< Yoshua 14 >

1 Basi haya ndiyo maeneo Waisraeli waliyopokea kama urithi katika nchi ya Kanaani, ambayo kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni na viongozi wa koo za kabila za Israeli waliwagawia.
Maeneo haya ya nchi ambayo watu wa Israeli waliyapokea kama urithi wao katika nchi ya Kanaani. Urith huu uligawanywa kwao na Eliazeri kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa makabila ya mababu wa familia zao kati ya watu wa Israeli.
2 Urithi wao uligawanywa kwa kura kwa yale makabila tisa na nusu, kama Bwana alivyoamuru Mose.
Urithi wao ulichaguliwa kwa kupiga kura kwa makabila tisa na nusu, kama vile Yahweh alivyoagiza kwa mkono wa Musa.
3 Mose alikuwa amewapa yale makabila mawili na nusu urithi wao upande wa mashariki mwa Yordani, lakini Walawi hawakupewa urithi miongoni mwa hao wengine,
Kwa kuwa Musa alikuwa amewapa urithi makabila mawili na nusu ng'ambo ya Yordani, lakini Walawi hawakupewa urithi wowote.
4 kwa kuwa wana wa Yosefu walikuwa makabila mawili; Manase na Efraimu. Walawi hawakupata mgawo wa ardhi, bali walipewa miji tu kwa ajili ya kuishi, pamoja na maeneo ya malisho kwa ajili ya makundi yao ya kondoo, mbuzi na ngʼombe wao.
Kabila la Yusufu kwa uhalisia yalikuwa makabila mawili, Manase na Efraimu. Na hakuna sehemu yoyote ya urithi waliyopewa Walawi katika nchi, lakini walipewa miji ya kuishi ndani yake pamoja na sehemu ya malisho ya mifugo yao na kwa ajili ya riziki zao.
5 Kwa hiyo Waisraeli wakagawana ile nchi, kama vile Bwana alivyomwagiza Mose.
Watu wa Israeli walifanya hivyo kama vile Yahweh alivyomwagiza Musa, basi waliiganywa nchi.
6 Kisha watu wa Yuda wakamwendea Yoshua huko Gilgali, naye Kalebu mwana wa Yefune yule Mkenizi, akamwambia, “Unajua jambo ambalo Bwana alimwambia Mose mtu wa Mungu huko Kadesh-Barnea kukuhusu wewe na mimi.
Kisha kabila la Yuda lilikuja kwa Yoshua huko Giligali. Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi, akamwambia,”Unajua kile Yahweh alichomwambia Musa mtu wa Mungu juu yako na mimi huko Barnea.
7 Nilikuwa na umri wa miaka arobaini, wakati Mose mtumishi wa Bwana, aliponituma kutoka Kadesh-Barnea kuipeleleza hiyo nchi. Nami nikamletea taarifa kama kulingana na nilivyosadiki moyoni.
Nilikuwa na umri wa miaka arobani wakati Musa mtumishi wa Yahweh aliponituma kutoka Kadeshi Barnea kuipeleleza nchi. Nilimletea taarifa tena kama nilivyotakiwa kufanya katika moyo wangu.
8 Lakini ndugu zangu tuliopanda nao waliifanya mioyo ya watu iyeyuke kwa hofu. Bali mimi, nilimfuata Bwana Mungu wangu kwa moyo wote.
Lakini ndugu zangu walioenda pamoja nami waliifanya mioyo ya watu iyeyuke kwa woga. Lakini mimi nilimfuata Yahweh kabisa.
9 Hivyo katika siku ile, Mose akaniapia, ‘Nchi ambayo umeikanyaga kwa miguu yako itakuwa urithi wako na wa watoto wako milele, kwa sababu umemfuata Bwana Mungu wangu kwa moyo wote.’
Musa aliapa katika siku hiyo akisema, “Hakika nchi ambayo miguu yako imetembea juu yake itakuwa urithi wako na kwa watoto wako milele, kwasababu umemfuata kabisa Yahweh Mungu wangu.
10 “Sasa basi, kama vile Bwana alivyoahidi, ameniweka hai kwa miaka arobaini na mitano tangu wakati alipomwambia Mose jambo hili, wakati Waisraeli wakiwa wanazunguka jangwani. Hivyo mimi hapa leo, nina umri wa miaka themanini na mitano!
Tazama! sasa, Yahweh amenihifadhi hai kwa miaka hii arobaini na tano, kama alivyosema - tangu kipindi kile Yahweh alivyomwambia Musa neno hili, wakati huo Waisraeli walikuwa wakitembea jangwani. Tazama! sasa katika siku hii ya leo nina miaka themanini na mitano.
11 Bado ninazo nguvu kama siku ile Mose aliponituma. Bado ninazo nguvu za kwenda vitani sasa kama vile nilivyokuwa wakati ule.
Bado hata siku hii ya leo nina nguvu kama nilivyokuwa katika siku ile ambayo Musa alinituma. Nguvu zangu za sasa ni sawa na nguvu zangu za kipindi kile, kwa ajili ya vita na kwa kwenda na kwa kuja.
12 Basi nipe nchi hii ya vilima, ambayo Bwana aliniahidi siku ile. Wewe mwenyewe ulisikia wakati ule kwamba Waanaki walikuwako huko na miji yao ilikuwa mikubwa na yenye maboma, lakini, kwa msaada wa Bwana, nitawafukuza watoke huko kama vile alivyonena.”
Sasa basi, nipe nchi hii ya milima, ambayo Yahweh aliniahidi katika siku hiyo. Kwa kuwa ulisikia katika siku hiyo kuwa Wanakimu walikuwa huko katika miji yenye ngome. Itakuwa kwamba Yahweh atakuwa pamoja nami na ya kwamba nitawafukuzia mbali, kama vile Yahweh alivyosema.”
13 Ndipo Yoshua akambariki Kalebu mwana wa Yefune, na akampa Hebroni kama urithi wake.
Kisha Yoshua alimbariki Kalebu mwana wa Yefune na alimpa Hebroni kama urithi wake.
14 Hivyo Hebroni imekuwa mali ya Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi tangu wakati ule, kwa sababu alimwandama Bwana, Mungu wa Israeli, kwa moyo wote.
Hivyo Hebroni ikawa urithi wa Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi hata leo, kwasababu alimfuata kabisa Yahweh, Mungu wa Israeli.
15 (Hebroni uliitwa Kiriath-Arba hapo mwanzo, kutokana na huyo Arba ambaye alikuwa mtu mkuu kupita wote miongoni mwa Waanaki.) Kisha nchi ikawa na amani bila vita.
Basi, jina la Hebroni hapo mwanzo lilikuwa ni Kiriathi Arba ( Arba ambaye alikuwa ni mtu mkuu miongoni mwa Wanakim). Kisha nchi ikawa na raha bila vita.

< Yoshua 14 >