< Yoshua 15 >

1 Mgawo kwa kabila la Yuda, ulienea ukoo kwa ukoo, ukishuka kufikia eneo la Edomu, hadi Jangwa la Sini mwisho kabisa upande wa kusini.
Ugawanaji wa nchi kwa kabila la watu wa Yuda, walipewa kwa kufuatana na koo zao, kutoka upande wa kusini hadi mpaka wa Edomu, pamoja na nyika ya Sini iliyokuwa mbali sana kuelekea kusini.
2 Mpaka wao wa kusini ulianzia kwenye ghuba iliyoko kwenye ncha ya kusini mwa Bahari ya Chumvi,
Mpaka wao wa upande wa kusini ulianzia mwisho wa Bahari ya Chumvi, kutoka ghuba iliyokabili upande wa kusini.
3 ukakatiza kusini mwa Akrabimu, ukaendelea hadi Sini ukaenda hadi kusini mwa Kadesh-Barnea. Tena ukapitia Hesroni ukapanda hadi Adari na ukapinda hadi Karka.
Mpaka wao mwingine ulielekea upande wa kusini wa mlima wa Akrabimu na kupita kuelekea Sini, na kupanda upande wa Kadeshi Barnea, karibu na Hezroni, hadi Addari mahali ambapo ulipinda kuelekea Karika.
4 Kisha ukaendelea mpaka Azmoni na kuunganika na Kijito cha Misri, na kuishia baharini. Huu ndio mpaka wao wa upande wa kusini.
Ulipita katika Azimoni, kuelekea kijito cha Misri, na mwisho ulikuwa katika bahari. Huu ulikuwa ni mpaka wa kusini.
5 Mpaka wa upande wa mashariki ni Bahari ya Chumvi ukienea mahali Mto Yordani unapoingilia. Mpaka wa upande wa kaskazini ulianzia penye ghuba ya bahari mahali Mto Yordani unapoingilia,
Mpaka wa mashariki ulikuwa ni Bahari ya Chumvi, katika mdomo wa Yordani. Mpaka wa upande wa kasikazini ulianzia katika ghuba ya bahari katika mdomo wa Yordani.
6 ukapanda hadi Beth-Hogla, na kuendelea kaskazini mwa Beth-Araba hadi kwenye Jiwe la Bohani mwana wa Reubeni.
Ulielekea mpaka Bethi Hogla na ulipita kaskazini mwa Bethi Araba. Kisha ulipanda hata JIwe la Bohani mwana wa Rubeni.
7 Kisha mpaka ulipanda hadi Debiri kutoka Bonde la Akori na kugeuka kaskazini hadi Gilgali inayotazamana na materemko ya Adumimu, kusini mwa bonde. Ukaendelea sambamba hadi maji ya En-Shemeshi na kutokeza huko En-Rogeli.
Basi mpaka ule ulienda hadi Debiri kutoka katika bonde la Akori, kuelekea upande wa kasikazini, kuendelea hadi Giligali, ambayo iko mkabala na mlima Adumimu, iliyo upande wa kusini wa bonde. Kisha mpaka uliendelea hata katika chemichemi za Eni Shemeshi na kufika Eni Rogeli.
8 Kisha ukapanda kwa kufuata Bonde la Ben-Hinomu sambamba na mteremko wa kusini wa mji mkubwa wa Wayebusi (yaani Yerusalemu). Kutoka hapo ukapanda juu ya kilima magharibi ya Bonde la Hinomu mwisho wa ncha ya kaskazini mwa Bonde la Warefai.
kisha mpaka ulishuka hadi bonde la Beni Hinomu kuelekea upande wa kusini wa mji wa Wayebusi ( ambao ni Yerusalemu). Kisha ulipanda hata katika mlima ulio juu ya bonde la Hinomu, katika upande wa magharibi, ulio mwishoni mwa bonde la Refaimu katika upande wa kasikazini.
9 Kutoka juu ya kilima mpaka ule ukaendelea hadi kwenye chemchemi ya maji ya Neftoa, ukatokea kwenye miji ya Mlima Efroni na kuteremka kuelekea Baala (yaani Kiriath-Yearimu).
Kisha mpaka ulitanuka kutoka katika kilele cha milima hata chemichemi ya Nefutoa, na ulipanda kutoka hapo kuelekea miji ya Mlima Efroni. Kisha mpaka ulipiga kona kuelekea Baala ( ambao ndio Kiriathi Yearimu).
10 Kisha ukapinda upande wa magharibi kutoka Baala hadi Mlima Seiri, ukafuatia sambamba mteremko wa kaskazini mwa Mlima Yearimu (yaani Kesaloni), ukaendelea chini hadi Beth-Shemeshi na kukatiza hadi Timna.
Baadaye mpaka ulizunguka kuelekea magharibi mwa Baala kukabili Mlima Seiri, na kupita kufuata upande wa Mlima wa Yearimu katika upande wa kasikazini (ambao ndio Kesaloni), ulienda chini hadi Bethi Shemeshi na kuvuka hata ng'ambo ya Timna.
11 Ukaelekea hadi kwenye mteremko wa kaskazini mwa Ekroni, ukageuka kuelekea Shikeroni, ukapita hadi Mlima Baala na kufika Yabineeli. Mpaka ule ukaishia baharini.
Mpaka uliendelea karibu na mlima wa kasikazini mwa mlima wa Ekroni, na kisha ukakata kona kuzunguka Shikeroni na kupita kuelekea sambasamba na Mlima Baala, kutoka hapo uliendelea hadi Yabneeli. Mpaka ule ulikomea katika bahari.
12 Mpaka wa magharibi ni pwani ya Bahari Kuu. Hii ndiyo mipaka ya watu wa Yuda kwa koo zao.
Mpaka wa magharibi ulikuwa Bahari Kuu na katika ukanda wa pwani yake. Huu ndio mpaka uliozunguka kabila la Yuda, ukoo kwa ukoo.
13 Kwa kufuata maagizo ya Bwana kwake, Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune sehemu katika Yuda: Kiriath-Arba, yaani Hebroni (Arba alikuwa baba wa zamani wa Anaki).
Katika kulitunza agizo la Yahweh kwa Yoshua, Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune mgao wa nchi ya. miongoni mwa kabila la Yuda, alimgawia nchi Kiriathi Arba, ambayo ndio Hebroni (Arba alikuwa ni baba wa Anaki).
14 Kutoka Hebroni Kalebu alifukuza hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, Ahimani na Talmai, wazao wa Anaki.
Kalebu aliwafukuzia mbali wana watatu wa Anaki: Sheshai, Ahimani na Talmai, wazawa wa Anaki.
15 Kutoka hapo akaondoka kupigana dhidi ya watu walioishi Debiri (jina la Debiri hapo kwanza uliitwa Kiriath-Seferi).
Alipanda kutoka pale kinyume cha wenyeji wa Debiri (Debiri hapo mwanzo iliitwa Kiriathi Seferi).
16 Kalebu akasema, “Nitamwoza binti yangu Aksa kwa mtu atakayeweza kupigana na kuteka Kiriath-Seferi.”
Kalebu akasema, “Mtu atakayeishambulia Kiriathi Seferi na kuiteka, nitampa binti yangau, Akisa, awe mke wake.
17 Basi Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu yake Kalebu, akauteka; hivyo Kalebu akamtoa Aksa binti yake aolewe naye.
Wakati huo Othinieli mwana wa Kenazi, kaka yake na Kalebu, aliuteka mji, na Kalebu alimpatia Akisa, binti yake awe mke wake.
18 Siku moja Aksa alipokuja kwa Othnieli, alimsihi Othnieli amwombe baba yake, Kalebu, shamba. Aksa aliposhuka kutoka juu ya punda wake, Kalebu akamuuliza, “Je, wataka nikufanyie nini?”
Mara baada ya hayo, Akisa alienda kwa Othinieli na alimsihi amwombe baba yake shamba. Na mara aliposhuka kutoka katika punda wake, Kalebu alimwambia Akisa, “Unataka nini?”
19 Akamjibu, “Naomba unifanyie jambo moja la hisani. Kwa kuwa umenipa ardhi huko Negebu, nipe pia chemchemi za maji.” Basi Kalebu akampa chemchemi za juu na za chini.
Akisa akamjibu, “Nifanyie neema. Kwa kuwa umeshanipa nchi ya Negevu, nipe pia baadhi ya chemichemi za maji.” Na Kalebu alimpa chemichemi ya juu na chemichemi ya chini.
20 Huu ndio urithi wa kabila la Yuda, ukoo kwa ukoo:
Huu ulikuwa ndio urithi wa kabila la Yuda, waliopewa kufuatana na koo zao.
21 Miji ya kusini kabisa ya kabila la Yuda katika Negebu kuelekea mpaka wa Edomu ilikuwa: Kabseeli, Ederi, Yaguri,
Miji iliyo mali ya kabila la Yuda katika upande wa kusini, kuelekea mpaka wa Edomu, ilikuwa ni Kabzeeli, Eda, Yaguri,
22 Kina, Dimona, Adada,
Kina, Dimona, Adada,
23 Kedeshi, Hazori, Ithnani,
Kadeshi, Hazor, Ithinani,
24 Zifu, Telemu, Bealothi,
Zifu, Telemu, Bealothi.
25 Hazor-Hadata, Kerioth-Hezroni (yaani Hazori),
Hazori Hadata, Keriothi Hezroni (mji huu ulijulikana kama Hazori),
26 Amamu, Shema, Molada,
Amamu, shema, Molada,
27 Hasar-Gada, Heshmoni, Beth-Peleti,
Hazari Gada, Heshimoni, Bethi Peleti,
28 Hasar-Shuali, Beer-Sheba, Biziothia,
Hazari Shuali, Beerisheba, Biziothia.
29 Baala, Iyimu, Esemu,
Baala, Limu, Ezemu,
30 Eltoladi, Kesili, Horma,
Eltoladi, Kesili, Horma,
31 Siklagi, Madmana, Sansana,
Ziklagi, Madimana, Sansana,
32 Lebaothi, Shilhimu, Aini na Rimoni; hiyo yote ni miji ishirini na tisa, pamoja na vijiji vyake.
Lebaothi, Shilihimu, Aini, na Rimoni. Miji hii ilikuwa ishirini na tisa kwa ujumla, kujumlisha na vijiji vyake.
33 Kwenye shefela ya magharibi: Eshtaoli, Sora, Ashna,
Katika nchi iliyo chini ya mlima upande wa magharibi, kulikuwa na miji ya Eshtaoli, Zora, Ashina,
34 Zanoa, En-Ganimu, Tapua, Enamu,
Zanaoa, Eni Ganimu, Tapua, Enamu,
35 Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka,
Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka,
36 Shaaraimu, Adithaimu na Gedera (au Gederothaimu); yote ni miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake.
Shaaraimu, Adithaimu, na Gedera ( ambayo ndio Gederothaimu). Hesabu ya miji hii ilikuwa ni kumi na nne, pamoja na vijiji vyao.
37 Senani, Hadasha, Migdal-Gadi,
Zena, Hadasha, Migidagadi,
38 Dileani, Mispa, Yoktheeli,
Dileani, Mizipa, Yokitheeli,
39 Lakishi, Boskathi, Egloni,
Lakishi, Bozikathi, Egloni.
40 Kaboni, Lamasi, Kitlishi,
Kaboni, Lahmamu, Kitilishi,
41 Gederothi, Beth-Dagoni, Naama na Makeda; yote ni miji kumi na sita pamoja na vijiji vyake.
Gederothi, Bethi Dagoni, Naama, Makeda. Hesabu ya miji hii ilikuwa kumi na sita, kujumlisha na vijiji vyao.
42 Libna, Etheri, Ashani,
Libna, Etheri, Ashani,
43 Yifta, Ashna, Nesibu,
Ifuta, Ashina, Nezibu,
44 Keila, Akzibu na Maresha; yote ni miji tisa pamoja na vijiji vyake.
Keila, Akizibu, na Maresha. Hii ilikuwa ni miji tisa, kujumlisha na vijiji vyao.
45 Ekroni, pamoja na viunga vyake na vijiji vyake;
Ekroni, pamoja na miji na vijiji vyake vinavyoizunguka;
46 magharibi ya Ekroni, maeneo yote yaliyokuwa karibu na Ashdodi, pamoja na vijiji vyake;
kutoka Ekroni kuelekea Bahari Kuu, makazi yote ambayo yalikuwa karibu na Ashidodi, pamoja na vijiji vyake.
47 Ashdodi, miji yake na vijiji vyake na Gaza viunga vyake na vijiji vyake, hadi kufikia Kijito cha Misri na Pwani ya Bahari Kuu.
Ashidodi, na miji na vijiji vyake vinavyoizunguka; Gaza na miji na vijiji vyake vinavyoizunguka; hata kufika kijito cha Misri, na kuelekea Bahari Kuu pamoja na ukanda wake wa pwani.
48 Katika nchi ya vilima: Shamiri, Yatiri, Soko,
Katika nchi ya milima, kuna miji ya Shamiri, Yatiri, Soko,
49 Dana, Kiriath-Sana (yaani Debiri),
Dana, Kiriathi Sana (ambayo ndio Debiri),
50 Anabu, Eshtemoa, Animu,
Anabu, Eshitemo, Animu,
51 Gosheni, Holoni na Gilo; miji kumi na mmoja pamoja na vijiji vyake.
Gosheni, Holoni, na Gilo. Hii ilikuwa ni miji kumi na moja, kujumuisha na vijiji vyake.
52 Arabu, Duma, Ashani,
Arabu, Duma, Ehani,
53 Yanimu, Beth-Tapua, Afeka,
Yanimu, Bethi Tapua, Afeka,
54 Humta, Kiriath-Arba (yaani Hebroni), na Siori; miji tisa pamoja na vijiji vyake.
Humta, Kiriathi Arba (ambayo ndio Hebroni), na Ziori. Hii ilikuwa miji tisa, pamoja na vijiji vyake.
55 Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta,
Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta,
56 Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa,
Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa,
57 Kaini, Gibea na Timna; miji kumi pamoja na vijiji vyake.
Kaini, Gibea, na Timna. Hii ilikuwa ni miji kumi, kujumuisha na vijiji vyake.
58 Halhuli, Beth-Suri, Gedori,
Halhuli, Bethi Zuri, Gedori,
59 Maarathi, Beth-Anothi na Eltekoni; miji sita pamoja na vijiji vyake.
Maarathi, Bethi Anothi, na Elitekoni. Hii ilikuwa miji sita, pamoja na vijiji vyake.
60 Kiriath-Baali (yaani Kiriath-Yearimu) na Raba; miji miwili pamoja na vijiji vyake.
Kiriathi Baali (ambayo ndio Kiriathi Yearimu), na Raba. Hii ilikuwa ni miji miwili, pamoja na vijiji vyake.
61 Huko jangwani: Beth-Araba, Midini, Sekaka,
Katika nyika, kulikuwa na miji ya Bethi Araba, Midini, Sekaka,
62 Nibshani, Mji wa Chumvi, na En-Gedi; miji sita pamoja na vijiji vyake.
Nibushani, mji wa chumvi, na Eni Gedi. Hii ilikuwa miji, pamoja na vijiji vyao.
63 Yuda hakuweza kuwafukuza Wayebusi, waliokuwa wakiishi Yerusalemu; hadi leo Wayebusi huishi huko pamoja na watu wa Yuda.
Lakini kwa Wayebusi, wenyeji wa Yerusalemu, kabila la Yuda halikuweza kuwafukuza, na hivyo, Wayebusi wanaishi pamoja na kabila la Yuda hadi leo hii.

< Yoshua 15 >