业是从犹大人地业中得来的;因为犹大人的分过多,所以西缅人在他们的地业中得了地业。
10 Kura ya tatu ikaangukia kabila la Zabuloni, ukoo kwa ukoo: Mpaka wa urithi wao uliendelea hadi Saridi.
为西布伦人,按着宗族,拈出第三阄。他们地业的境界是到撒立;
11 Kuelekea upande wa magharibi ukafika Marala, ukagusa Dabeshethi, na kuendelea mpaka kwenye bonde karibu na Yokneamu.
往西上到玛拉拉,达到大巴设,又达到约念前的河;
12 Ukageuka mashariki, kuanzia Saridi kuelekea mawio ya jua hadi kwenye nchi ya Kisiloth-Tabori, na kwenda hadi Daberathi, kupanda Yafia.
又从撒立往东转向日出之地,到吉斯绿·他泊的境界,又通到大比拉,上到雅非亚;
13 Kisha ukaendelea mashariki hadi Gath-Heferi na kufika Eth-Kasini, ukatokea Rimoni na kugeuka kuelekea Nea.
从那里往东,接连到迦特·希弗,至以特·加汛,通到临门,临门延到尼亚;
14 Huko mpaka ukazungukia upande wa kaskazini hadi Hanathoni na kuishia katika Bonde la Ifta-Eli.
又绕过尼亚的北边,转到哈拿顿,通到伊弗他·伊勒谷。
15 Miji mingine iliyojumuishwa ni Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala na Bethlehemu. Kulikuwa na miji kumi na miwili pamoja na vijiji vyake.
还有加他、拿哈拉、伸 、以大拉、伯利恒,共十二座城,还有属城的村庄。
16 Miji hii na vijiji vyake ilikuwa ndio urithi wa Zabuloni, ukoo kwa ukoo.
这些城并属城的村庄就是西布伦人按着宗族所得的地业。
17 Kura ya nne ikamwangukia Isakari, ukoo kwa ukoo.
为以萨迦人,按着宗族,拈出第四阄。
18 Eneo lao lilijumuisha: Yezreeli, Kesulothi, Shunemu,
他们的境界是到耶斯列、基苏律、书念、
19 Hafaraimu, Shioni, Anaharathi,
哈弗连、示按、亚拿哈拉、
20 Rabithi, Kishioni, Ebesi,
拉璧、基善、亚别、
21 Remethi, En-Ganimu, En-Hada na Beth-Pasesi.
利篾、隐·干宁、隐·哈大、伯·帕薛;
22 Mpaka ule ukagusa Tabori, Shahasuma na Beth-Shemeshi, na ukaishia kwenye Yordani. Ilikuwa miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.
又达到他泊、沙哈洗玛、伯·示麦,直通到约旦河为止,共十六座城,还有属城的村庄。
23 Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Isakari, ukoo kwa ukoo.
这些城并属城的村庄就是以萨迦支派按着宗族所得的地业。
24 Kura ya tano ikaangukia kabila la Asheri, ukoo kwa ukoo.
为亚设支派,按着宗族,拈出第五阄。
25 Eneo lao lilijumuisha: Helkathi, Hali, Beteni, Akishafu,
他们的境界是黑甲、哈利、比田、押煞、
26 Alameleki, Amadi na Mishali. Upande wa magharibi mpaka uligusa Karmeli na Shihor-Libnathi.
亚拉米勒、亚末、米沙勒;往西达到迦密,又到希曷·立纳,
27 Tena ukageuka mashariki kuelekea Beth-Dagoni, ukagusa Zabuloni na Bonde la Ifta-Eli, ukaenda upande wa kaskazini hadi Beth-Emeki na Neyeli, ukipitia Kabul upande wa kushoto.
转向日出之地,到伯·大衮,达到细步纶;往北到伊弗他·伊勒谷,到伯·以墨和尼业,也通到迦步勒的左边;
28 Ukaendelea hadi Abdoni, Rehobu, Hamoni na Kana, na kufika Sidoni Kuu.
又到义伯 、利合、哈们、加拿,直到西顿大城;
29 Mpaka huo ukageukia nyuma kuelekea Rama na kwenda hadi kwenye mji wenye ngome wa Tiro, ukageuka kuelekea Hosa na kutokeza baharini katika eneo la Akzibu,
转到拉玛和坚固城泰尔;又转到何萨,靠近亚革悉一带地方,直通到海;
30 Uma, Afeki na Rehobu. Ilikuwepo miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake.
又有乌玛、亚弗、利合,共二十二座城,还有属城的村庄。
31 Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa ndio urithi wa kabila la Asheri, ukoo kwa ukoo.
这些城并属城的村庄就是亚设支派按着宗族所得的地业。
32 Kura ya sita ikaangukia kabila la Naftali, ukoo kwa ukoo:
为拿弗他利人,按着宗族,拈出第六阄。
33 Mpaka wao uliendelea kutoka Helefi na kwenye mti mkubwa ulio katika Saananimu, ukipitia Adami-Nekebu na Yabineeli hadi Lakumu, na kuishia katika Mto Yordani.
他们的境界是从希利弗从撒拿音的橡树,从亚大米·尼吉和雅比聂,直到拉共,通到约旦河;
34 Mpaka ukaendelea magharibi kupitia Aznoth-Tabori na kutokea Hukoki. Ukagusa Zabuloni upande wa kusini, Asheri upande wa magharibi, na Yordani upande wa mashariki.
又转向西到亚斯纳·他泊,从那里通到户割,南边到西布伦,西边到亚设,又向日出之地,达到约旦河那里的犹大。
35 Miji yenye ngome ilikuwa Sidimu, Seri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi,
坚固的城就是:西丁、侧耳、哈末、拉甲、基尼烈、
37 Kedeshi, Edrei, na En-Hasori,
基低斯、以得来、隐·夏琐、
38 Ironi, Migdal-Eli, Horemu, Beth-Anathi na Beth-Shemeshi. Kulikuwa na miji kumi na tisa na vijiji vyake.
以利稳、密大·伊勒、和琏、伯·亚纳、伯·示麦,共十九座城,还有属城的村庄。
39 Miji hiyo pamoja na vijiji vyake ndio iliyokuwa urithi wa kabila la Naftali, ukoo kwa ukoo.
这些城并属城的村庄就是拿弗他利支派按着宗族所得的地业。
40 Kura ya saba ikaangukia kabila la Dani, ukoo kwa ukoo.
为但支派,按着宗族,拈出第七阄。
41 Eneo la urithi wao lilijumuisha: Sora, Eshtaoli, Iri-Shemeshi,
他们地业的境界是琐拉、以实陶、伊珥·示麦、
42 Shaalabini, Aiyaloni, Ithla,
沙拉宾、亚雅 、伊提拉、
44 Elteke, Gibethoni, Baalathi,
伊利提基、基比顿、巴拉、
45 Yehudi, Bene-Beraki, Gath-Rimoni,
伊胡得、比尼·比拉、迦特·临门、
46 Me-Yarkoni na Rakoni, pamoja na eneo linalotazamana na Yafa.
美·耶昆、拉昆,并约帕对面的地界。
47 (Lakini Wadani walipata shida kulimiliki eneo lao; kwa hiyo walipanda kuishambulia Leshemu, wakaitwaa, wakawaua watu wake kwa upanga na kuukalia. Walikaa Leshemu na kuuita Dani kufuatana na jina la baba yao.)
但人的地界越过原得的地界;因为但人上去攻取利善,用刀击杀城中的人,得了那城,住在其中,以他们先祖但的名将利善改名为但。
48 Miji hii na vijiji vyake ndio iliyokuwa urithi wa kabila la Dani, ukoo kwa ukoo.
这些城并属城的村庄就是但支派按着宗族所得的地业。
49 Walipomaliza kugawanya nchi katika migawo kulingana na sehemu zao zilizowaangukia, Waisraeli wakampa Yoshua mwana wa Nuni urithi katikati yao,
以色列人按着境界分完了地业,就在他们中间将地给嫩的儿子约书亚为业,
50 kama vile Bwana alivyokuwa ameamuru. Walimpa mji alioutaka, ambao ni Timnath-Sera ulio katika nchi ya vilima ya Efraimu. Naye akajenga mji, akakaa huko.
是照耶和华的吩咐,将约书亚所求的城,就是以法莲山地的亭拿·西拉城,给了他。他就修那城,住在其中。
51 Haya ndiyo maeneo ambayo kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa koo za kabila za Israeli waliyoyagawanya kwa kura huko Shilo mbele za Bwana penye ingilio la Hema la Kukutania. Hivyo wakamaliza kuigawanya nchi.
这就是祭司以利亚撒和嫩的儿子约书亚,并以色列各支派的族长,在示罗会幕门口,耶和华面前,拈阄所分的地业。这样,他们把地分完了。