< Yoshua 12 >
1 Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:
Basi hawa ndio wafalme wa nchi, ambao watu wa Israeli walishindwa. Waisraeli walichukua miliki ya nchi katika upande wa mashariki mwa Yordani sehemu ambako jua huchomoza, kutoka bonde la Mto Arnoni hadi Mlima Hermoni, na nchi yote ya Araba kuelekea kusini.
2 Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni. Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi.
Sihoni, mfalme wa Waamori, aliishi katika Heshiboni. Alitawala kutoka Aroeri, ambayo iko juu ya bonde la Arnoni kutoka katikati ya bonde, na nusu ya Geleadi kushuka mpaka Mto Yaboki katika mpaka wa Waamori.
3 Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga.
Sihoni pia alitawala juu ya Araba mpaka Bahari ya Kinerethi, kwenda mashariki, kuelekea Bahari ya Araba (Bahari ya Chumvi) upande wa mashariki, hadi huko Bethi Yeshimothi na upande wa kusini, kuelekea chini ya miteremko wa Mlima Pisiga.
4 Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.
Ogu, mfalme wa Bashani, mmoja kati ya mabaki ya Rephaimu, aliyeishi huko Shatarothi na Edrei.
5 Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.
Alitawala juu ya Mlima Hermoni, Saleka, na Bahani yote, hadi mpaka wa watu wa Geshuri na Wamakathi, na nusu ya Gleadi, hadi kufika mpaka wa Sihohi, mfalme wa Heshboni.
6 Mose, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.
Musa mtumishi wa Yahweh, na watu wa Israeli walikuwa wamewashinda, na Musa mtumishi wa Yahweh aliwapa nchi kama mali ya Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase.
7 Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao:
Hawa ndio wafalme wa nchi ambayo Yoshua na watu wa Israeli waliwashinda katika upande wa magharibi mwa mto Yordani, kutoka Baali Gadi katika bonde karibu na Lebanoni hadi Mlima Halaki karibu na Edom. Yoshua aliyapa nchi makabila ya Israeli ili yaimiliki.
8 nchi ya vilima, shefela, upande wa magharibi, Araba, materemko ya milima, jangwa, na Negebu; nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi):
Aliwapa nchi ya milima, tambarare, Araba, sehemu za milima, nyika na Negevu, nchi ya Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi.
9 mfalme wa Yeriko mmoja mfalme wa Ai (karibu na Betheli) mmoja
Wafalme hawa walikuwa ni mfalme wa Yeriko, mfalme wa Ai iliyo karibu na Betheli,
10 mfalme wa Yerusalemu mmoja mfalme wa Hebroni mmoja
mfalme wa Yerusalemu, mfalme wa Enaimu,
11 mfalme wa Yarmuthi mmoja mfalme wa Lakishi mmoja
mfalme wa Yarmuthi, mfalme wa Lakishi,
12 mfalme wa Egloni mmoja mfalme wa Gezeri mmoja
mfalme wa Egloni, mfalme wa Gezeri,
13 mfalme wa Debiri mmoja mfalme wa Gederi mmoja
mfalme wa Debiri, mfalme wa Gederi,
14 mfalme wa Horma mmoja mfalme wa Aradi mmoja
mfalme wa Horima, mfalme wa Aradi,
15 mfalme wa Libna mmoja mfalme wa Adulamu mmoja
mfalme wa Libna, mfalme wa Adula,
16 mfalme wa Makeda mmoja mfalme wa Betheli mmoja
mfalme wa Makeda, mfalme wa Betheli,
17 mfalme wa Tapua mmoja mfalme wa Heferi mmoja
mfalme wa Tapua, mfalme wa Heferi,
18 mfalme wa Afeki mmoja mfalme wa Lasharoni mmoja
mfalme wa Afeki, mfalme wa Lasharoni,
19 mfalme wa Madoni mmoja mfalme wa Hazori mmoja
mfalme wa Madoni, mfalme wa Hazori,
20 mfalme wa Shimron-Meroni mmoja mfalme wa Akishafu mmoja
mfalme wa Shimroni - Meroni, mfalme wa Akshafu.
21 mfalme wa Taanaki mmoja mfalme wa Megido mmoja
mfalme wa Taanaki, mfalme wa Megido,
22 mfalme wa Kedeshi mmoja mfalme wa Yokneamu katika Karmeli mmoja
mfalme wa Kedeshi, mfalme wa Jokineamu katika Karmeli,
23 mfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori) mmoja mfalme wa Goimu katika Gilgali mmoja
mfalme wa Dori katika Nafutali Dori, mfalme Goyimu katika Giligali, na
24 mfalme wa Tirsa mmoja wafalme jumla yao ilikuwa thelathini na mmoja.
mfalme Tiriza. Hesabu ya wafalme ilikuwa ni thelathini na moja kwa ujumla wake.