< Yoshua 18 >

1 Kusanyiko lote la Waisraeli likakusanyika huko Shilo na kusimamisha Hema la Kukutania. Nchi ikawa chini ya utawala wao,
Kisha kusanyiko lote la watu wa Israeli walikusanyika pamoja hapo Shilo. Walilijenga hema la kukutania hapo na waliishinda nchi mbele yao.
2 lakini palikuwa bado makabila saba ya Israeli ambayo yalikuwa hayajapokea urithi wao.
Kulikuwa na makabila saba miongoni mwa watu wa Israeli ambayo yalikuwa bado hayajapewa urithi wao.
3 Hivyo Yoshua akawaambia Waisraeli, “Je, mtasubiri hata lini ili kuingia kumiliki nchi ambayo Bwana, Mungu wa baba zenu, amewapa?
Yoshua aliwaambia watu wa Israeli, “Je mtaacha mpaka lini katika kuingia nchi ambayo Yahweh, Mungu wa baba zenu, amewapeni ninyi?
4 Chagueni watu watatu kutoka kwenye kila kabila. Nitawatuma hao watu kukagua hiyo nchi na kuniandikia mapendekezo ya mgawanyo wa urithi wa kila kabila. Nao watanirudia.
Chagueni ninyi wenyewe watu watatu kutoka katika kila kabila, na nitawatuma. Wataenda na kuipeleleza nchi juu na chini. Wataandika maelezo pamoja na maelekezo kuhusu urithi wao, na kisha watarudi kwangu.
5 Mtaigawanya hiyo nchi katika sehemu saba. Yuda atabaki katika eneo lake upande wa kusini na nyumba ya Yosefu katika nchi yake upande wa kaskazini.
Wataigawanya nchi katika sehemu saba. Yuda itasalia katika eneo lao upande wa kusini, na nyumba ya Yusufu itaendelea katika himaya yao katika upande wa kaskazini.
6 Baada ya kuandika maelezo ya hizo sehemu saba za nchi, yaleteni kwangu, nami nitawapigia kura kwa kura mbele za Bwana Mungu wetu.
Mtaigawanya nchi katika sehemu saba na kisha mtaniletea maelezo hayo hapa kwangu. Nami nitapiga kura kwa ajili yenu hapa mbele za Yahweh Mungu wetu.
7 Hata hivyo, Walawi hawatakuwa na sehemu miongoni mwenu, kwa maana huduma ya ukuhani kwa Bwana ndio urithi wao. Nao Gadi, Reubeni na nusu ya kabila la Manase wameshapata urithi wao upande wa mashariki mwa Yordani, ambako Mose mtumishi wa Bwana aliwapa.”
Walawi hana sehemu miongoni mwenu, kwa kuwa ukuhani wa Yahweh ni urithi wao. Makabila ya Gadi, Rubeni na nusu ya kabila la Manase wameshapokea urithi wao ng'ambo ya Yordani. Huu ni urithi ambao Musa mtumishi wa Yahweh aliwapa wao.
8 Watu hao walipokuwa wanaondoka kwenda kuandika vizuri kuhusu hiyo nchi, Yoshua akawaagiza, “Nendeni mkakague hiyo nchi na mwandike maelezo kuihusu. Kisha mrudi kwangu, nami nitawapigia kura hapa Shilo mbele za Bwana.”
Hivyo, watu waliinuka na wakaenda. Yoshua akawaamuru wale walioenda kuandika maelezo ya nchi, akisema, “Pandeni juu na mshuke chini katika nchi na andikeni maelezo kuhusu nchi na kisha mrejee kwangu. Nitapiga kura kwa ajili yenu hapa mbele za Yahweh huko Shilo.
9 Ndipo hao watu walipoondoka na kupita katika ile nchi. Wakaandika maelezo yake kwenye kitabu, mji kwa mji, katika sehemu saba na kurudisha taarifa kwa Yoshua huko kambini Shilo.
Watu walienda na walitembea juu na chini katika nchi na wakaandika maelezo kuihusu nchi hiyo juu ya gombo kwa miji yake katika sehemu saba, kwa kutaja miji, kila mmoja katika sehemu moja. Kisha wakarudi kwa Yoshua katika kambi huko Shilo.
10 Basi Yoshua akawapigia kura huko Shilo mbele za Bwana, na hapo akagawanya ile nchi kwa Waisraeli kufuatana na mgawanyo wa kabila zao.
Kisha Yoshua akapiga kura kwa ajili yao huko Shilo mbele za Yahweh. Na hapo Yoshua akaigawa nchi kwa watu wa Israeli, kila kabila lilipewa sehemu ya nchi.
11 Kura iliangukia kabila la Benyamini, ukoo kwa ukoo. Eneo lao walilogawiwa lilikuwa kati ya kabila la Yuda na la Yosefu.
Katika kabila la Benyamini, ugawanaji wa nchi ulifanyika kwa kupewa kwa koo zao. Eneo la nchi waliyopewa lilikuwa kati ya wazawa wa Yuda na wazawa wa Yusufu.
12 Upande wa kaskazini mpaka wao ulianzia pale Yordani, kupitia kaskazini ya mteremko wa Yeriko na kuendelea magharibi kuingia katika nchi ya vilima, ukitokea kwenye jangwa la Beth-Aveni.
Katika upande wa kusini, mpaka wao ulianzia katika Yordani. Mpaka ulipanda hata sehemu ya juu kaskazini mwa Yeriko, na kisha ukapita katikati ya nchi ya milima upande wa magharibi. Huko ukafika hadi nyika ya Bethi Aveni.
13 Kutoka hapo ulikatiza kwenye mteremko wa kusini mwa Luzu (yaani Betheli) na kushuka hadi Ataroth-Adari katika kilima kusini mwa Beth-Horoni ya Chini.
Kutoka hapo mpaka ulipita upande wa kusini katika mwelekeo wa Luzi (sehemu ile ile inayoitwa Betheli). Kisha mpaka ukashuka chini hata Atarothi Adda, karibu na mlima uliolekea kusini mwa Bethi Horoni.
14 Kutoka kilima kinachotazamana na Beth-Horoni upande wa kusini mpaka ule ukazunguka kusini kufuatia upande wa magharibi, na ukatokezea Kiriath-Baali (yaani Kiriath-Yearimu), mji wa watu wa Yuda. Huu ndio uliokuwa upande wa magharibi.
Kisha mpaka ukaendelea upande mwingine: katika upande wa magharibi uligeukia upande wa kusini, ulienda mbele kuukabili mlima ulio ng'ambo ya Bethi Horoni. Mpaka huu ulikomea huko Kiriathi Baali ( ambao ndio Kiriathi Yearimu), mji ambao ulikuwa ni wa kabila la Yuda. Na huu ndio ulikuwa ni mpaka katika upande wa magharibi.
15 Upande wa kusini mpaka ulianzia kwenye viunga vya Kiriath-Yearimu kwa upande wa magharibi, nao ukatokeza kwenye chemchemi ya maji ya Neftoa.
Katika upande wa kusini, mpaka ulianzia nje tu ya Kiriathi Yearimu. Mpaka uliendelea kutoka Efroni hata chemichemi ya maji ya Neftoa.
16 Mpaka ukateremka hadi shefela inayotazamana na Bonde la Ben-Hinomu, kaskazini mwa Bonde la Refaimu. Ukaendelea chini kwenye Bonde la Hinomu sambamba na mteremko wa kusini mwa mji mkubwa wa Wayebusi na kisha hadi En-Rogeli.
Kisha mpaka ulishuka chini hadi mpaka wa mlima ambao ulikuwa mkabala ya bonde la Beni Hinomu, ambalo lililokuwa katika upande wa kaskazini mwishoni mwa bonde la Refaimu. Kisha ulishuka chini kuelekea bonde la Hinomu, sehemu ya kusini mwa mteremko wa Wayebusi, na uliendelea kushuka chini hadi Eni Rogeli.
17 Kisha ukapinda kuelekea kaskazini, ukaenda hadi En-Shemeshi na kuendelea mpaka Gelilothi, inayotazamana na Njia ya Adumimu, ukateremka hadi kwenye Jiwe la Bohani mwana wa Reubeni.
Ulizunguka upande wa kaskazini, kuelekea mwelekeo wa Eni Shemeshi, na kutoka hapa ulienda hadi Gelilothi, ambao ulikuwa mkabala na mwinuko wa Adumimu. Kisha ulishuka chini kuelekea Jiwe la Bohani mwana wa Rubeni.
18 Ukaendelea upande wa mteremko wa kaskazini wa Beth-Araba ukateremka hadi Araba.
Ulipita kuelekea upande wa kaskazini wa bega la Bethi Araba na chini kuelekea Araba.
19 Kisha ukaenda mpaka kwenye mteremko wa kaskazini wa Beth-Hogla na kujitokeza kwenye ghuba ya kaskazini ya Bahari ya Chumvi, kwenye maingilio ya Yordani upande wa kusini. Huo ulikuwa mpaka wa kusini.
Mpaka ulipita hadi upande wa bega la kaskazini la Bethi Hogla. Mpaka ulikome katika ghuba ya kaskazini mwa Bahari ya Chumvi, katika upande wa kusini mwishoni mwa Yordani. Huu ulikuwa ni mpaka wa upande wa kusini.
20 Nayo Yordani ikawa ndio mpaka wa upande wa mashariki. Hii ilikuwa ndiyo mipaka iliyoonyesha urithi wa koo za Benyamini pande zote.
Yordani ulikuwa mpaka wake katika upande wa mashariki. Na huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Benyamini, na walipewa kwa kila ukoo wao, mpaka baada ya mpaka, kwa kuizunguka nchi yote.
21 Kabila ya Benyamini, ukoo kwa ukoo, ilikuwa na miji mikubwa ifuatayo: Yeriko, Beth-Hogla, Emeki-Kesisi,
Kwa hiyo sasa miji ya kabila la Benyamini kufuatana na koo zao ilikuwa ni Yeriko,
22 Beth-Araba, Semaraimu, Betheli,
Bethi Hogla, Emeki Kezizi, Bethi Araba, Zemaraimu, Betheli,
23 Avimu, Para na Ofra,
Avimu, Para, Ofra,
24 Kefar-Amoni, Ofni, na Geba; miji kumi na miwili pamoja na vijiji vyake.
Kefari Amoni, Ofini, na Geba. Ilikuwa ni miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake.
25 Gibeoni, Rama na Beerothi,
Kulikuwa pia na miji ya Gibeoni, Rama, Beerothi,
26 Mispa, Kefira, Moza,
Mizpe, Kefira, Moza,
27 Rekemu, Irpeeli, Tarala,
Rekemu, Iripeeli, Tarala,
28 Zela, Elefu, mji wa Wayebusi (yaani Yerusalemu), Gibea na Kiriathi; miji kumi na minne pamoja na vijiji vyake. Huu ndio uliokuwa urithi wa Benyamini kwa ajili ya koo zake.
Zela, Haelefu, Yebusi (ambao ndio Yerusalemu), Gibea, na Kiriathi. Kulikuwa na miji kumi na nne, pamoja na vijiji vyake. Huu ulikuwa ni urithi wa Benyamini kufuatana na koo zao.

< Yoshua 18 >